Serikali, angalieni hali ya uongozi Vyuo Vikuu

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,006
2,165
Ninauliza kuhusu uongozi ktk Universities zetu. Taarifa niliyopata ni kwamba sasa hivi vyuo vikuu vitatu vya serikali yaani, chuo kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo kikuu Dar (UD) pamoja Mzumbe, vyote vinaongozwa na wastaafu.

Viongozi wa vyuo hivi wamemaliza muda wao wa uongozi au wameshastaafu kwa mjibu wa sheria lakini wameruhusiwa na serikali kuendelea kuongoza taasisi hizi.

Inavyoelekea sasa kila mkuu wa chuo na hata taasisi za serikali anajaribu kung’ang’ania kwenye nafasi. Kwa upande wa Universities naona ni kama aibu kwa sababu wanavyuo ndo wamekuwa mstari wa mbele ktk kuwataka wanasiasa kuheshimu katiba za nchizao. Imekuwaje viongozi wa vyuo hivi hawataki kuheshimu taratibu za kisheria ktk vyuo hivyo?

Alianza huyu wa hapa UD ikasemekana ni mwana-kijiwe wa mkuu wa nchi na sasa wamefuata wegine. Inakuwaje urafiki wa kisiasa unavunja sheria za nchi? ‘Wasomi’ wa vyuo munawezaje kuruhusu hali kama hiyo wakati munafahamu fika kwamba watu kama hao hawataleta jambo lolote la maana ktk ustawi wa vyuo vyenu? Nani kati yao ana malengo mazuri kwa maendeleo yenu?

Ni kweli hakuna anayefaa zaidi ya hao muliopewa kwa mkataba?
 
Ndugu unaweza kuwa na point nzuri lakini je unauhakika hao wameshafikisha umri wa kustaafu? Are you sure Mkandala kafikisha 60!? Nadhani point ni utafutwe utaratibu ambapo wakuu wa vyuo na wakuu wa vyuo wasaidizi hawatateuliwa na raisi. Maana the way it is now its too political!
 
Website ya udsm inaonesha kazaliwa 1953! Atastaafu kwa lazima mwakani! Then your point will be valid, as of now its premature
 
Website ya udsm inaonesha kazaliwa 1953! Atastaafu kwa lazima mwakani! Then your point will be valid, as of now its premature

ndugu yangu hii nchi mimi na wewe ndo tutastaafu. Kuna watu walianza kazi tangu enzi za mwanzo za mwalimu mpaka leo bado ni vijana na hawataki kuachia nafasi. Ukitaka kujua ukweli fuatilia wale aliosoma nao kama bado wako ofisini au walishastaafu.
 
Huwa wanaastaafu watu wa kipato cha chini na mafao hawapewi watafuatilia mpaka mauti yanawafika bila kupewa stahili zao.Lakini kwa akina wale wanaojiita vigogo na magogo ukistaafu hapa unapewa kitengo kingine.Mfano ukistaafu u kanali,katibu mkuu utateuliwa mkuu wa wilaya,mkoa,tume n.k Na wanavyo ongeza mikoa kila kukicha ili wapeane vyeo. Ifikapo 2050 Tanzania tutakuwa na mikoa takribani 50
 
sio hao viongozi wenye shda,pia mie nina tatizo na hawa marais wa vyuo vikuu kula hela nyingi sana,kwanini hawakaguliwi,hi imetokea ktk moja ya vyuo vikuu hapa dodoma cha private,m2 unapata urais ndani ya muda mdogo unatembelea gari,na hi ni baada ya kufanya kufuru ya ukarabati wa ofisi ya uongoz wa chuo hcho,kweli hlo limeniweka pabaya sana,ila ntaliweka vizuri mda ukifika wapendwa.bdo nipo kwa uchunguz wa kina,
 
Ndugu unaweza kuwa na point nzuri lakini je unauhakika hao wameshafikisha umri wa kustaafu? Are you sure Mkandala kafikisha 60!? Nadhani point ni utafutwe utaratibu ambapo wakuu wa vyuo na wakuu wa vyuo wasaidizi hawatateuliwa na raisi. Maana the way it is now its too political!
Nachofahamu na nina uhakika nacho mkandala si mkuu wa chuo bali ni makamu mkuu wa chuo,ila mkuu wa chuo ni balozi kazaura
 
nachofahamu na nina uhakika nacho mkandala si mkuu wa chuo bali ni makamu mkuu wa chuo,ila mkuu wa chuo ni balozi kazaura


hata kama mukandara akiwa makamu mkuu wa chuo

kivyovyote haiwez kufuta uzito wa hoja hii iliyopo mezani kwa sasa
 
katika aina za ajira tanzania kwa kuzingatia hasa za zamani (miaka ya 60-80)(mpya sijui km wamefuta au la)
mkuu wa dola anaweza kumwajili mtu aliyestaafu kwa kuzingatia maslahi ya kitaifa,kiusalama nk na aina ya ajila yake itakua apointment emproyment
 
Ndugu unaweza kuwa na point nzuri lakini je unauhakika hao wameshafikisha umri wa kustaafu? Are you sure Mkandala kafikisha 60!? Nadhani point ni utafutwe utaratibu ambapo wakuu wa vyuo na wakuu wa vyuo wasaidizi hawatateuliwa na raisi. Maana the way it is now its too political!

Website ya udsm inaonesha kazaliwa 1953! Atastaafu kwa lazima mwakani! Then your point will be valid, as of now its premature

Thrd hii ilikuwa na lengo la kuwazungumzia viongozi wakuu watendaji. Vice-Chancellors na wasaidizi wao. Kila chuo kikuu cha serikali kinaendeshwa na Charter. Utaratibu wa kuwapata viongozi wa vyuo hivi vyote, zinafanana kabisa. Hakuna kiongozi anayepatikana kwa uteuzi wa Rais. Wooote wanapatikana kwa kamati (Search committee).

Kwa VCs wote wanatakiwa wakae madarakani kwa vipindi viwili vya miaka mitano kila kimoja. Kwa maana nyingine ukishamaliza muhula wa miaka mitano unaweza kuomba tena au kupitishwa kama umri unakuruhusu miaka mitano mingine. Hapo ndo kuna muzozo na kuna makundi ya watu;
1. kuna viongozi umri hauwaruhusu kuendelea na madaraka kwa kuwa hawana miaka mitano mbele yao
2. kuna watu wamemaliza vipindi viwili vya uongozi na kimya kimya wamepewa tena kinyume cha charter.
3. kuna wengine wamestaafu kwa umri (miaka 60 lakini wamepewa tena kuongoza vyuo.

Tuamini kwamba nchi haina muelekeo kwa sababu haya yote yanatokea hata ktk taasisi zingine za serikali. Nawashangaa sana watu wa vyuo vikuu kwa sababu wao walistahili kuheshimu sheria na taratibu za vyuo vyao lakini sasa yaonekana ni kufahamiana.

Na kibaya sana ni jinsi hizo search committee zinavyopatikana. Zinapendekezwa na baraza la chuo. Mkuu wa baraza wa kila chuo ni mstaafu. Mkuu wa baraza anapatikana kwa kupendekezwa na viongozi wa chuo chenyewe tena na kumpelekea Rais ambaye mara zote hupitisha. Kwa hiyo ni mzunguko, yaani anapitishwa kwa mapemdekezo ya viongozi ambao nao wanapitishwa kwa mapendekezo yake tena! RUBBISH!!

Kama mmoja wetu alivyoeleza vyuo vimejaa ufisadi bila hata kuingiliwa. Eti wakiguswa wanasema wanataka uhuru wa vyuo. uhuru wa kuiba?

Tusiwateteee. Wanauwa elimu na sasa kazi kubwa yao ni kujikomba kwa wanasiasa na tuuuu!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom