Serikali, Airtel zavutana kuhusu hisa za TTCL

Serikali, Airtel zavutana kuhusu hisa za TTCL

The Fixer

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2008
Posts
1,365
Reaction score
599
Wanabodi,
Sisi huku mikoani tunaikosa hii habari kwa mapana yake. Nawaomba mlio na data za kutosha mtuambie nini kinaendelea kwani hii kitu ilitokea miaka ile Mh Rais Mkapa akiwa madarakani na ni moja kati ya sehemu zilizotia doa kubwa sana Mkapa's administration, Kulikuwa na kila dalili za UFISADI !

Tunaomba mwenye issue nzima hii kwa urefu zaidi !
 
Hii kitu anaijua vizuri Mark Mwandosya na Maua Daftari kwani ndo walioigawa ttcl kwa wahindi wa celtel bila senti tano na kisha wahindi hao wakawauzia waarabu wa kuwait nao wakawauzia tana wahindi wa airtel. Wawili hao pamoja na Ben Mkapa wana majibu ya kwa nini walifanya yote hayo ya kuligawa shirika la umma lililokuwa likifanya vyema. Watuambie kama celtel ililipa chochote serikalini. Nchi hii watu tuliowaamini ndo wanaifilisi kwa kuwaalika wenzao kutoka nje na huenda wanaambulia vijisenti tu. Aibu!
 
natamani ningekuwepo kwenye mgao... :wof:

Prof Mark Mwandosya na Maua Daftari ni watu ambao hata sikuwadhania kama wanaweza kuwa na maamuzi ya hovyo namna hii ? TTCL imezungushwa mikononi kwa watu kana kwamba haina mwenyewee . Huwezi kuamini mpaka leo moja ya asset kubwa ya TTCL ile SWITCH yao pale Kijitonyama ndio gateway kubwa sanaa ya Mawasiliano nchini ilianza kutumiwa na Celtel, zain na sasa Airtel - hofu yangu ni kama wanalipia wala hata pango ama ada tu ya kutumia mtambo huo mkubwa nchini !
 
hiyo SWITCH imerudi mikononi kwao au wamempa mwengine? :A S-eek:
 
Yaaaaah ! Switch kubwa ( inayotegemewa ) kuliko zoote Tanzania
 
Hii nchi ingeshapita kwenye zama za viwanda miaka 200 nyuma na leo tungekuwa tuna tungekuwa tunarusha satellite, ICBM, kutoa misaada ya kibinadamu Amerika na Ulaya lakini wahuni na majizi wachache wanatufanya tubaki kuwa omba omba hadi leo.
Wamelifanya taifa liwe la kimatonya kabisa na wanaendelea kudunda tu na kutuita mabwege
 
Back
Top Bottom