Uchambuzi wangu mechi ya jana
Ukweli ni kwamba kwa Simba na Yanga furaha ya ushindi huwasahaulisha mambo mengi mfano ni pale ambapo ushindi wa jana umetusahaulisha kabisa kipigo cha ZESCO halii hii hufanya tushindwe kufanya tathmini ya kina ya mchezo wenyewe
- Simba ilianza na Mfumo wa 3-5-2 ambapo Gallas (William Lucian) alitakiwa kuanzisha mashambulizi kutokea mwanzo akichukua mipira toka kwa mabeki na kumsukumia Awadh Juma ambaye alikua Holding midfielder kwa jana, Awadh alitakiwa kumsoma Kigisa/Okwi/Maguli na kurusha high balls, Simba iliua wingi ya kushoto kwa kuwa na viungo wengi katikati.......kwa kuwa Gallas hakutimiza majukumu yake huku akichanganyana na Awadh, ilibidi atolewe na nafasi yake kuchukuliwa na Uhuru Sellemani hapo ndipo mfumo ulibadilika na kuwa 4-4-2 Mashambulizi yakitokea pembeni sasa!!! na Simba ndio ilianza kucheza mpira wa kuonekana..na viungo kupiga pasi za mwendo
- Ivo Mapunda amebadilika sana (Of course falsafa ya makipa inasema kwamba unavyozidi kuzeeka ndio unakuwa mzuri zaidi) Ivo anacheza krosi, hatemi na anafika kwenye matukio hatari....sasa Simba ina golikipa na si mlinda lango
- Mbavu ya Abdi Banda ni nzuri ila anaonekana anataka muda sana kucheza soka a ushindani, ni mtu anayejua kukaba kwenye njia lakn anatakiwa achezeshwe winga mazoezini ili apate uchungu wa buti (kugongwagongwa)na ndipo anaweza kuja kukaza uwanjani
- Miraji Adamu alicheza vizuri lakn baada ya kugongwa kidogo alipotea ila ni mrithi mzuri sana wa Chollo, (sema pia aliyemkaba anajua soka) anaonekana pia anahitaji mazoezi mengi ya tumbo apate wepesi sababu beki ya pembeni ndio mbavu za mbwa kwa timu (kupanda na kushuka) vitu ambavyo Abdi Banda anavikosa pia
- Owino alicheza vizuri na kwa majukumu aliyonayo sasa (kusafsha makosa ya chipukizi) anayaetendea haki (na beji ya Unahodha)
- Isihaka Hassan hafahamiki sana miongoni mwa wapenzi wa soka lakn ni lulu kwa Simba hapo usoni japo kwa muda fulani alionekana kucheza kindondo zaidi (kubutua pasipostahili)-Alipandishwa toka timu B NA SIMBA ILITAKA KUMPELEKA KWA MKOPO
- Awadhi Juma anaongeza ushindani kwenye dimba la chini (kumbuka Mkude na Kwizera wanasubiri), alicheza vizuri sana na anaonesha ana pumzi ya muda wote na anajua NJIA ZA MPIRA-Simba hawatajuta kutompleka Stand United kwa mkopo
- Okwi hakua mchezoni kipindi cha kwanza japo alionesha kupania ila bado uwezo wake ni uleule na hakika si mchezaji wa dk 90 na bado hakuweza kutengeneza kombinenga nzuri na Kiongera japo alimpasia pasi/krosi ya goli la kwanza
- Kisiga naweza kusema ndiye fundi wa pasi za mwisho kwa sasa na ana bahati ana watu wanaozijua na kuzitendea haki pasi zake, ana tatizo la kuchoka kuna muda wa mwishoni alikua anakaba kwa macho na kubweteka na mashabiki kwa kucheza show game (kanzu matobo nk ambavyo vingeigharimu timu) lakn nadhani Ndemla/Hajib/Kiemba wanaweza kupokea mikoba yake pindipo achokapo, naona pia amepungua kupiga mashuti anapotazama lango
- Muguli anahitaji kucheza kwa nafasi na kutumia nguvu zake kupiga mashuti mengi, kwa fowadi ya Simba sasa anapaswa kuanzishwa kuwachosha mabeki wa timu pinzani ili anapoingia Kiongera/Tambwe anafunga tu kirahisi kama ilivyokuwa jana'
- Uhuru anacheza na Jukwaa na hasaidii timu ama badu anahodhi mipira lakn anaangalia chini hivyo kupoozesha timu na kuishambulia badala ya kushambulia.........
- Kiongera ni mzuri lakn ni mzito anahitaji mazoezi kuendana na kasi za akina Okwi, Tambwe na wengine
- Huyu Ibrahim Hajib anatakiwa kupewa mechi nyingi azoee mashabiki (pia Banda)...alipiga shuti moja la hatari kitu kinachoonesha ameoata stamina tofauti na alivyokuwa B
- Ibrahim Twaha anapapara sana uwanjani, huyu alitakiwa kwenda kwa mkopo timu fulani ili arudi kwa adabu na kwa staili ya Simba
- Shabalala alionyesha uwezo wa kumudu shavu la kushoto na Banda aangalie sana, anapanda na kushuka ingawa si mmiminaji wa krosi BOMBA kama alivyokua Twaha Hamidu, au AMIR MAFTAH
- Cholo umri na maumivu vimemgharimu sana ingwa Ng'ombe hazeeki maini
- Simba imekuwa na mchanganyiko mzuri maana sub zina maana na hii inamrahishia kazi Mwalimu
Kwa ujumla si vyema kutathmini uwezo kwa mechi moja tu na pia USHINDI/UBORA wa Simba ya sasa usiwe ni kigezo kwamba itaifunga Yanga kirahisi (kama mashabiki walivyoanza kutabiri baada ya mechi jana), uzoefu unaonesha kwamba timu inayokua nzuri ndiyo hufungwa na pia LIGI si Yanga tu
Itaendelea............................