Serikali 2 au 1 HAPANA 3

Serikali 2 au 1 HAPANA 3

Mbogela

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2008
Posts
1,384
Reaction score
261
Baaada ya marekebisho ya katiba ya Zanzibar watu wengi wa upande wa Zanzibar na Tanzania bara wamekuwa na hoja ya kutaka kuwepo serikali tatu ili kuweza kuweka usawa kati ya Tanzania Bara na Tanzania visiwani. Muundo huo utamaanisha kuwa na serikali ya Zanzibar, serikali ya Tanzania bara (sijui kama jina litarudi la Tanganyika) na serikali ya muungano.

Mimi binafsi sioni sababu ya kuwa na muundo wa serikali tatu. Tunataka serikali tatu ili iweje? Sioni madhumuni ya serikali ya Muungano, kama kutakuwa na serikali ya Tanganyika na kutakuwa na serikali ya Zanzibar ambazo zitashughurikia masuala ya utawala na ustawi wa jamii kwa pande zote mbili ipasavyo serikali ya muungano itafanya kazi gani?

Kuwepo kwa muundo wa serikali tatu ni kuwaongezea wananchi mzigo kwenye uendeshaji wa serikali hizo. Na bahati mbaya sana naona kama hili suala la serikali tatu linapenya pia katika sera za CHADEMA ingawa sijawasikia CCM (walio kwenye serikali ya JMT ) wakisema kitu. Wananchi tutalazimika kuwalipa na kuwatunza Rais wa muungano na baraza lake, pia Rais wa Tanganyika na baraza lake alafu Rais wa Zanzibar na baraza lake. Bado mabunge ambayo mpaka sasa hakuna anayesema muundo wake pampja na vyombo vingine vya dola kama mahakama utakuwaje?

Nadhani wazanzibar wana nia ya kuwa na serikali na nchi yenye mamlaka kamili kwa hiyo basi mimi ningedhani jambo la msingi sisi kama Watanzania ni kujadili je tuelekee serikali moja au tubaki na muundo tulio nao sasa? Option ya kuongeza muundo mwingine ni kutuumiza walipa kodi. La sivyo basi tukubaliane kwa hiari yetu wenyewe kabisa kutokuwa na muungano tubaki kuwa nchi mbili zitakazoshirikiana kwa karibu huku tukisubiri mambo ya east Africa federal government. Sioni sababu ya kuwa na serikali tatu labda mtu anieleweshe hapa.
 
Ziwe mbili na kila nchi iwe kama kabla ya muungano, yaani kuvunja muungano na kuangalia upya kama tunahitaji kitu kama hiki kwa kuwashirikisha wananchi wa nchi hizi mbili!
 
Ziwe mbili na kila nchi iwe kama kabla ya muungano, yaani kuvunja muungano na kuangalia upya kama tunahitaji kitu kama hiki kwa kuwashirikisha wananchi wa nchi hizi mbili!

hata mimi nakubaliana na wazo lako, kwani Muungano huu watu kama wame bakwa vile! Na sasa wanalazimishwa waishi katika ndoa ambayo hawakutoa ridhaa yao
 
Back
Top Bottom