Sera za nchi na usigini wa katiba

Waridi

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,025
172
Ndugu wananchi,
Sheria mama inayoliongoza taifa lolote ni katiba ya taifa husika. Kwetu sisi watanzania tunayo katika ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.Katiba yetu hii ndio mzani wa kupima usahihi wa sheria, taratibu na sera zitumikazo nchini.Inasikitisha sana kuona kwamba katiba yetu imesiginwa sana na serikali ya CCM kupitia sera zake za kiuchumi hususan ubinafsishaji pasi Hekima.

katiba inasema wazi katika Ibara ya 9, ibara ndogo(J) kwamba;
serikali ina jukumu la kuhakikisha kwamba shughuli za kiuchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha ulimbikizwaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi'
Oooh poor Tanzania, kinyume cha hili ndicho kinachofanyika! Kumbe Tanzania inaongozwa na katiba ipi??
 
Back
Top Bottom