Serengeti vs Maasai Mara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serengeti vs Maasai Mara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkereketwa_Huyu, Jul 25, 2012.

 1. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #1
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Baada ya kuangalia "The Great Migation" ya wanyama wanaotoka Serengeti kwenda Maasai Mara Kenya kukimbia ukame Tanzania, kwa kweli nimeshikwa na hasira. Kwa nini? Maasai Mara ni sehemu ndogo sana tena sana kulinganisha na Serengeti, ila TV za dunia zimehamia huko na kuitangaza Kenya as if Serengeti iko huko. Yaani wanavyotangaza ni kama vile Serengeti is nothing compared to Maasai Mara. Pia kinacho udhi ni kwamba Kenya wanapata pesa za utalii wa hii Great Migration mara 20 zaidi ya Tanzania (source - CCTV China). TANAPA kazi yao ni nini? Kila kukicha viongozi wanasafiri nje ya nchi kuitangaza Tanzania, sasa kwanini tunazidiwa kete na majirani? Hakuna nchi duniani yenye mbuga kama zetu, kwanini tunakuwa mazezeta? Je, Maasai Mara ni bora shinda The mighty Serengeti? Hii nchi bwana, basi tu.
   
 2. k

  kev Senior Member

  #2
  Jul 25, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania hakuna barabara nzuri ndani ya serengeti kama masai mara.hotel za serengeti hazilingani kwa ubora na za masai mara ila za serengeti bei ni mara dufu za mara.njia za kuzunguka kutafuta wanyama ni chache na hazipitiki kwa muda wote.yaani ni vi2 vidogo ndo vinafanya wa2 waikimbie serengeti
   
 3. Rodcones

  Rodcones JF-Expert Member

  #3
  Jul 25, 2012
  Joined: Oct 16, 2007
  Messages: 403
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwasababu tanzania hakuna kitu kilicho siliasi katika sirikali ni siasa tu hata kutunza mbuga na kuzitangaza tunashindwa tunaishia kuuza wanyama na ukisema utakiona????????
   
 4. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #4
  Jul 25, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  :israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel::israel:
   
 5. P

  PolisiB52 Member

  #5
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serengeti ndo mambo yote duniani kwani wakenya wanachokifanya ni kujitangaza kwa sana, pia rate za hotel zao ziko chini kwani migration wanakuwepo Masai Mara kwa 2months kwaiyo muda mwingi wapo kwa upande wa Tanzania, cha kufanya hapa kwanza bei ya hotel ziwe chini pili barabara zirekebishwe hakuna haja ya kuongeza kwani zilizopo zinatosha, tatizo letu ni kwamba haya mashirika ya umma yanaendeshwa kisiasa.
   
 6. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #6
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280

  Sitashangaa Kikwete anasoma hizi habari huku akitukana na kutukashifu.
   
 7. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #7
  Jul 25, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Wakulu walishapewa 10% yanini tena kuanza kuhangaikia the great migration?
   
 8. Dhuks

  Dhuks JF-Expert Member

  #8
  Jul 25, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 1,470
  Likes Received: 350
  Trophy Points: 180
  Do anything you want to market Serengeti which is a wonderful place but lets not resort to this
  from
  Standard Digital News : Business : Animal journey across Mara starts

  I hope it is just irresponsible journalism
   
 9. M

  MLERAI JF-Expert Member

  #9
  Jul 25, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 673
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Wenzetu wakenya wanajitangaza sana sisi huku tumebaki na useme hifadhi ni mambo ya asili.Watalii wenyewe wanakiri hifadhi zetu ni bora kuliko za kenya na wangelijua mapema wasinge pitia kenya ila hakuna wa kuwaapa taarifa.Sekta ya utalii inaliingizia taifa pato kubwa sana ususani hifadhi ya serengeti na ngorongoro ila zimebaki kama nyumba ya yatima hakuna anayezijali barabara ni mbaya kupita kiasi.ukitoka serengeti kwenda ngorongoro utajuta kwanini umekuwa dereva.Kama kurekebisha tuu barabara wameshindwa je wataweza kuzitangaza?
   
 10. D

  Dango4Dango Member

  #10
  Jul 26, 2012
  Joined: Sep 13, 2008
  Messages: 8
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Inasikitisha sana kwa kiasi gani huduma zetu za utalii ni za enzi ya nyerere , wahudumu hawana ujuzi wa kuhudumia watalii ,kiingereza cha form two, miundo mbinu choka mbaya , magari mengi chokah mbaya. Ina nikumbusha kilimo chetu cha jembe na kungojea mvua kwa miaka 50 ya uhuru .
  Roho inauma sana nashindwa kupanga maelezo. Thanks mkereketwa for posting this topic. Ntarudi.
   
 11. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #11
  Jul 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160


  Bilila 5star hotel! Ya Ndg yetu jk! Kenya wanapromot Masai Mara!

  Jk+wenzake,acheni uchu wa madaraka jamani!
  Haitawasaidia chochote bali ni matatizo tosha kwenu!

  Matendo yenu yatafuatana nanyi!
  Ndio tutajua kama MUNGU tunayemlilia amelala!
   
 12. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #12
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu mambo mengine nakubaliana nawe isipokuwa kuhusu barabara, hata Masai Mara barabara zake ni za udongo kama zilivyo za Mbuga ya Serengeti - juzi juzi niliona kwenye TV madereva wa minibus zinazo safirisha watalii wanalalamikia barabara hiyo kwamba inaharibu magari yao wakaiomba Serikali ya Kenya iboreshe.
   
 13. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Mkuu mambo mengine nakubaliana nawe isipokuwa kuhusu barabara, hata Masai Mara barabara zake ni za udongo kama zilivyo za Mbuga ya Serengeti - juzi juzi niliona kwenye TV madereva wa minibus zinazo safirisha watalii wanalalamikia barabara hiyo kwamba inaharibu magari yao wakaiomba Serikali ya Kenya iboreshe.
   
 14. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Kila mtu anajua Serengeti ndio mambo yote DUNIANI, swali ni je Tanzania inapata faida gani kutokana na mbuga hiyo zaidi ya ufisadi wa kuhuza wanyama kwa Warabu kinyemela na hatujali mambo ya kitalii-wizi,wizi,wizi!! Juzi juzi hapa niliona afisa mmoja wa Kenya akilalamika kwamba wenyewe wanahangahika kuhifadhi na kuwalinda wanyama kama black rhinos na wengine, lakini sisi Watanzania tunawapa wawindaji blocks za kuwinda na hakuna anayefatilia wanawinda nini au wanafanya nini huko! Kwa hiyo tuna-undermine juhudi za Wakenya za kulinda rare Animals! Afisa wa Kenya alicho sema ni kweli TUPU.

  Chukulia mfano wa rhino walio tolewa na Serikali ya Africa Kusini kwa heshima ya Rais Kikwete-kwani wanyama hao walichukua round walipo pelekwa Mbuga ya Serengeti? walichinjiliwa mbali na pembe zao kung'olewa. Badala ya kuhamasisha watu kutumia CAMERA ku-shoot animals sisi tunatumia a telescopic sighted rifles kuwa-shoot.

  Wenzetu Wakenya wana mbinu nyingi kuhusu biashara za kitalii na Serikali yao suala hili inalichukulia seriously, na hawana utani katika ufanyaji kazi wao na wanafanya homework ya kutosha kabla hawaja tagaza kitu kwa kuangalia ni kitu gani watalii wanapendelea kuona na kusikia hata wakisema Serengeti ni GAME RESERVE kama Masai Mara, Watanzania wanakaa kimya TU!

  Shirika la letu la umma la utalii TANZANIA awafanyi effort yoyote kujitangaza zaidi ya kujishughulisha na utoaji vibali vya kuwinda na kuhuza wanyama kwa wageni, wenzetu wame-exploit udhaifu wetu katika nyanja hiyo to maximum. Mimi nashauri waende Kenya wakajifunze namna ya kufanya biashara za kitalii.
   
Loading...