Serengeti Fiesta vs Kili Music Tour

Serengeti Fiesta vs Kili Music Tour

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,402
Reaction score
1,618
Hayo ndio matamasha makubwa mawili nchini Tanzania ambayo yanafanyika kila mwaka.

Kwa mtazamo wako binafsi, unadhani kati ya Serengeti Fiesta na Kili Music Tour wapi ni bora zaidi (katika kila kitu) na wanaojaza watu wengi zaidi.

Dr. MCHUNGUZI HURU (PhD)
 
Last edited by a moderator:
Kili Music wapo vema, Wana ma Dj wakali, wasanii wao Wanakubalika, Jukwaa la maana, Kinywaji bure, Kiingilio bei rahc, wanajitahidi sana kuinua maswala ya burudani nchini.
 
Kili balaa, maana fiesta kuna wasanii wengine nadhani nyimbo zao hupigwa mawingu tu.
 
Zote sawa tofauti zao mwingine anajaza watu kwa vinywaj vya bure na kiingilio kidogo na mwingine anajaza watu kwa matangazo mazuri na kiingilio kikubwa
 
Mm nashauri haya matamasha yangekua yanapishana kuanzia miez mitatu au minne
 
Mm nashauri haya matamasha yangekua yanapishana kuanzia miez mitatu au minne

Ni kweli kwa sababu kubwa mbili.
1. Kili Music Tour inahusisha wasanii wote waliopata tuzo ktk KTMA, na huku unakuta msanii huyo anatakiwa pia kufanya show Serengeti Fiesta. Je ataacha wapi aende wapi? Kuna mgongano wa ratiba hapa mwishowe msanii anachoka anaweza kupata "fatique" kutokana na kutopata muda wa kupumzika.

2. Uzito wa matamasha yenyewe. Kutokana na umuhim wa matamasha haya ni muhimu kukawa na interval ya timing ili kila moja liweze kupewe uzito stahiki na watu waweze kuhudhuria kwa kujiachia zaidi. Sio mtu anaenda la Kili tour ila moyoni anajilaumu kukosa la Fiesta.

Nawasilisha.
 
Fiesta bado ni funiko. Kiingilio kikubwa lakini wanajaza. Jukwaa lao babkubwa huwezi linganisha na la kili. Angalia Mwanza na Tanga alafu unambie ni wapi kili wameshawahi kutengeneza jukwaa kama lile.

Alafu Fiesta wanajitahidi kwenye kujitangaza na kupatangaza kule wanakoenda kufanya show. Vilevile wanajitahidi kutangaza hata fursa zilizoko mikoani bila kusahau vivutio vya kitalii. Yote tisa, kumi wanaibua vipaji.

Fiesta inahamasisha watu, viongozi wa watu na kila mwaka wanakuja na kaulimbiu ya kuhamasisha watu wabadilike.

Kifupi KILI wamebaki ku-copy na ku-paste yale wanayoyafanya Fiesta kwa maana hawana ubunifu wowote zaidi ya kuiga.

Nenda kwenye Matamasha ya Fiesta utakuta Wabunge,wanasiasa hata baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya wanaudhulia.

Kifupi Fiesta ni zaidi ya tamasha.
 
Ukwel fiesta in zaid ya tamasha mkubwa mpshe hao kili wanaigatuu
 
TBL mambo ipo kule afu ndo walianza sasa hao wengine wangesubiri tumalize ndo waje
 
ImageUploadedByJamiiForums1409895401.613068.jpg
Haya sasa mwenye macho haambiwi tazama
 
Kiboko acha kupotosha watu kana kwamba hatuudhulii hayo matamasha. Usituletee picha za hotelini hapa. Tatizo mna chuki binafsi.

Leta majukwaa tulinganishe lipi jukwaa kali. Bahati nzuri sisi hatubagui matamasha yote tunaenda. Bado tamasha la fiesta ni mfuniko kuanzia stage mpaka kiingilio. Kili kiingilio ni bure. Unalipa buku 3 na bia ya bure, bado huoni kama kuna tofauti hapo?
 
Kwenye upande wa wasanii bado wako 50/50 kwani wasanii wengi wao ni walewale kwenye watamasha yote tofauti ni kidogo sana hasa kwa wale wenye mabifu yao.

Tofauti yao imebaki kwenye ubunifu na promo. Hapo Fiesta wame-advance mbele kidogo kuliko kili.

Kili wamebaki copy and paste tu.
 
TBL mambo ipo kule afu ndo walianza sasa hao wengine wangesubiri tumalize ndo waje

Sizani kama wewe unakijua ulichoandika au ni mihemko ya kishabiki tu ndo inakusumbua. Kili imeanza lini kupiga matamasha tofauti na mwaka jana?
 
Back
Top Bottom