neema shamuhenya
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 312
- 216
MSEMAJI Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas amesema serikali haijakurupuka kutekeleza mradi mkubwa zaidi wa umeme nchini wa Stiegler’s Gorge utakaozalisha umeme mwingi kuliko wote unaozalishwa kwenye miradi yote ya sasa.
Dk Abbas amesema jijini Dar es Salaam kuwa, mradi huo wa kihistoria unatekelezwa kwa kuzingatia faida za kitaalamu ukiwemo usalama wa Gridi ya Taifa, urahisi wa gharama za kuzalisha nishati hiyo, urahisi wa kufanya matengenezo na unafuu wa bei.
Amesema, mradi wa Stiegler’s Gorge utakuwa na bwawa kubwa litakalojaa kwa miaka mitatu, na mashine tisa zitakazozalisha megawati 2,100.
Kwa mujibu wa Dk Abbasi, miradi yote ya umeme nchini kwa sasa inazalisha jumla ya megawati 1,500.
“Tutakuwa na umeme unaotosheleza matumizi ya ndani ya nchi na tutaweza pia kuuza nje ya nchi, kwa hiyo hayo ni manufaa machache,” amesema.
Alisema, utekelezaji wa mradi huo ni utashi wa Serikali ya Awamu ya Tano kuhakikisha nchi inakuwa na umeme wa kutosha.
Alisema, kutekeleza mradi huo haina maana kwamba vyanzo vingine vitaachwa. “Si kweli kwamba tumesahau vyanzo vingine, tunaendelea navyo,”alisema.
Alisema, wataalamu wote wa uzalishaji umeme duniani wanakubaliana kwamba, umeme wa maji ni chanzo rahisi zaidi..
“Kuna vifaa vinaungua, kuna vifaa vinawahi kuharibika, kuna vifaa hata kama hakijaungua lazima kitaalamu kibadilishwe, hiyo haipo kwenye umeme wa maji” alisema.
“Kwa hiyo tunapokwenda kwenye mradi huo hatuendi tu kwamba tumekurupuka, hapana, tumezingatia hayo maoni ya kitaalamu,” amesema.
Dk Abbasi pia alisema, wataalamu wanasema, umeme wa maji ni wa bei rahisi zaidi kwa sababu ya urahisi wa kuuzalisha, hautumii vifaa vingi, na pia hauharibu sana mazingira.