Serengeti kuuzwa kwa Waarabu!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serengeti kuuzwa kwa Waarabu!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ehud, Aug 16, 2012.

 1. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #1
  Aug 16, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mtandao mmoja unaojihusisha na harakati za haki za wanyama na binadamu umehabarisha kuwa Serikali ya Tanzania chini ya CCM imepanga kuuza sehemu kubwa ya mbuga maarufu duniani kwa Wafalme wa nchi za Kiarabu ili wawinde chui na Simba!!!

  Mtandao huo ambao kwa sasa upo kwenye kampeni kali kumtaka rais wa Tanzania aachane na deal hilo la hatari kwa nchi umeendelea kusema kuwa katika mkataba huo wa mauziano Wamasai wapatao 48,000 wanaoishi ndani ya hifadhi ya seringeti watahamishwa kimabavu ili wasiwasumbue wafalme hao toka arabuni!!!

  Kwa habari zaidi soma hapa: Avaaz - Stop the Serengeti Sell-off

  Wakati hayo yakiendelea Waziri wa Maliasili na Utalii amekanusha kuwa habari ya uuzwaji wa Mbuga ya Serengeti; soma hapa: Akanusha Wamasai kuhamishwa Serengeti


  Wanatukumbusha yale ya Loliondo na Marhem Stan Katabaro!
   
Loading...