Serikali: Dawa ya Loliondo ni salama

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Serikali: Dawa ya Loliondo ni salama Send to a friend Monday, 28 March 2011 21:50 0diggsdigg

Waandishi Wetu
SERIKALI imesema imeridhishwa na dawa inayotolewa na Mchungaji Ambilikile Masapila wa Kijiji cha Samunge, Loliondo ikisema haina madhara yoyote kwa matumizi ya binadamu.Akitoa tamko la timu ya wanasayansi waliofanya uchunguzi wa awali wa tiba hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Charys Ugullum, alisema timu hiyo ilianza utafiti wake wa awali Machi 7 mwaka huu.

Alisema timu hiyo ilijumuisha watalaamu kutoka Wizara ya Afya, TFDA, Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR), Mkemia Mkuu wa Serikali na Taasisi ya Utafiti wa Dawa za Asili ya Chuo Kikuu cha Afya ya Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).“Kinachofuata sasa tutachunguza kama kweli dawa hiyo inatibu magonjwa hayo matano aliyoyasema Babu. Hivyo wananchi wawe na subira ili watupe nafasi tufanye utafiti wa kina zaidi,” alisema Ugullum.
Alisema pia wameandaa utaratibu wa kuanza kufuatilia maendeleo ya kiafya ya wagonjwa 200 ambao wamekunywa dawa hiyo.Kaimu mkurugenzi huyo alisema watafuatilia matumizi ya mti huo kama unatibu katika sehemu nyingine kwani wana taarifa kuwa baadhi ya makabila kama Wagogo, Wamasai, Wasonjo na Wabarabeigi wamekuwa wakiutumia kwa dawa.
Mkurugenzi wa NIMR, Dk Mwele Malecela alisema mti huo kisayansi unajulikana kama Carissa Spinarum na hapo awali ulijulikana kama Carissa edulis. Alisema ulikuwa unatumika kama mmea tiba sehemu mbalimbali lakini utafiti wa kina ulikuwa bado haujafanywa.“Mti huu umetufungulia mlango wa utafiti na kinachofuata sasa ni kujua ufanisi wa dawa hii,” alisema Dk Malecela.

Kuhusu suala la hatimiliki, Mkurugenzi wa Uendelezaji na Uratibu Utafiti kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia, Dk Rose Kingamkono alisema wanafuatilia ili waweze kujua kama kuna hatimiliki ya tiba hiyo.“Wananchi wasitoe mbegu au mti huo ovyoovyo maana wajanja wanaweza wakauchukua kwenda kutengeneza dawa kisha kuja kutuuzia tena kwa gharama kubwa,” alisema Dk Kingamkono.Msajili wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Dk Paulo Mhame alisema hivi sasa wako katika hatua za mwisho za kumpatia cheti cha usajili Mchungaji Masapila.

Chikawe azuiwa kwenda Loliondo
Uamuzi wa Serikali kuzuia wagonjwa wapya kwenda Samunge kwa siku saba imeanza kutumika jana na kuwabana wananchi wengi wakiwamo vigogo wa Serikali.Uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa habari wa Mwananchi Mjini Loliondo na Kijijini Samunge, umebaini kwamba waathirika wa kwanza wa amri hiyo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utawala Bora, Mathias Chikawe.Chikawe alitarajiwa kutua kwa ndege ndogo katika Uwanja wa Ndege wa Wasso jana asubuhi ili kwenda kupata tiba Samunge lakini alizuiwa, huku kukiwa na taarifa kwamba pia maofisa wengine kadhaa wa Serikali wamezuiwa kutokana na amri hiyo.

Kuahirishwa kwa safari ya Chikawe kuliwafanya maofisa kadhaa wa Serikali wilayani Loliondo kuondoka uwanjani hapo na kurejea katika maeneo yao ya kazi.Magari zaidi ya 300 yakiwa na mamia ya wagonjwa pia yamezuiwa kufika Samunge kutokana na vizuizi vilivyowekwa katika barabara kuu zote za kuingia Loliondo.Vizuizi hivyo vipo katika maeneo ya Meserani na Mto wa Mbu, wilayani Monduli; Babati mkoani Manyara; Mugumu wilayani, Serengeti; na Musoma Mjini.
Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias Wawa Lali, alithibitisha kuzuiwa kwa vigogo wa Serikali, waliokuwa wamepanga kwenda Samunge kwa kutumia usafiri wa anga na kwamba wameshauriwa wapange safari zao pale hali itakapokuwa nzuri.“Ni kweli tumewazuia viongozi wa juu wa Serikali kufika hapa kwani kuna idadi kubwa ya watu ambao bado hawajapata tiba,” alisema Lali.
Mbali ya Waziri Chikawe, helikopta ya Mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), Phillemon Ndesamburo iliyokuwa ikielekea Samunge kupeleka wagonjwa nayo ilizuiwa ikiwa ni kutekeleza maagizo hayo ya Serikali yaliyoridhiwa na Mchungaji Masapila.

Vurugu za wagonjwa
Usiku wa kuamkia jana, mamia ya watu ambao magari yao yalizuiwa nusura wavunje vioo vya magari ya viongozi waliokuwa wakielekea Samunge.Mmoja wa abiria hao, John Lemuya alisema alikuwa ameondoka Dar es Salaam tangu juzi akiwa na wazazi wake na alikuwa hana taarifa zozote za kusitisha kwa kwa safari za kwenda kwa Mchungaji hali ambayo inampa wakati mgumu asijue la kufanya.

“Sasa mimi nipo hapa Meserani, wametuzuia tangu usiku, nina wagonjwa na kuna wenzangu wana wagonjwa hatujui hatma yetu lakini tunaona magari ya viongozi yanakwenda Samunge kupata tiba, hii siyo haki,” alisema Lemuya.Lakini Lali alisema kutokana na hali ilivyo huko Samunge lazima safari zisitishwe akisema huo ni uamuzi wa pamoja baina ya Serikali na mchungaji huyo... “Hata mimi nina ndugu zangu wamekwama kwenye foleni hali ni mbaya nimewaambia kama wanaweza warudi Singida halafu wasubiri hali ikiwa nzuri tutatoa taarifa, lakini kama wana chakula na fedha za kujikimu basi wasubiri kwenye foleni.”
Babu aongeza idadi ya magonjwa anayotibu
Katika hatua nyingine, Mchungaji Masapila ametangaza magonjwa mengine kadhaa ambayo yanaweza kutibiwa kwa dawa anayoitoa. Moja ya magonjwa hayo ni kuongeza au kurejesha nguvu za kiume.
Magonjwa mengine ni kama kutopata mimba kwa kina mama wajawazito... “Nimeulizwa swali hapa je, dawa hii inaweza kutibu magonjwa mengine zaidi ya kisukari, pumu, Kansa na Ukimwi? Nawaambia kunyweni kama magonjwa haya yanatoka kwa Mungu na dawa hii ni ya Mungu kwa nini yasitibike,” alisema.

“Jingine niwaambie kina baba wenye wasiwasi kwamba eti wakinywa dawa hii nguvu zao zitapungua, sasa nasema hivi ukishakunywa hii dawa, wakati unaondoka kwenda nyumbani ndiyo nguvu zitakuwa zikiongezeka na utakuwa mwanaume sawasawa,” alisema.Baada ya kutoa matamshi hayo umati wa watu uliokuwa ukimsikiliza wakati wakisubiri kunywa dawa ulilipuka kwa vicheko huku wengine wakipiga makofi na vigelegele.

Huduma za vyakula
Mchungaji Masapila pia aliwataka wenyeji wa eneo la Sonjo (vijiji vinavyozunguka Kijiji cha Samunge), kuacha kuwapandishia wageni bei za huduma mbalimbali kama za vyakula na vinywaji.

“Nawaomba msifanye ujio wa wagonjwa hawa kukuza uchumi wenu maradufu, uzeni vyakula kwa bei nafuu, kwani mkitaka faida kubwa sana Mungu atatoboa mifuko yenu na msijue fedha zenu zimepotelea wapi,” alisema.
Mchungaji huyo pia aliwataka wamiliki wa magari na madereva kutojitajirisha kwa kuongeza gharama za kubeba wagonjwa akisema fedha hizo zitapotea bila wao kujua.

Hivi sasa gharama za bidhaa na vyakula ni kubwa na kwa magari yaliyopo kwenye foleni, maji makubwa ya Kilimanjaro yanauzwa Sh4,000 na chakula ni kati ya Sh5,000 na 10,000.

Kutokana na ughali huo wa bidhaa, wengi wa wagonjwa wanaosubiri kupata tiba wamelazimika kununua vyombo na kujipikia wenyewe. Hata bei ya bidhaa za vyakula visivyopikwa pia zimepanda. Kilo moja ya mchele na unga vinauzwa Sh3,000 na maji dumu moja la lita 20 ni kati ya Sh6,000 na 10,000.
Habari hii imeandikwa na Nora Damian, Dar Mussa Juma na Neville Meena, Samunge
 
babukijiji.jpg
Magari yakiwa katika foleni kuelekea kwa Mchungaji Ambilikile Mwasapile katika kijiji cha Samunge, Loliondo, Mkoani Arusha jana

Source: Mwananchi.

Hivi inakuwaje waziri anakwenda kwenye kikombe cha babu kwa kutumia safari ya kikazi?? Au waziri anapokwenda mahali hata kama siyo kikazi lazima apokelewe na maafisa wa serikali??
 
Babu aongeza idadi ya magonjwa anayotibu

Katika hatua nyingine, Mchungaji Masapila ametangaza magonjwa mengine kadhaa ambayo yanaweza kutibiwa kwa dawa anayoitoa. Moja ya magonjwa hayo ni kuongeza au kurejesha nguvu za kiume.
Magonjwa mengine ni kama kutopata mimba kwa kina mama wajawazito... “Nimeulizwa swali hapa je, dawa hii inaweza kutibu magonjwa mengine zaidi ya kisukari, pumu, Kansa na Ukimwi? Nawaambia kunyweni kama magonjwa haya yanatoka kwa Mungu na dawa hii ni ya Mungu kwa nini yasitibike,” alisema.

“Jingine niwaambie kina baba wenye wasiwasi kwamba eti wakinywa dawa hii nguvu zao zitapungua, sasa nasema hivi ukishakunywa hii dawa, wakati unaondoka kwenda nyumbani ndiyo nguvu zitakuwa zikiongezeka na utakuwa mwanaume sawasawa,” alisema.Baada ya kutoa matamshi hayo umati wa watu uliokuwa ukimsikiliza wakati wakisubiri kunywa dawa ulilipuka kwa vicheko huku wengine wakipiga makofi na vigelegele.

Source: Mwananchi

My take: Naona sasa mambo yanavyokwenda itakuwa tu kama waganga wa jadi wa mitaani.
 
Back
Top Bottom