SERBIA: Rais amteuwa Waziri Mkuu msagaji

SERBIA: Rais amteuwa Waziri Mkuu msagaji

View attachment 524873
Rais wa Serbia amemteua mwanamke ambaye ni mpenzi wa jinsia moja kuwa waziri mkuu katika jimbo la kihafidhana la Balkan.

Ana Brnabic alichaguliwa na rais mpya , Aleksandar Vucic. Kuidhinishwa kwake na bunge kutakuwa rasmi kwa kuwa chama chake na washirika wake wana wajumbe wengi.

Miaka michache iliopita uteuzi wa mtu wa mapenzi ya jinsia moja usingedhaniwa.
Lakini Serbia inayosubiri kujiunga na bara Ulaya imeonyesha ithibati kwamba kuna ongezeko la uvumilivu miongoni mwa raia wa eneo hilo.

Hatahivyo kiongozi wa chama kidogo katika muungano wa rais huyo Dragan Markovic Palma wa muungano wa Serbia alisema kuwa bi Brnabic ''sio chagua lake la waziri wake mkuu''.

Bi Brnabic atajiunga na idadi ndogo ya mawaziri wakuu ambao ni wapenzi wa jinsia moja ili kuongoza serikali barani Ulaya ikiwemo Leo Varadkar wa Jamhuri ya Ireland na Xavier Bettel wa Luxenbourg.

Wadhfa wa waziri mkuu katika utawala huo utakuwa na uwezo hafifu.

Chanzo: BBC
Hapo namuunga mkono Raisi kwa kazi nzuri bila kuangalia sex life issue muhimu wajibu wa kazi anaujua
 
Mungu mvumilivu sana
Sidhani kama sodoma walifikia huku
Sisi tumezidi
 
Asiye na dhambi, na awe wa kwanza kutoa hukumu kwa huyu mama.
 
Hapo ndipo ninapoipa nguvu BIBLIA
pamoja na mkanganyiko mwingi ndani yake
daah siku za mwisho!


Biblia ikishasema kitu huwa inakuwa hivyo. Tazama jinsi ilivyozungumza kuhusu Ishmael na uzao wake, ona kinachoendelea sasa. Na haina mkanganyiko wowote wowote ila sisi wanadamu, ndio huwa tunajikanganya kwa ama kuokuielewa au kupotosha kwa makusudi
 
Yan mimi naona hawa jamaa wapo sawa kabisa!sababu sioni umaana wa kuwa na mtu ambaye sio msagaji na ni msomi halafu anakuwa mwizi kama akina chege na akina bashite.
bora msagaji tuuuuuuu🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁🙁
 
Wawatafute na watwangaji na wapondaji sasa wafungue kiwanda maana wamezidi sifa za kijinga
 
Back
Top Bottom