WAZIRI wa Uchukuzi Omary Nundu amesema kuwa serikali haitaweza kutoa fedha za kuendesha na kufufua Kampuni ya Reli Nchini (TRL) hadi pale uongozi utakapobadilishwa.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Uchukuzi ilisema kuwa Nundu alitoa kauli hiyo katika ziara ya siku moja mkoani Morogoro akiwa ameambatana na Naibu wake Athman Mfutakamba.
Ilisema kuwa ni lazima uongozi ubadilishwe na kuwekwa mwingine madhubuti ndipo fedha hizo zitolewe na kuwa zoezi hilo linahitajika kutekelezwa mapema.