Victor Mlaki
JF-Expert Member
- May 1, 2016
- 4,739
- 4,933
MAHITAJI YA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI TANZANIA NI MZIGO WETU SOTE NA SIYO SERIKALI PEKE YAKE.
Kutokana na ukweli kuwa hakuna jipya chini ya jua. Leo baada ya kufuatilia maadhimisho ya siku ya kimataifa ya wafanyakazi Duniani nililazimika kukaa katika maktaba yangu nyumbani na kutafuta kitabu ambacho kiingeweza kunionesha mtazamo wa Taifa ulivyokuwa mwanzo na kinachofanyika leo. Kwa haraka nilikiona Kitabu cha UJAMAA" Kilichoandikwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mwaka 1968 na nilijaribu kukipitia hususan kuanzia uk 17-25 ndipo nilipopata mawazo na msukumo wa kuandika haya unayoyasoma.
Kuna kosa kubwa ambalo Taifa letu lilishalifanya juu ya kuchagu silaha ya kupambana na unyonge wetu. Kosa hili mpaka leo linaendelea licha ya miaka mingi kupita. Ni kama tulikosea na tukaamua kuendelea kukosea. TUCTA walichokitamka leo kama hitaji la wafanyakazi siyo kipya ila ni7 muendelezo wa kosa lile lile.
Katika kitabu hiki cha Ujamaa uk. 17 na 18 "...ni dhahiri kwamba tumefanya makosa katika kuchagua silaha; kwani silaha tuliyoichagua ni fedha. Tunataka kuondoa unyonge wetu kwa kutumia silaha ambayo sisi wenyewe hatuna. Katika mawazo yetu na vitendo vyetu ni kama tumemkata shauri kwamba bila fedha mapinduzi Mapinduzi haiwezekani. Ni kama tumesema Fedha ndiyo msingi wa maendeleo. Bila fedha hakuna maendeleo".
Ukiangalia kwa kina utagundua hali hii leo umekuwa kama imani kwa viongozi wa Serikali, wanasiasa na watumishi. Maombi makuu kwa Serikali ni "FEDHA". Ni kama tumeafikiana kuwa "Tukipata fedha tutaendelea, bila fedha hatutaendelea".
Mbunge akisimama bungeni kuwakilisha wananchi anaowaongoza hutaja mipango inayoitaka Serikali kutoa fedha. Kiongozi wa chama au shirikisho la wafanyakazi mara kadhaa huikumbusha Serikali kuongeza kima cha mishahara na kuboresha miundombinu ya kazi ambayo kwa kweli huhitaji fedha.
Mawaziri kila mwaka hufanya makadirio ya matumizi na kuonesha fedha wanazohitaji ili kutekeleza mipango ya maendeleo isipokuwa Waziri mmoja tu, Waziri wa fedha ambaye hushughulika na hesabu za makadirio ya mapato. Hi ni sawa na kusema wengine wote wao hufanya hesabu za makadirio ya matumizi.
Serikali kusema haina fedha siyo jibu jipya. Katika kitabu hiki cha Ujamaa( uk.20) "...kusema Serikali haina fedha maana yake Wananchi hawana fedha". Kumbe tunaposema fedha maana yake zipo mifuko I mwa wanachi na tunapoidai Serikali fedha zaidi ni sawa na kutaka fedh tulizo nazo sisi (yaani, mimi na wewe) zitumike zaidi.
Kwa maana nyingine tunapohitaji serikali itoe fedha zaidi ni sawa na kukubali kuwa kiasi cha kodi inayochukua serikali ni kidogo mno na hakiwezi kuendesha masuala mengi yanayohitaji fedha, hivyo iongeze kututoza kodi mara dufu. Ni ngumu kulipokea hili lakini lilishasemwa na ndivyo ilivyo.
Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambrage Nyerere aliutoa pia mfano huu "..kukataa kodi na kutaka Serikali iongeze fedha ni sawa na kudai maziwa zaidi bila kutaka ng'ombe akamuliwe tena.
..................................................................................................................................
Siku njema ya Wafanyakazi Duniani.
"NG'OMBE HANA MAZIWA ZAIDI"
..............
"Jambo letu lipo"