Sera za Majimbo ni za Lazima! Asiyetaka ahame Nchi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sera za Majimbo ni za Lazima! Asiyetaka ahame Nchi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Waberoya, May 18, 2012.

 1. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #1
  May 18, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  Unajua kuna kipimo cha ujinga na upumbavu lakini heri mjinga maana anaweza kueleweshwa na mpumbavu katu anajua ukweli ila anaupindisha kwa faida zake

  Ridhwan Kikwete na wana CCM wenzie ni moja ya makundi dhaifu kiakili na kihuhalisia, huku kundi linguine la wenye ulemavu wa akili ni baadhi ya wanachadema ambao ni fuata mkumbo, wasiozijua seraza chama chao na hawawezi kuzitetea..poleni!


  Faida za sera za majimbo


  1. Faida za utawala

  Sera za majimbo zinaweza kabisa kufananishwa na Decentralisation system, ambako maamuzi hufanywa na watu wa chini kabisa, kwa jambo husika na kwa wakati husika.

  Wananchi wanapewa uwezo wa kujitafuatia uongozi wao, na hivyo kumjweka mtu ambaye anajua mazingira ya eneo hilo, shinda walizonanzo na way forward kuzitatua. Mtu huyu pengine anajua utamaduni wa eneo husika, tabia zao na kupanga mikakati ya kujikwamua kutokana na walivyo.

  Kwa kifupi ita improve quality of decision kwa jambo loloye liwe kwa eneo husika kitu ambacho hakipo kwa sasa

  2. Faida za uchumi

  Mtu yeyote mjinga na asiyeelewa ni yule anayedhani au kufikiri kuwa kuna maeneo nchi hii ni maskini na mengine ni tajiri.

  Kansa ya mawazo haya iko kwa viongozi wa CCM na serikali yao wakihubiri kuwa majimbo ni mifarakano na wengine watakuwa maskini
  Sema jimbo gani ni maskini, nitakueleza wafanye nini kupata utajiri..

  Hakuna kijiji, mkoa au wilaya maskini Tanzania haipo!!! Umaskini ukiwapo ni wa ubongo mdogo wa raia wa mahali hapo

  Sera ya majimbo itaharakisha maendeleo kwani ita ‘motivate' au ku'stimulate brain za watu wa eneo husika kuwaza na kufikiri kipi kifanyike kuleta maendeleo

  Wataalamu wa sosholojia wanatanabaisha kuwa, jamii inayotengeneza sere zake, au kuamua mambo yake hufanya kazi kwa bidii ili maamuzi na malengo waliyoyaamua yafikiwe….kwa mfano sera ya kilimo kwanza haitaweza kufanikiwa kwa sababu haijaamuliwa na wananchi na haijaingia akilini au mioyoni mwao ..kwa nini ‘kilimo kwanza' hata kama sera hii ni nzuri!!

  Ni matatizo waliyoyapata akina Nyerere enzi hizo..wakati mpaka leo hii israel ina vijiji ya ujamaa kama alivyoanzisha Nyerere sisi vyetu havipo na kama vipo ni kibahati tu!!

  Leo wengi hawajui wilaya ya Mbinga ndiyo tajiri kuliko zote Tanzania kwa kilimo cha kahawa, ufugaji na sasa wanapanda miti!!Nani anajua kuwa mkoa wa mtwara ni wa saba kuliingizia pato taifa?

  Au hamjui kuwa wilaya za Ngaka, kiwira zina makaa ya mawe na liganga kuna chuma, nani asiyejua utajiri wa madini na kilimo morogogoro na mazao ya madawa mkoa wa Pwani?

  Au nani asiyetamani kuona utajiri za zabibu Dodoma unavuka mipaka na kushindana na Israel ambayo inategemea zabibu kwa sana
  Tanzania haina sehemu maskini, J

  Juzi Mkongeumeongelewa sana, Mafuta na ziwa ni utajiri wa Kigoma na Rukwa inasifika kwa kilimo…semeni tujue wilaya maskini ni ipi?

  Au haiumi kuona Lindi na Mtwara wana gesi ambayo inasafirishwa kuletwa DSM huku wao wakihangaika kucheza ngoma kwa kukosa kazi??

  Haiumi kusikia Tanzania ni wazalishaji wakubwa wa dhahabu duniani uku wilaya husika ni maskini wakutupwa, au Almasi ya shinyanga ikiliwa kimya kimya!!! Kweli asali ya tabora na kijani cha Bukoba sio mtaji wa maendeleo ya taifa hili? Nani anabisha??

  Sera hii italeta ushindani wa majimbo katika kuongeza kipato cha kaya, kijiji, kata, jimno na taifa!!

  Dubai wameweza kuuweka mji wao kuwa sehemu ya kibiashara duniani sehemu ambayo ni jangwa kabisa!!

  Kama kuna sehemu kuna jangwa, basi tutaweka DAR LIVE nyingi sana (Ridhwan tenda hiyoo dogo), na starehe nyingine zote ili watu wakipiga kazi ngumu wanaenda kupumzika na kujiburidisha sehemu ambazo zitakuwa haziwezekaniki..japo hamna hizo sehemu

  3. Faida za kulinda utamaduni

  Hakuna utumwa mbaya na wa kipekee kama kuacha tamaduni zetu, tumeiga wazungu mpaka wanatushangaa, vijana wetu wamekuwa kama mabinti, eti wanabana pua na MASCULINE behavior haipo!!

  Malezi duni!!!
  Kijana gani leo yuko tayari kupigana na kusema msitu huu wa baba yangu, na yuko tayari kuua simba na kulinda hadhi za kikoo, kifamilia, kikabila na hatimaye taifa??

  Sera majimbo japo zimejikita ki-uchumi zaidi, lakini zina faida kubwa sana hata kiutamaduni

  Utamaduni wa eneo husika huleta ubunifu wa eneo husika na kuongeza hadhi ya eneo hilo…leo hatuangalii nyimbo za wamasai ila tunanunuA MAKHIRIKHIRI kwa raha zooote huku tukijiona tumeendelea!

  Kumbuka pia utamaduni hapa pia ni kurithisha vizazi vijavyo mambo ambayo kizazi cha sasa kinafanya, kama kulima, kufuga nyuki, kuchimba madini , kutengeneza vitu mbali mbali! kurithisha kizazi kijacho.......this is called informal education which is sometime far better than formal education!!

  kuna faida gani kumaliza na degree uchwara ya uhandisi wa ujenzi na huwezi kazi wakati kuna fundi aliyejifunza tangu utotoni alianzia kubeba vifaa vya baba yake!!! anajua kila kitu kuliko injinia aliyekuwa na stress za bodi ya mikopo na shida za kukosa vifaa vya mafunzo??


  4.
  Faida ya kukusanya mawazo

  Unapoona mwenzio kaendelea utajiuliza how? Kafanyaje? Maendeleo ya baadhi ya sehemu Fulani Fulani zitaleta ‘data collection' na mawazo kuwa kwa nini wengine wameendela wanafanyaje fanyaje.

  Sera za majimbo zinaweza kupelekea kubadilisha sera za uongozi wa taifa na kufikia kufanya maamuzi ambayo huwezi kuyajutia na una mifano yake.


  5.
  Kulinda Rasilimali za Taifa

  Kumbuka ikiwa kama majimbo yatagawanywa na kuwa mfumo wa states….basi taifa la Tanzania lina weza kuitwa ‘United Sates of Tanzania' majimbo ambayo yana dola ya local na kitaifa, kulinda maeneo husika.

  Ukiwa na mali lazima ulinde mali…kutorosha vitu kama wanyama hakutakuwepo, kuiba michanga ya madini hakutakuwepo, kukata miti ovyo na kuuza kwa bei ya kutupa hakutakuwepo!!! Do I need to say more here??...no!


  6.
  Kujenga Taifa Imara na viongozi wazuri wa kitaifa


  Tuna taifa dhaifu kwa sababu tuna viongozi dhaifu! Tuna viongozi dhaifu kwa sababu tuna taasisi dhaifu, tuna taasisi dhaifu kwa sababu tuna familia dhaifu!


  Taasisi kama uongozi wa ngazi mbalimbali ukiwa makini unaleta viongozi makini, taasisi hata za kidini zinaweza kuchochea kupata viongozi wazuri na akina baba wazuri
  Ikiwa tyuna kiognozi wa jimbo Fulani aliweka strategy za kupata maendelao na yakaoneka, je hawezi kuwa ndio candidate mzuri wa wizara husika na hata taifa??

  Viongozi watakuwa judged na kazi zao za kwenye majimbo na tutakuwa na hakika ya kuwa atafanya jambo akiwa rais let say…sio kuwa na viongozi vimeo kama hawa wasasa ambao haujui katoka wapi, kafanya nini, anaweza nini, unashtukia tu kiongozi na kesho mnalia HAWEZI…kwani nani alisema anaweza??


  7.
  Mwingiliano wa watu


  Uzuri wa sera hizi kwa sababu tunaongelea taifa moja, mtu ataishi sehemua mabayo anajua atazichanga. ‘atatoka' atatengeneza fedha kulingana na akili zake na ujuzi wake!! Hili huleta maendeleo ya haraka kwa wenye akili! Sio wanaokalia majungu, kuchezabao na kuwaza uchawi!

  Sera za majimbo kwa maendeleo ya Taifa, kumbuka kuna limitation zako au hasara zake, japo ni ndogo sana kw ataifa letu change sera za majimbo is not a matter of discussion…is a must!!

  8. Kodi husika

  Kodi inakatwa kulingana na eneo husika, kwa mfano kodi ya jimbo la Ontario nchini kanada iko tofauti na kodi ya British Columbia japo wako nchi moja, ukasanyaji wa kodi utakuwa rahisi na itafanya kazi iliyokusudiwaLeo hii kaodi zetu hatujui zinafanya nini na haujui umuulize nani! Aibu

  9. Watu watapungua DSM (miji mikubwa) ha ha ha ha!!

  I hate DSM but I am in!..ila nina kazi yangu na some prospects…ila naona watu wakitaabika, hawajui wafanye nini, hawana future, asubuhi tunajaziana foleni wengine wakiwa na decent jobs wengine hawana na cha ajabu ambao hawana kazi wanaishi maisha mazuri kabisa…sisi wafanya kazi tunakatwa kodi kubwa na ilimradi vituko tupu

  Hawa wenyeji wengi waDSM ambao ni jobless ambao wanaweza kwenda elfu arobaini kwenye msiba wa kanumba siku ya kazi asubuhi..wakisikia wenzao mikoani wanazalisha na maisha yao yanaenda vizuri watarudi tu!!

  Hata kama wasipoondoka hawa kwasababu wameishalemaa at least tutazuia watu kukimbilia mijini. Maisha ya bahati bahati , maisha yasiyo na muda wala malengo…maisha ambayo unatoka nyumbani saa kumbi na mbili na kufika kazini saa nne!!

  Unafikia chai,kucheza karata kufacebook kidogo, lunch na unasinzia kidogo saa tisa unaanza kuangalia usafiri wa kurudi…asilimia 90 ya wafanya kazi wa serikalini ndio wanavyoishi!! Ha ha ha ha!


  Watu hukimbilia mijini wakidhani ndiko kuna hela, sera ya majimbo itazuia hili! Japo hatari yake ni kuwa jimbo Fulani kukiwa kuzuri zaidi watu watakimbilia huko….

  lakini kama wanazalisha is okay hakuna shida, siyo kama wakazi wa DSM wengi…hawaishi bali wanatafuta maisha!


  10.
  inatosha

  wenu

  Waberoya s. Waberoya

  N.B huu sio uchambuzi wa sera rasmi ya chadema, maneno rasmi ya sera za chadema kuhusu hili , tafuta sera zake fika ofisi ya chadema iliyo karibu nawe utaipata, hapa nimeelezea tu kwa ufahamu wangu ubora wa sera hii, kumbuka pia kuwa mimi sio mwana chadema wala chama chochote cha siasa.
   
 2. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #2
  May 18, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mkuu Waberoya ulichoandika ni sahihi sana. Hii system ya sasa imesha fail.
   
 3. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  Huwa sikubaliani na wewe kwa mengi lakini hapa lazima niseme umegonga penyewe. Laiti viongozi na watanzania tungefuata ushauri huu nina matumaini tungeenda mbali sana. Na labda niseme mimi nafikiria huenda sehemu nyingi za Afrika zina matatizo kwa sababu ya ukubwa wa maeneo ya utawala. Ni kazi sana sana kuongoza nchi kubwa kama Tz kutoka sehemu moja. Ni kazi sana sana. Na viongozi wetu wanaonekana kama hawajalitambua hili au wanalitambua lakini kwa sababu ya hofu ya kupoteza nguvu za madaraka wanakataa kujaribu hii system. Hongera Waberoya kwa kuleta huu mjadala. Hii ndio mijadala ya Great thinkers!!!!
   
 4. Mbassa

  Mbassa JF-Expert Member

  #4
  May 18, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 247
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 45
  Waberoya, umenisaidia sana kuielewa vizuri hii sera ya majimbo. Ni sera nzuri sana na namtakia kila mwenye mapenzi mema na nchi hii aiunge mkono. Nawashangaa sana wanaoipotosha sera hii kwa manufaa yao binafsi! Tena ya kisiasa. Nawaomba makamanda wanapoendelea na M4C waelimishe wananchi pia kuhusu hii sera maana wengi hawajaielewa vizuri.
   
 5. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,840
  Likes Received: 471
  Trophy Points: 180
  Ni sahihi kabisa,ni lazima liwepo kapu la taifa ambako kila jimbo litachangia kwa ajili ya serikali kuu ili kuziba slacks.hapo tanzania utaona itakavyokimbia na uchumi wa kupaa.itakuwa mfano Afrika hasa EA.kAGAME sasa hivi anatukimbiza vibaya.
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  May 18, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  kweli wakati tunashindana na issue ya globalisation ambayo tumeachwa nyuma sana

  ili kwenda kasi lazima tubebe sera zenye kutupeleka kasi, ubinafsi na kupindisha ukweli hakutasaidia hili

  CCM wakiona kama vipi waichukue tu hii sera kwani dhambi??
   
 7. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Wabeloya, katika serikali za Majimbo, Zanzibar itakuwa Jimbo au itaendelea na status yake ya sasa kisha kuwe na Jimbo la Unguja na lingine la Pemba? Swali hili ni la msingi kama tutaendelea na muundo wa sasa wa muungano au kama tutaopt muundo wa serikali tatu.

  Swali la Pili, nimeona kunasehemu unatoa maelezo yanayomaanisha kwamba serikali za majimbo ni vehicle ya utajiri, unamaanisha watu wote watakuwa matajiri au majimbo yatakuwa matajiri?

  tusaidie kutuwekea sketch ya majimbo, sababu haiwezekani tukawa tunazungumzia hewani tu, mgawanyo wa majimbo utategemea na nini? kuna sehemu umesema muundo huu utawezesha kulinda tamaduni zetu, kwa maana gani? au majimbo yataundwa kwa misingi ya ukabila?

  Mwisho, kwa sasa, hili la kupunguza watu Dar es Salaam sijalielewa kabisa kabisa, naomba maelezo ya ziada.
   
 8. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #8
  May 18, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Mkuu mara nyingi nakuwa against you na nilishaleta mada ya wewe usiheshimiwe kabisa hapa jamvini,lakini kwa hili naanza kubadilika na kuiona point yako ilivyosimama,ingawa wakati mwingine unakuwa mgumu kueleweka lakini hii naona umeleta kama ABC inaeleweka na inakubalika 100%
   
 9. A

  Awo JF-Expert Member

  #9
  May 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Wabe, huko nyuma uliwahi kushauri, kama sijakosea, CDM waanze kutekeleza sera hii katika muundo wa uendeshaji wa chama. Sijui kama wamelipokea wazo hilo au vipi. Dr Slaa, kama upo, hebu lizungumzie hilo. Kuna ugumu gani kwa CDM kubadilisha katiba ili muundo wa chama uchukue sura ya majimbo?
   
 10. M

  Makupa JF-Expert Member

  #10
  May 18, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  nyie cdm kama mnataka kufutika kwenye ramani ya siasa endelezeni siasa zenu za majimbo , msisahau kwamba Nasari aliteleza kule arumeru then muda muafaka ukifika lazima wataalamu wataunganisha na swala la majimbo
   
 11. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #11
  May 18, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,660
  Likes Received: 3,310
  Trophy Points: 280
  Mkuu Waberoya!hii ndiyo moja kati ya hoja inayostahili hasa kujadiliwa na GF's,hasa kwenye kipengele cha Vigezo vya kumpata kiongozi bora,nakubaliana na wewe 100%kuwa kuwepo kwa serikali ya namna hii kutafanya majimbo yawe majiko ya kupikia viongozi walio bora,na itapunguza kazi ya mh rais ya kuokoteza viongozi mitaani,na kisha kujilaumu baada ya muda mfupi tu.asante mkuu umenipa mwanga.
   
 12. A

  Akamai01 Member

  #12
  May 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kaka ahsante kwa elimu.
   
 13. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #13
  May 18, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  nakubaliana na wewe japo kuna majimbo watu wake watakiona cha moto kutokana na hulka yao ya kutokupenda kujishughulisha.
   
 14. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #14
  May 18, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Wabeloya, Nigeria kuna serikali za Majimbo, WHERE ARE THEY NOW?
   
 15. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #15
  May 18, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Asante Mwalimu!
   
 16. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #16
  May 18, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  mkuu zanzibar itabaki kama nchi...!! wanajitawala wenyewe na watajua wenyewe huko kwao wajitawale vipi...! marekebisho katikba mpya tunatakiwa tuipunguzie zanzabar kutufanyia maamuzi upande wa bara! hizi hitilafu za muungano zitafutiwe suluhisho .. ikishindikana wapewe nchi yao

  Katika sera za CDM ... hii ya majimbo na support 100% ... ..! mfano.... tanga. + . moshi .+.kilimanjaro + arusha....! = jimbo moja !"nadhani hili litakuwa jimbo tajiri tanga wana bandari" arusha ina border na kenya.. tanga kuna border na mombasa ... ! kilimanjaro watalii ! LoL!.

  but nina wasiwasi kuna mikoa tegemezi ndani ya tanzania...! Ila Ni sera nzuri naunga mkono 100%
   
 17. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #17
  May 18, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mkuu Wabe,

  Nimeamua kuiprint na kuisoma vizuri maana hii inahusika sana.....,

  Thanks kwa uchambuzi.
   
 18. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #18
  May 18, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Waberoya nimeipenda hii licha ya kwamba kuna vijembe, vipepsi, vifuti, vigingi, yani evrising lol!
   
 19. REBEL

  REBEL Senior Member

  #19
  May 18, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Na watanzania hawasomi tu.Katiba mpya ya Kenya imeweka sera za majimbo na wataanza kutekeleza kama sikosei mwaka wa uchaguzi.Kutakuwa na ma-senators na governors.Sema nachouliza: mosi, ni Je sera ya majimbo Nigeria mbona haijafanikiwa?Pili,Ni wapi Nigeria wamekosea ili na nini tusirudie makosa yao?.Pia mimi nataka kutofautiana na wewe kuhusu miji mikubwa Arusha,mwanza,mbeya na dar itabaki kuvutia watu kutokana na mzunguko wa pesa uliopo,Kwa hilo sidhani kama sera majimbo itakuwa muarobaini wa watu kukimbilia DAR.Sema yatasaidia kutoa ukiritiba wa dsm kutawala na kumiliki raslimali yote ya Jamuhuri.Na kama watakata sera ya majimbo basi wakuu wa mikoa na wilaya inabidi wawe wanachaguliwa na wananchi wa sehemu husika na tuwape majukumu mengine katika mustakbari wa maendeleo ya mikoa yetu katika katiba mpya.na maamuzi yanabidi yasiwe yanatolewa na dsm.Mwisho viongozi amieni dodoma jamani.
   
 20. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Hata mie naunga mkono kwa sababu umewafumbua mawazo wale wote ambao wamekuwa vinara wa kupinga sera hii. Nassari hakukosea wala hakuteleza ulimi alipo sema jambo hili bali alidhamiria na alicho fanya ni kuchokoza tu! Tatizo ni kwamba bado fikra za watu kuhusu jambo hili ni finyu na alijua wataelewa muda ukifika. Namshauri aendelee na msimamo wa kulisisitiza hili sababu watu wa Arumeru kwa mfano wakisimamia mambo yao wenyewe watakuwa na mafanikio makubwa kuliko kama ilivyo hivi sasa ambapo watu walitoka kwingine na kuuzaa mashamba yao bila ridhaa yao.

  Ukiona watu wana pinga jambo fulani sana kwa nguvu zote kama wanavyo fanya magamba katika hili jua kuna kitu. Big up Waberoya umetoa shule. Post jambo hili kwenye magazeti yanayo somwa sana ili wengi hata wa vijijini wasio na access na internet wajisomee.
   
Loading...