Serikali haistahili kuwepo Dar, iuze majengo ikamalizie Dodoma

Iga

Senior Member
Dec 17, 2007
112
6
NAIPONGEZA serikali ya chama cha mapinduzi (CCM) kwa kuizawadia hoteli ya Kempinsky zawadi ya eneo la mahakama.

Ninaamini serikali yetu ipo kwenye mji usiostahili kuwepo, na kutokana na hili utendaji wa watendaji wake unakuwa wakibabaishaji (kiasi cha kushindwa hata kuandika vizuri bajeti ya taifa kiwizara) na kwa upande mwingine serikali hiyo na Ikulu yake leo ni mwiba kwa wakazi wa jiji kutokana na kuwachelewesha asubuhi, mchana na usiku kutokana na kuwa na misafara inayolazimisha wao kusimama kwa masaa kila siku kuwapisha waheshimiwa wapite.

Ninaamini huu ni uamuzi sahihi na ambao umecheleweshwa sana. Na isitoshe eneo lote la maofisi ya serikali pale Kivukoni ni vizuri likauzwa kwa bei nzuri (ambayo ninaamini itakuwa ni matrilioni ya shilingi za Kitanzania) ili fedha ipatikane siyo tu ya kumalizia Makao Makuu Dodoma na kutuondolea foleni tusizozihitaji katika jiji hili ambalo ndio Makao Makuu ya nchi KIBIASHARA na sio kisiasa. Kama CCM inaona Dodoma mbali basi Makao Makuu ya Kisiasa yawe Kibaha au Chalinze au Bwawani kama sio Morogoro kabisa.

Dar es salaam pawe na ghorofa moja tu kubwa ambayo itakuwa na ofisi ndogo za wizara zote.

Ikulu yetu imepitwa na wakati. Pauzwe na pajengwe hoteli ya Kitalii kwa ushirikiano na Benki ya Jamii Dar es salaam (Dar es salaam Community Bank) na CRDB Bank na wapenda kujenga wa NSSF. Hoteli hiyo itakayojengwa katika eneo la Ikulu itatusaidia kuepukana na gharama za Mawaziri wapya kukaa hoteli za bei mbaya za Kitalii, kwani nusu ya shea za Tanzania One International Hotel zitakuwa ni za serikali, robo za vyama vya Kisiasa na robo iliyobakia kwa wananchi wa kawaida.

BILA mzaha, majengo ya serikali ya JMT Dar yameoza na sasa ni tishio kwa maisha ya waliomo humo. Yauzwe. Tubadilishe sura ya jiji letu ili liwe na hadhi angalau moja ya kumi ya Kuala Lumpur!!!

iga,
mzizima.
 
tungekuwa na mawaziri angalau watatu ndani ya serikali hii wenye mawazo kama yako, kwa kweli Tanzania ingekuwa imeshapiga hatua kubwa sana. tatizo la Serikali ya kikwete wapowapo tu wanasubiri kila kitu washinikizwe na CHADEMA.
 
Back
Top Bottom