Serikali haioni fursa katika mbio za baiskeli?

INNOMATIX

Senior Member
Aug 24, 2013
113
47
Habari wana jamvi, natumai ni wazima kadri ya Mungu alivyowajalia.
Tanzania ni nchi yetu, twaipenda.Usipoipenda utapenda nchi gani tena.
Leo nakuja na hii mada ambayo sio ngeni ila ni mada ambayo imewekwa kapuni kwa muda mwingi na kuweka mkazo katika michezo mingine, serikali ikitumia pesa nyingi huku mrejesho wake ukiwa mdogo.
Naongelea mbio za baiskeli.Labda niseme mimi ni moja ya watu wengi waliofanikiwa kuishi katika jiji la mwanza na kutembea maeneo kadhaa haswa sehemu inayoitwa misungwi (waliowahi kwenda wananielewa vizuri).Mara ya kwanza kwenda pale nilishangaa, sio kwa kuwa hakuna boda boda au usafiri mwingine bali watu hupendelea sana usafiri wa baiskeli kutoka sehemu moja kwenda nyingine, waendesha baiskeli hudai malipo ya kati ya sh.200 na 400, inategemea na umbali wa sehemu yenyewe.Nikasema nijaribu na mimi kutumia huu usafiri huku lengo ni kutaka kujua kwa siku anaweza kutengeneza shilingi za kitanzania kiasi gani.Hapo ndipo aliponiduwaza zaidi.kwa sh.200 anaweza kutengeneza elfu 10 mpaka ishirini kwa siku, hiyo ina maana ni safari 50 mpaka 100 kwa siku na ni za mwenda wa kilometa 2 hata 5 kila safari hii inamaana huyu mtu anaweza kutembea kwa baiskeli kila siku kwa zaidi ya kilometa100.....

SWALI:serikali haioni hii fursa,kuwatumia hawa watu na wengine wa aina hii kuleta heshima ya nchi katika michezo?
Ni wazi michezo mingine imekuwa haileta matokeo tunayoyatarajia licha ya kutumia pesa nyingi katika maandalizi yake.Ni wakati sasa wa serikali kupitia wizara yake ya sanaa, utamaduni na michezo kutupia jicho huu mchezo, kuwakusanya hawa watu, kuwapa mafunzo na kuwaaminisha wanaweza kupeperusha vyema bendera ya taifa letu.....
Nakaribisha maoni.
 
Back
Top Bottom