Sera ya Kuachina majimbo ya wana UKAWA iliifufua CUF bara, sio Maalim wala Lipumba

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,729
2,000
Baada ya ukawa kuundwa walikubaliana vyama wanachama viachiane majimbo, na hii mliona hata Lowassa na Duni haji kugombea urais kwa tiketi ya chadema, na mliona kura walizopata Lowasa na Duni kwenye uchaguzi ule. Isingekuwa Sera ya kuachiana majimbo CUF bara isinge ambulia hata jimbo moja maana Chadema walikuwa wamejipanga kubeba yote, na kwa sera hiyo mliona wabunge wa CUF maana hata wapiga kura wa chadema walihimizwa kuwapigia wagombea wa CUF kwa sababu mpango ulikuwa kuunda kambi imara, na ilikuwa Maalim akishinda Zanzibar, na Lowasa Bara basi ingekuwa rahisi kwa wao kufufua Katiba mpya ya JMT pia wangeunda Muungano wenye maslahi ya pande zote mbili, tofauti na sasa tunauona muungano wa nchi moja na nusu.

Leo watu wana mshabikia Lipumba aliyekimbia mapambano, hata wabunge wanaomuunga Lipumba ni kwa sababu wanafahamu ubunge wao au posho na mshahara wao uko mikonono mwa Lipumba. Lakini wamevumilia hadi mwisho kwa hilo nawapongeza wanaorudi kwasababu wanafahamu bila Lipumba hawawezi kugombea tena huko majimboni mwao kwa ticket za CUF maana anaye sign form zao ni Lipumba. Hata hivyo wote tuna fahamu kwa lililotokea CUF haita pata kiti hata kimoja siyo bara wala Zanzibar, na tutaisahau na huo ndio utakuwa mwisho wa kumsikia lipumba na Magdalena sakaya ,wataungana na akina Mrema, na Cheyo.

Kwa upande mwingine pia chadema watakuwa na maadui wawili CCM na ACT, maana hata kama hamtaki siasa za CUF zilikuwa zinalenga maeneo yenye waislamu wengi, na huko ndiko walikuwa na ngome ngumu, na sasa inaweza ikawa ngome ya ACT ama isiwe hivyo, badala yake ikawa ngome ya ccm na tukashuhudia mahasimu wawili wenye siasa za jino kwa jino yani ccm na chadema wakiyagombea na kuwaacha ACT wakitafuta hata mifupa yani madiwani katika maeneo hayo.
Kwa chadema Bara wana mtaji tayari isipokuwa kule Zanzibar itakuwa mvurugano, wapo ambao watarejea ccm kutoka CUF na ACT inaweza ikakumbwa na pepo la ccm ambalo hukumba CUF miaka yote kwamba watapokwa kura zao kwa kisingizio ni wageni hawakubariki kule na kuifanya ccm sasa ichukue Zanzibar kwa urahisi kabisa.

Lililo tokea lilikuwa mpango wa muda mrefu wa ccm kwa CUF, baada ya mataifa ya kigeni kuwalazimisha ccm kumrejeshea Maalim ushindi na tukashuhudia ubabe uliotokea, sasa wamepumua kwamba hakuna CUF tena hivyo Dr.shein analala bila hofu yoyote, na ccm itakwenda kwa wale waliotaka Maalim Seif apewe urais wake na kuwaambia sasa mtu wenu kaenda ACT na mgogoro Zanzibar hakuna hivyo sasa mtupe pesa tuendeshe nchi na kuwaletea maendeleo wananchi.

Mliona Juzi rais mstaafu alimtembelea Rais Magufuli hii haikuwa bahati mbaya, ilikuwa ni furaha ya msimamo wao ulioiponya ccm Zanzibar kuendelea kuwepo na muungao kuendelea kuwepo kwa angalao miongo mingine miwili kama huyu ACT hatokuwa na impact 2020.
kIKWETE alifurahi binafsi kwa sababu lolote lingetokea asinge epukwa kusemwa, lakini na hili lilipotokea la CUF kufa Zanzibar lazima asemwe kwasababu kwa vyovyote anahusika,iwe direct au indirect.

Walifahamu tangu mwanzo walipomrudisha Lipumba ni kama walijua nini kingetokea, na kimeokea hifo auheni ya mzigo huo Rais Mstaafu Kikwete lazima afurahi sasa wanafahamu ni kucheza na sharia mpya za mikutano yavyama vya siasa kutokuruhusu ACT ijijenge Zanzibar na Bara, ila hasa Zanzibar kwasababu wameona yaliyotokea hawatafumba macho na hawataruhusu ACT kamwe iwe na ngome Zamnzibar kama ilivokuwa kwa CUF. Mikutano marufuku Zanzibara na bara, na hta ikiruhusiwa wameambiwa ni MARUFUKU kuisema vibaya serikali iliyopo madarakani, eti ndiyo siasa za kistaarabu, wapinzani wana paswa kusifia na kupongeza wakati wakinadi sera za vyama vyao.

Mwisho ni mpongeze Zitto na ACT, lakini pia kijiingiza kwenye migogoro na serikali rasmi. CCM inataka wasiwepo, lakini wanalzimisha kuwepo na sasa tujiandae kuona yeye atafanyaje tofauti, ambacho chadema wameshindwa. bahati aliyo nayo Maalim anakubalika Zanzibar lakini Bara, lkutakuwa na walakini. Zitto asipogombea ubunge kigoma 2020, kwa vyovyote hatorudi bungeni, hawezi kuwa rais na hana ushawishi bara kugombea urais na akashinda.

Hivyo CUF lipumba wasahau kuchaguliwa labda wateuliwe na rais wa ccm kama ilivyo tokea kwa Mbatia na Mrema, na RC wa Kilimanjaro, lakini isipotokea hakuna mbunge wa CUF anarudi bungeni, maana hakutakuwa na kuachiana majimbo tena. Na Lipumba keshaonekana ni mali ya ccm hivyo ni ngumu kuaminika tena kama mpinzani.

Haikuwa sera za CUF kama Lipumba alivyokuwa akitamba kwamba ndizo ziliiwezesha CUF kupata wabunge bara, ni sera ya UKAWA ya kuachina majimbo iliiwezesha CUF kupata wabunge. Ajiandae ki saikolojia sasa, labda aachiwe jimbo na ccm, otherwise hakuta kuwa CUF bungeni baada UCHAGUZI WA 2020. Furaha yao ya mwisho ni hii kuweza kumuondoa Maalim Seif CUF.
 

shungurui

JF-Expert Member
Sep 1, 2008
3,757
2,000
Huu ndio kweli na wanaujua ila wanajifanya hawauoni, au ndio mkakati yao fake ili wapiga hela ya jiwe, wajinga ndio waliwao,.ila safari bado inaendelea.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,729
2,000
Mods naombeni mbadirishe kichwa cha habari kisomeke "Kuachiana" siyo kiachina, tafadhalini
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom