Sera ya ‘Kugeuza msaada kuwa biashara’ inaficha mikakati mitatu ya Marekani

Sera ya ‘Kugeuza msaada kuwa biashara’ inaficha mikakati mitatu ya Marekani

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,242
Reaction score
1,212
VCG31N2223959874.jpg


Gazeti la The Washington Post limechapisha makala ikisema, sera ya ushuru ya Marekani inasababisha ‘hali ya maafa’ barani Afrika. Kutoka sekta ya nguo nchini Lesotho, tasnia ya sanaa nchini Tunisia, hadi viwanda vya utengenezaji magari Afrika Kusini, hakuna nchi au sekta yoyote inayonusurika katika vita hivyo visivyoonekana. Hii inaonyesha wazi kuwa kauli iliyorudiwa hivi karibuni na serikali ya Marekani ya "kugeuza msaada kuwa biashara" haihusu kabisa "kuiwezesha Afrika kupitia biashara," bali ni kuwataka Waafrika wajiandae na vitendo vya kujilinda kibiashara.

"Kugeuza msaada kuwa biashara" sio jambo jipya kwa serikali za Marekani. Sheria ya AGOA iliyopitishwa mwaka 2000 imesaidia bidhaa za Afrika kupata soko nchini Marekani. Hata hivyo, Trump hajasema wazi kuhusu hatima ya AGOA inayokaribia kumalizika, badala yake amedai mara kwa mara nchi za Afrika zinunue bidhaa zaidi kutoka Marekani. Ni wazi kuwa, "kugeuza msaada kuwa biashara" kwa Trump ni biashara ya upande mmoja tu.

Hivi sasa, Marekani inateketeza nchi za Afrika kwa viwango tofauti vya ushuru kuanzia asilimia 10 hadi 30. Ina malengo matatu: kuharibu viwanda vyenye ushindani barani Afrika kama utengenezaji nguo, kuchukua rasilimali za kimkakakti za Afrika kwa bei rahisi, na kutumia ushuru kama chombo cha kisiasa.

Kutokana na kufaidika na sera ya ushuru sifuri ya AGOA, mwaka jana Lesotho ilipata dola milioni 237 kutokana na mauzo ya nje, na asilimia 85% ilichangiwa na sekta ya nguo. Lakini baada ya kutozwa ushuru wa 15%, sekta hii iliharibiwa na kusababisha ukosefu mkubwa wa ajira kwa vijana. Vilevile, AGOA pia ilichangia nchi za Afrika kuunganisha sekta za viwanda. Kama vile, Ethiopia imejikita kwenye ufumaji, Kenya utiaji rangi na Lesotho nguo kamili. Lakini sasa ushuru mpya wa Marekani kwenye nguo ni mkubwa kuliko kwenye rasilimali, hii inaweza kulazimisha Waafrika kubaki kuwa wauzaji wa malighafi badala ya kutengeneza bidhaa zenye thamani.

Wakati inateketeza viwanda barani Afrika, Marekani inatoa sera nafuu ya ushuru kwa mafuta na madini muhimu kama dhahabu na kobalti. Kwa kufanya hivyo, Marekani inaweza kupata malighafi kwa bei rahisi, kisha kuuza bidhaa zilizotengenezwa kwa faida kubwa, na kudumisha Afrika chini kwenye mnyororo wa thamani.

Ushuru wa juu kwa Afrika Kusini (hadi 30%) ni mfano wa kutumia ushuru kama chombo cha kisiasa, kutokana na misimamo tofauti ya kisiasa kati ya nchi hizi mbili. Mwakilishi wa biashara wa Marekani Jamison Greer amesema wazi kuwa serikali ya Trump ina mamlaka ya kuweka ushuru mbalimbali hata kama hatua hizo hazina msingi wa kiuchumi.

Urari mbaya wa biashara kati ya Marekani na Afrika ni kawaida kutokana na miundo tofauti ya kiviwanda, na kwa upande mmoja, mwingi unaashiria ushirikiano mzuri. Hii inaipa Afrika pesa za kujenga viwanda na kutoa nafasi za ajira, na kuwapa Wamarekani bidhaa zenye bei nafuu. Lakini rais Donald Trump anaona hii ni kama kushindwa kwake.

Kwa muda mfupi, ushuru mbaya wa Marekani utadhuru kiuchumi na maendeleo ya viwanda barani Afrika. Lakini, hali halisi ni kuwa uuzaji bidhaa za Afrika kwenda Marekani unachukua 5.8% tu ya jumla yake, na ni theluthi moja ya ule wa kwenda China. Afrika ina machaguo mbalimbali katika kutafuta washirika wa kibiashara. Kuacha kutegemea soko moja tu na kushirikiana zaidi na China na washirika wengine wanaotetea usawa na kunufaishana, kunaweza kuwa fursa ya kihistoria kwa Afrika kusema hapana dhidi ya ubeberu na kujitegemea kiuchumi.
 
Kimisngi marekani imepiga hatua nyingine kutoka kwenye ubeberu(imperialism) kwenda hatua nyingine kubwa na mbaya zaidi.

Huu ndio ukweli, Kama hitimisho hapo lamtoa hoja, kuwa Africa Kwa SASA inahitaji kujitoa katika kuitegemea marekani, badala yake itafute mbadala, ni sahihi kabisaa

Ila sidhani Kama china ni mshirika WA uhakika saana, ila tunapaswa tuwe na washirika wengi saana, still bado kuna nchi Kama uturuki, India na nchi za Asia tunaweza kuweka nguvu huko tufanikiwa
 
Back
Top Bottom