Sera ya elimu 2014 Tanzania

AZUSA STREET

JF-Expert Member
Oct 31, 2013
2,007
1,894
Sera ya elimu tz imeruhusu kufundisha watoto wetu toka primary school hadi university kwa kutumia lugha mbili, yaani ukiamua mtoto aanze kiswahili basi atatumia kiswahili kama medium of instruction hadi chuo kikuu, na ukiamua kuanzia primary atumie kiingereza basi atatakiwa kwenda na kiingereza hivyohivyo hadi univerity. nimejiuliza maswali mawili.

1. je? tutakuwa na vyuo vikuu vya aina mbili? vyuo vikuu vya kiswahili na vile vya kiingereza?

2. unawezaje kuwaweka pamoja katika chuo kimoja watu waliotoka kwenye mikondo ya lugha mbili tofauti? yaani mtu aliyesoma kwa kiswahili elimu yake yote na yule aliyesoma kwa kiingereza elimu yake yote wakutane chuo kikuu kimoja, watasoma course ile ile wengine wanasoma kwa kiingereza na wengine wanaisoma kwa kiswahili?

3. kama wakiwekwa pamoja na vitabu vingi vya chuo kikuu vimelalia kwenye kiiingereza na waandishi wengi sio watanzania, je, tutatafsiri vitabu vyote viwe kiswahili? au je, wale wa kiswahili wataswitch kwenda kiingereza wakifika university?

4. kama mtu ameanza kusoma kwa kiingereza kuanzia secondary school, A level hadi university lakini kiiingereza bado haongei vizuri, je, akitumia kiswahili secondary na A level akakutana na kiingereza university ataelewa anachokisoma? wameshindwa wale walioanza tangu secondary utaweza wewe unayeanzia kujifunza kiingereza university halafu ukitumie kwenye kusomea degree?

5. tukiweka matabaka haya mawili, mbona kutakuwa na watz wa kiswahili na watz wa kiingereza, tabaka hilo litakuwepo mtaani, litakuwepo makazini watu wanapoajiriwa, litakuwepo maeneo yote. kwanini tunawabagua watz wagawanyike namna hii?

6. pendekezo langu, WATOTO WASOME kwa KIINGEREZA KUANZIA chekechea HADI UNIVERSITY.

7. wale wote wanaoshabikia watoto wafundishwe kwa kiswahili, watoto wao wanasoma english medium schools. mimi nimesoma shule kayumba, na sitataka mtoto wangu yeyote asome kayumba, watoto wangu watasoma kiiingereza tangu chekechea hadi university na kama nikiona tz wamezingua kulazimisha tusome kwa kiswahili ambacho hakitusaidiii, watoto wangu nitawapeleka hata uganda, kenya au zambia wakasome huko wakimaliza watarudi. ila kamwe watoto wangu hawatasoma kwa kiswahili kwasababu nimeona umuhimu wa kiingereza katika dunia hii ya utandawazi, mtu ukiwa fluent kwenye kiingereza unafanikiwa mambo mengi sana kimataifa, unapata confidence na unaaminika.

8. kama Rwanda wameamua watoto wao wote wasome kiingereza, kwanini tz tusiseme watoto watumie kingereza tu na kiswahili tutakiongea mtaani?au wanaogopa tutasahau kiswahili?

9. tangu ujue kiswahili, kimekusaidia nini kimataifa?

10. watu wanajilinganisha na japan, china etc kwamba wanatumia lugha zao na wameendelea, wale walishaendelea, sisi tukitumia kiswahili, wakati uchumi wetu wote, biashara zetu zote tunahitaji kuzitangaza kwa kiingereza, kuzisambaza kwa kiingereza etc, tuna mvuto gani wa kumfanya mtu asiyejua kiiswahili ajifunze ili aje afaidike na Tanzania, manake ukienda ujerumani unatakiwa kujifunza kijerumani, so is china na japan, ili uweze kufanya mambo yako kule, lakini sisi tunajibembeleza kwao kuliko wao kujibembeleza kwetu hivyo ni sisi tunaotakiwa kujifunza lugha zao. imagina ungekuwa haujui kiingereza kabisa leo, namna ambavyo ungekuwa kipofu wa mambo mengi yanayoendelea duniani? hivi hawa watunga sera wameenda shule kweli?
 
sera ipo kwenye mtandao mkuu. tafuta utaipata, download kaisome home upendavyo.
 
Mleta mada umeelezea jinsi unavyohisi. Eti kutakua na 2 options, kama utataka usome kwa kiingereza au kiswahili.

Mimi nimeisoma sera. nimeona matamko mawili. Kwa upande wangu nimeshindwa kujua ni jinsi gani hayo matamko mawili yatafanikiwa kwa wakati mmoja, kuna maandalizi gani mpaka sasa, na ni lini hayo matamko yataanza kutekelezwa.

Matamko yenyewe ni haya:
1. Lugha ya taifa ya kiswahili itatumika kufundishia na kujifunzia ktk ngazi zote za elimu na mafunzo na serikali itaweka utaratibu wa kuwezesha matumizi ya lugha hii kua endelevu na yenye ufanisi ktk kuwapatia walengwa elimu na mafunzo yenye tija kitaifa na kimataifa.

2. Serikali itaendelea na utaratibu wa kuimarisha matumizi ya lugha ya kiingereza ktk kufundishia na kujifunzia, ktk ngazi zote za elimu na mafunzo.
 
Ukiachilia mbali hayo matamko, kuna maelezo mazuri ya kuelezea umuhimu wa hizo lugha mbili. Tusipinge kila kitu. Tuangalia faida na hasara ya kitu husika, kwa kuangalia mifano ya nchi kadhaa zilizoamua kutumia lugha zao badala ya kiingereza.
 
Mi binafsi nakubaliana na hoja ya kutumia lugha yetu ya kiswahili katka level zote kujifunzia na kufundishia, lkn sera lazima itoe hatua za mda mfupi (10- 15yrs) na za mda mrefu(20 na kuendelea) kwa sababu swala hili ni kubwa na la muhimu, ambalo linajumuisha gharama kubwa sana na utafiti wa kutosha.
 
Back
Top Bottom