Wabeloya, Nigeria kuna serikali za Majimbo, WHERE ARE THEY NOW?
Na watanzania hawasomi tu.Katiba mpya ya Kenya imeweka sera za majimbo na wataanza kutekeleza kama sikosei mwaka wa uchaguzi.Kutakuwa na ma-senators na governors.Sema nachouliza: mosi, ni Je sera ya majimbo Nigeria mbona haijafanikiwa?Pili,Ni wapi Nigeria wamekosea ili na nini tusirudie makosa yao?.Pia mimi nataka kutofautiana na wewe kuhusu miji mikubwa Arusha,mwanza,mbeya na dar itabaki kuvutia watu kutokana na mzunguko wa pesa uliopo,Kwa hilo sidhani kama sera majimbo itakuwa muarobaini wa watu kukimbilia DAR.Sema yatasaidia kutoa ukiritiba wa dsm kutawala na kumiliki raslimali yote ya Jamuhuri.Na kama watakata sera ya majimbo basi wakuu wa mikoa na wilaya inabidi wawe wanachaguliwa na wananchi wa sehemu husika na tuwape majukumu mengine katika mustakbari wa maendeleo ya mikoa yetu katika katiba mpya.na maamuzi yanabidi yasiwe yanatolewa na dsm.Mwisho viongozi amieni dodoma jamani.
Mipaka yenyewe tunayolinda na kuipigania kuwa ni ya Taifa, iliwekwa na Mkoloni kwa misingi ya kutenganisha waafrika, so sioni shida yoyote kwa sisi kujaribu hili la majimbo.Tuhakikishe tu mfumo hautaihatarisha "National identity", at least kwasasa, kwasababu kupigania mipaka ya mkoloni ni utumwa in many ways.
Asante sana, naona umejipanga kweli kweli kuipitisha hii hoja. Sasa jielekeze kwenye kutuwekea hapa sketch ya Majimbo sababu mpaka sasa Jimbo linalojulikana ni ka Kaskazini peke yeke.Mkuu Sangara asante kwa angalizo lako, kuna taratibu za kufuata kuanzisha haya majimbo, na moja ya makosa ya Nigeria na Indonesia ni kuwa na matatizo ya nyuma ambayo hayajafanyiwa kazi, lingine ni kuwa na hidden ajenda katika kugawa majimbo...hivi vitaleta tatizo
Nimetafuta paper moja ya kukusaidia kusoma from A to Z kuhusu Nigeria na Indonesia na tunaweza kujifunza wapi wamekosea
Read
http://www.crise.ox.ac.uk/pubs/workingpaper49.pdf
soma pia katika moja ya report zao zinazoeleza takwimu na sababu mbalimbali za ku-adopt hii style
ftp://ftp.fao.org/sd/SDA/SDAR/Nigeria.pdf
maswali mengi yamejibiwa humo
Wabeloya, katika serikali za Majimbo, Zanzibar itakuwa Jimbo au itaendelea na status yake ya sasa kisha kuwe na Jimbo la Unguja na lingine la Pemba? Swali hili ni la msingi kama tutaendelea na muundo wa sasa wa muungano au kama tutaopt muundo wa serikali tatu.
Swali la Pili, nimeona kunasehemu unatoa maelezo yanayomaanisha kwamba serikali za majimbo ni vehicle ya utajiri, unamaanisha watu wote watakuwa matajiri au majimbo yatakuwa matajiri?
tusaidie kutuwekea sketch ya majimbo, sababu haiwezekani tukawa tunazungumzia hewani tu, mgawanyo wa majimbo utategemea na nini? kuna sehemu umesema muundo huu utawezesha kulinda tamaduni zetu, kwa maana gani? au majimbo yataundwa kwa misingi ya ukabila?
Mwisho, kwa sasa, hili la kupunguza watu Dar es Salaam sijalielewa kabisa kabisa, naomba maelezo ya ziada.
Mkuu Waberoya ulichoandika ni sahihi sana. Hii system ya sasa imesha fail.
nyie cdm kama mnataka kufutika kwenye ramani ya siasa endelezeni siasa zenu za majimbo , msisahau kwamba Nasari aliteleza kule arumeru then muda muafaka ukifika lazima wataalamu wataunganisha na swala la majimbo
Wabeloya, Nigeria kuna serikali za Majimbo, WHERE ARE THEY NOW?
nakubaliana na wewe japo kuna majimbo watu wake watakiona cha moto kutokana na hulka yao ya kutokupenda kujishughulisha.
Sikubaliani na wewe kwamba tatizo la wanigeria ni udini, sababu hakuna dini inayohubiri wananchi kuishi maisha ya kimasikini. Usipokuwa makini utabadilisha hoja ya msingi sasa hivi. Nigeria si nchi ya kidini na kama unazungumzia matatizo ya Waislamu wa Nigeria, nakutegemea uwe na mtizamo kwamba serikali za majimbo zimechangia kurutubisha hali hiyo na sio kwamba ufanisi wa serikali za majimbo unazoroteshwa na misimamo ya imani za kidini.wameendekeza sana udini. Ndo maana watu wa majimbo ya kaskazini wanataka kuwe na sheria za kiislamu. Huwezi kuendesha nchi moja yenye dini tofauti kwa sheria za dini moja. Hii ndo iliyoishinda sudan. Kuna mambo ambayo yatakuwa yanaendeshwa na central government kama vyuo vikuu,referal hospitals,majeshi,viwanja vya ndege.
Hatuhitaji majimbo ili kuweza kuyapata hayo aliyoyaorodhesha waberoya, infact kwa system hii tuliyokuwa nayo tunaweza kuyapata hayo iwapo (1) sheria tunazozitunga zinafuatwa vizuri (2) viongozi wetu wanafanya kazi vizuri na kwa moyo wa kizalendo (3) wananchi kuwa alert na pia kuhakikisha wanawawajibisha viongozi wao (4) mipango na sera zinazotungwa ziwe nzuri na kusimamiwa vyema tanzania si nchi kubwa ya kushindwa kuwa governed iwapo tuko serious, kiufupi ni kwamba kama tumeshindwa kuigovern tanzania ambayo inazidiwa ukubwa na jimbo moja la xinjiang la china, basi usitegemee kwamba hata hayo majimbo yanaweza kuwa governed vizuri( wenye ueledi wa kanuni ya mathematical induction wanaweza kunipata nazungumzia nini). Nchi zinazopaswa kugawanywa katika majimbo ni zile (1) zenye eneo kubwa sana na population kubwa. Kwa standard ya eneo la tanzania na population yake ya watu milioni 45, mfumo wa sasa wa mikoa chini ya serikali kuu unatufaa sana, kinachotakiwa ni kuziongezea serikali za mikoa na wilaya nguvu fulani fualani katika kufanya maamuzi katika mikoa hiyo, lakini sera kuu ipangwe na serikali kuu ikishirikiana na mikoa husika. Hasara za serikali ya majimbo kwa nchi kama ya tanzania ni (1) udini majimbo yenye watu wa dini fulani wengi, yanaweza yakatrump religious minority katika majimbo husika. Hii inaweza ikasababisha backlash kwenye majimbo mengineyo na matokeo yake ukajenga nchi yenye tension ya udini vibaya sana. Kwa mfumo tuliokuwa nao sasa hii inaondoshwa na serikali kuu. Kama muasisi wa chadema mwenyewe mzee mtei ambaye ni msomi anaonekana yuko religious sensitive, unategemea nini kwa wale ambao wanatamani wawe na dola ya kidini uwape jimbo ambalo wao ndiyo majority?
The only difference is the depth of decentralization. kwa mfano sisi tunaweza kuamua kwamba kutakuwa kuna vyama vya siasa ambavyo vinaoperate kwenye level ya Jimbo tu kama havina au vimeshindwa kujitanua na kutapakaa nchi nzima kama CCM na CHADEMA.Weberoga,
Please educate me the difference btw local goverment of Tanznaia and Sera ya Majimbo mnayozungumzia? I think tuna jadili lugha but mifumo iko similar... and i'm not say equal.. hivyo sio kweli kamba Tanzania haina sera ya Majimbo...