Sera ya Faragha ya Google iliyofafanuliwa kwa Kiswahili isome na uielewe

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
630
957
Watu wengi hutumia mtandao na miundombinu ya internet inayoendeshwa na Kampuni ya Google bila ya kusoma na kuelewa Sera ya Faragha, pitia sehemu ya sera hii kwa kusoma maelezo yafuatayo;

Unapotumia huduma zetu, unaamini kuwa tutalinda maelezo yako. Tunaelewa kuwa hili ni jukumu kubwa na tunafanya tuwezalo ili kulinda maelezo yako na kuhakikisha kuwa unaweza kuyadhibiti.

Sera hii ya Faragha imekusudiwa kukusaidia uelewe maelezo tunayokusanya, sababu za kuyakusanya na jinsi unavyoweza kusasisha, kudhibiti, kuhamisha na kufuta maelezo yako.

Inatumika kuanzia 15 Oktoba 2019 | PDF imeambatanishwa kwenye uzi huu.



Tunaunda huduma mbalimbali zinazosaidia mamilioni ya watu kuwasiliana na kufahamu yanayotukia ulimwenguni kote kila siku kwa njia mpya. Huduma zetu zinajumuisha:

  • Programu, tovuti na vifaa vya Google kama vile Tafuta na Google, YouTube na Google Home
  • Mifumo kama vile kivinjari cha Chrome na mfumo wa uendeshaji wa Android
  • Bidhaa ambazo zinatumiwa na programu na tovuti nyingine, kama vile matangazo na Ramani za Google zilizopachikwa
Unaweza kutumia huduma zetu kwa njia mbalimbali kudhibiti faragha yako. Kwa mfano, unaweza kufungua Akaunti ya Google ikiwa ungependa kuunda na kudhibiti maudhui kama vile barua pepe na picha, au kuona matokeo ya utafutaji yanayokufaa. Unaweza pia kutumia huduma nyingi za Google ukiwa umeondoka katika akaunti au hata ukiwa huna akaunti kama vile kutafuta kwenye Google au kutazama video kwenye YouTube.

Pia, unaweza kuvinjari wavuti kwa faragha katika Hali fiche ukitumia Chrome. Unaweza kubadilisha mipangilio yako ya faragha kwenye huduma zetu zote ili udhibiti maelezo yako tunayokusanya na tunavyoyatumia.

Ili tuweze kufafanua mambo wazi kabisa, tumejumuisha mifano, video zenye maelezo na ufafanuzi wa masharti muhimu


Maelezo ambayo Google hukusanya
Tungependa ujue maelezo tunayokusanya unapotumia huduma zetu

Sisi hukusanya maelezo ili kutoa huduma bora kwa watumiaji wetu wote — kutoka kubashiri vitu vya msingi kama vile lugha unayozungumza, hadi vitu changamani zaidi kama vile matangazo yanayokufaa, watu muhimu sana kwako mtandaoni, au video ambazo huenda utapenda kwenye YouTube. Maelezo yanayokusanywa na Google na jinsi yanavyotumika inategemea unavyotumia huduma zetu na unavyodhibiti vidhibiti vyako vya faragha.

Ikiwa hujaingia katika Akaunti ya Google, sisi huhifadhi maelezo ambayo tumekusanya kwa kutumia vitambulishaji vya kipekee vilivyojumuishwa ndani ya kivinjari chako, programu au kifaa unachotumia. Hii inatusaidia kutekeleza mambo kama vile kudumisha lugha unayopendelea unapovinjari kokote.

Ukiwa umeingia katika akaunti, sisi hukusanya pia maelezo tunayohifadhi kwenye Akaunti yako ya Google na tunayachukulia kuwa maelezo ya binafsi.

Maudhui unayounda au kutupa
d1b68e2cd423aba52d74f02573df2d2d.svg

Unapofungua Akaunti ya Google, unatupa maelezo ya binafsi yanayojumuisha jina na nenosiri lako. Unaweza pia kuongeza nambari ya simu au maelezo ya malipo kwenye akaunti yako. Hata ikiwa hujaingia katika Akaunti ya Google, unaweza kutupa maelezo — kama vile anwani ya barua pepe ili upokee taarifa kuhusu huduma zetu.

Sisi pia hukusanya maudhui unayounda, unayopakia, au kupokea kutoka kwa watu wengine unapotumia huduma zetu. Hii inajumuisha vipengee kama vile barua pepe unazotuma na kupokea, picha na video unazohifadhi, hati na malahajedwali unayounda na maoni unayotoa kwenye video za YouTube.

Maelezo tunayokusanya unapotumia huduma zetu

Programu, vivinjari na vifaa vyako
e79ea0ed464fc8952d5b5582f9f9ae53.svg

Google hukusanya maelezo kuhusu programu, vivinjari na vifaa unavyotumia kufikia huduma zake. Hii hutusaidia kutoa vipengele kama vile masasisho ya kiotomatiki ya bidhaa na kipengele cha kupunguza ung'avu wa skrini ikiwa betri yako inakaribia kuisha chaji.

Maelezo tunayokusanya ni pamoja na vitambulishaji vya kipekee, aina na mipangilio ya kivinjari, aina na mipangilio ya vifaa, mfumo wa uendeshaji, maelezo ya mtandao wa simu ikiwa ni pamoja na jina la mtoa huduma na nambari ya simu na nambari ya toleo la programu. Sisi hukusanya pia maelezo kuhusu mawasiliano kati ya programu, vivinjari na vifaa vyako na huduma zetu, ikiwemo Anwani ya IP, ripoti za kuacha kufanya kazi, shughuli za mfumo na tarehe, saa na URL ya kuelekeza ya ombi lako.

Tunakusanya maelezo haya wakati huduma ya Google kwenye kifaa chako inawasiliana na seva zetu - kwa mfano, unaposakinisha programu kutoka kwenye Google Play au wakati huduma inatafuta masasisho ya kiotomatiki. Ikiwa unatumia Kifaa cha Android chenye programu za Google, kifaa chako kitawasiliana na seva za Google mara kwa mara kutoa maelezo ya kifaa na muunganisho kwenye huduma zetu.

Maelezo haya yanajumuisha mambo kama vile, aina ya kifaa chako, jina la mtoa huduma, ripoti za kuacha kufanya kazi na programu ulizosakinisha.

Shughuli zako
39b031d352a2e1586cf50ac7f2bbc18b.svg

Sisi hukusanya maelezo ya shughuli zako kwenye huduma zetu. Maelezo haya hutumika kutekeleza mambo kama vile kukupendekezea video ambazo huenda ukapenda kwenye YouTube. Maelezo ya shughuli tunayokusanya yanajumuisha:

  • Hoja unazotafuta
  • Video unazotazama
  • Unavyotazama na kutumia maudhui na matangazo
  • Maelezo ya sauti na matamshi unapotumia vipengele vya sauti
  • Shughuli za ununuzi
  • Watu unaowasiliana au kushiriki maudhui nao
  • Shughuli zako kwenye programu au tovuti nyingine zinazotumia huduma zetu
  • Historia yako ya kuvinjari kwenye Chrome ambayo umesawazisha na Akaunti yako ya Google
Ikiwa unatumia huduma zetu kupiga au kupokea simu au kutuma na kupokea ujumbe, tunaweza kukusanya maelezo ya kumbukumbu ya simu kama vile nambari yako ya simu, nambari ya anayekupigia, nambari ya unayempigia, nambari za kusambaza kwa simu, saa na tarehe ambayo simu zilipigwa au ujumbe ulitumwa, muda uliotumika kuongea kwenye simu, maelezo ya kutuma ujumbe na aina ya simu zilizopigwa.

Unaweza kutembelea Akaunti ya Google ili upate na kudhibiti maelezo ya shughuli ambayo yamehifadhiwa katika akaunti yako.

0d6da8d8c44e7e3ee95c4d56c19f04e1.svg

Nenda kwenye Akaunti ya Google
Maelezo mahali ulipo
4c5ee41d52605ff6f43538d46a1c0d35.svg

Tunakusanya maelezo ya mahali ulipo unapotumia huduma zetu. Maelezo haya hutusaidia kutoa vipengele kama vile ramani ya kukuelekeza unapoendesha gari kwa mapumziko ya wikendi au kukuarifu kuhusu filamu zinazochezwa karibu nawe.

Mahali ulipo panaweza kukadiriwa kwa kutumia:

  • GPS
  • Anwani ya IP
  • Data ya sensa kutoka kwenye kifaa chako
  • Maelezo kuhusu vitu vilivyo karibu na kifaa chako, kama vile maeneo ya kufikia Wi-Fi, minara ya mitandao na vifaa ambavyo vimewashwa Bluetooth
Aina za data ya mahali tunazokusanya zinategemea kwa kiwango fulani mipangilio ya kifaa na akaunti yako. Kwa mfano, unaweza kuwasha au kuzima kipengele cha mahali kwenye kifaa chako cha Android ukitumia programu ya mipangilio ya kifaa. Unaweza pia kuwasha kipengele cha Kumbukumbu ya Maeneo Yangu ikiwa ungependa kuunda ramani ya faragha ya unakokwenda ukiwa na vifaa vyako ambavyo umetumia kuingia katika akaunti.

Katika hali fulani, Google pia hukusanya maelezo yako kutoka kwenye vyanzo vinavyopatikana kwa umma. Kwa mfano, ikiwa umetajwa kwenye gazeti la eneo lako, mtambo wa kutafuta wa Huduma ya Tafuta na Google unaweza kunakili makala hayo katika faharasa na kuyaonyesha kwa watu wengine wakitafuta jina lako. Tunaweza pia kukusanya maelezo yako kutoka kwa washirika wanaoaminika, wakiwemo washirika wa biashara wanaotupa maelezo kuhusu wateja watarajiwa wa huduma zetu za biashara na washirika wa usalama wanaotupa maelezo ili kulinda dhidi ya matumizi mabaya. Pia tunapokea maelezo kutoka kwa watangazaji ili kutangaza na kutoa huduma za utafiti kwa niaba yao.

Tunatumia teknolojia mbalimbali kukusanya na kuhifadhi maelezo, vikiwemo vidakuzi, lebo za pikseli, hifadhi za ndani kama vile hifadhi ya kivinjari au akiba za data ya programu, hifadhidata na kumbukumbu za seva.

GOOGLE
 

Attachments

  • Google Privacy Policy.pdf
    416.4 KB · Views: 11
Siku utuandikie jinsi google na makampuni mengine yanavyopata faida ndio watu wataanza kusoma hizo kitu, ToS, Mtu mmoja aliziita Terms of Abuse
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom