Serengeti Breweries kudhibiti wanywaji wenye umri mdogo

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zenye kundi la watu wenye umri mdogo wanaotumia pombe kwa kiwango kikubwa, wakiwamo wanafunzi.

Hivyo, Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imezindua programu ya kupambana na unywaji pombe kwa watu wenye umri mdogo, ikilenga kudhibiti tabia hiyo.

Utafiti uliofanywa mwaka 2019 katika mikoa ya Mwanza na Kilimanjaro, ulibaini kuwepo kwa mwenendo wa matumizi ya pombe miongoni mwa wanafunzi wa shule za sekondari wenye umri wa miaka 15, ambapo mkoani Kilimanjaro ilikuwa kwa asilimia 63.9 wavulana na Mwanza asilimia 12.9 kwa wasichana.

Mwenendo wa matumizi ya pombe miongoni mwa wanafunzi wenye umri wa miaka 13-15 jijini Dar es Salaam yalikuwa asilimia 5.6.

Meneja Mawasiliano wa SBL, Rispa Hatibu alisema; “mpango huu unahusisha utoaji wa mafunzo muhimu juu ya athari mbaya za unywaji pombe katika umri mdogo kwa vijana na jamii na utatekelezwa nchi nzima, ukiwafikia wanafunzi 15,000.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kheri James aliipongeza SBL kwa kuja na mpango mzuri wa kukabiliana na tatizo hilo kwa vijana wenye umri mdogo.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom