Separation VS new relationship is it right?

EMT I got you, thanks! Kuhusu trial nafikiri ni wewe, coz acording to Erotica n me u have passed already. What am I thinking with? It gotta be my brain. LOL
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: EMT
EMT I got you, thanks! Kuhusu trial nafikiri ni wewe, coz acording to Erotica n me u have passed already. What am I thinking with? It gotta be my brain. LOL

Let's see. Maama unawezasema ni brain lakini baada ya trial ukaanza kufikiria with your heart na kutaka mazima mazima kabisa huku Erotica akiachwa solemba mchana kweupeeee.
 
Last edited by a moderator:
mimi nadhani hata huko kutaka divorce katika miezi 8 tu ni muda mfupi sana, kwanini una haraka ikiwa mwenzio bado hataki, which means anataka muwe na muda wa kutafakari zaidi kama kweli mnataka kuachana. kuanza mahusiano katika miezi 8 pia ni mapema kupita kiasi, inaanza kunipa wasiwasi mimi binafsi kua huenda wewe ndio una matatizo, sitaki ku conclude hivi lakini, nahisi tu. unaomba divorce haraka haraka kama unataka kuoelewa au kuoa tena, ndicho mnachotaka kufanya? kama sivyo basi naomba usubirie hiyo divorce na hayo mahusiano mapya. mfano mzuri, mimi pia nime separate kwa miaka kadhaa, sijawahi hata kuwaza ku divorce, maana sioni sababu ya msingi kwa sasa, maybe later.
kama mwenzio hakusumbui achana na hiyo divorce, muhimu lea watoto wako na achana na mahusiano mapya maana hakuna malaika, sanasana utaumia zaidi.
 
....Pole sana.... kama hutajali unaweza kuweka hapa sababu za kuamua kuvunja ndoa yako? Maana usije kuruka mkojo ukakanyaga kinyesi hasa ukitilia maanani kwamba mwenzako hataki kuivunja ndoa yenu na pia kwa kuwa mna watoto wawili tayari...Binadamu hubadilika na hivyo labda anaweza kabisa kubadilika na kuwa mume mwema na ndoa yenu kuimarika zaidi kutokana na hayo mabadiliko ambayo anaweza kuyafanya ili kuhakikisha unampa nafasi nyingine. Pole sana.
 
Nilisoma kule fesibuku: dating ur ex (hapa nachukulia huyu shosti karudisha moyo) is like buying the same book that you have been reading over and over again. Namaanisha hakuna mupya!
Mamito! Trust your guts, but lead your heart and don't just follow it. LEAD IT! Bible inasema 'moyo ni mdanganyifu kuliko vitu vyote..'
Kila la kheri.
 
mimi nadhani hata huko kutaka divorce katika miezi 8 tu ni muda mfupi sana, kwanini una haraka ikiwa mwenzio bado hataki, which means anataka muwe na muda wa kutafakari zaidi kama kweli mnataka kuachana. kuanza mahusiano katika miezi 8 pia ni mapema kupita kiasi, inaanza kunipa wasiwasi mimi binafsi kua huenda wewe ndio una matatizo, sitaki ku conclude hivi lakini, nahisi tu. unaomba divorce haraka haraka kama unataka kuoelewa au kuoa tena, ndicho mnachotaka kufanya? kama sivyo basi naomba usubirie hiyo divorce na hayo mahusiano mapya. mfano mzuri, mimi pia nime separate kwa miaka kadhaa, sijawahi hata kuwaza ku divorce, maana sioni sababu ya msingi kwa sasa, maybe later.
kama mwenzio hakusumbui achana na hiyo divorce, muhimu lea watoto wako na achana na mahusiano mapya maana hakuna malaika, sanasana utaumia zaidi.

Umeona eeh!...halafu mahusiano mapya yakishindikana inakuwa tabu nyingine.
 
Let's see. Maama unawezasema ni brain lakini baada ya trial ukaanza kufikiria with your heart na kutaka mazima mazima kabisa huku Erotica akiachwa solemba mchana kweupeeee.

EMT it takes 2 pumping hearts to chukuana mazima mazima; so l won't be the only guilty one! LOL
Ikitokea, Erotica si anahitaji Mbegu tu? Nitamruhusu, na good things, tunaweza zitoa hata kwenye mfuko na kumpa! LMAO
 
Last edited by a moderator:
Umeona eeh!...halafu mahusiano mapya yakishindikana inakuwa tabu nyingine.

BAK n Sal ni muda gani sasa asubiri before start seing someone? Sal umesema umeseparate for few years now; sex life yako ikoje? Unafikiri wote wanaweza ishi 2 yrs bila sex? Na unajua (according to some people hapo juu) kuwa kutoka na mtu mwingine ukiwa katika hiyo separation ni cheating?

Mimi nafikiri wewe bado una mapenzi na mumeo, hii si case kwa mleta mada na sidhani kuwa case zenu zafanana!
 
@Kaunga sijui sababu za huyu dada kuamua kuvunja ndoa yake...Mumewe bado anampenda vinginevyo naye angeshanyoosha mikono juu kwamba ndoa ifikie tamati. Sasa kwa kuwa bado mumuwe anampenda kwanini asimpe nafasi nyingine katika ndoa yao!? au alishapewa nafasi siku za nyuma ili kubadilika na hatimaye kuimarisha ndoa yao hakufanya hivyo? Itakuwa vizuri kujua details ya kile kinachojiri ndani ya ndoa hii ili kuweza kumpa ushauri wa kina vinginevyo anaweza kabisa kupewa ushauri ambao si mzuri...Ni mawazo yangu tu.
 
BAK ukisoma post zake za nyuma utapata majibu yote, hadi polisi amepelekwa hoping ataxha kuwa abusive!

Mdada hadi kufikia hatua hiyo maana imeshindikana, kwani wanawake wengi (my mom included) huvumilia ndoano for the sake of kids.

Dada hajawa na mtu mwingine, lkn anajua it will happen ndio maana kauliza when is morally legally acceptable?

I am sure,angeanza na case yake (abusive marriage) na kuuliza avumilie au la; wengi wetu tungemshauri atoke kwenye hiyo ndoa (it happened before) lkn to me, case yake was so clear na she knew what she wanted ndio maana hakuileta humu kwa ushauri.

Alichokileta humu ndicho kinachomtatiza!
 
...Ahsante sana Kaunga muda ukiniruhusu nitaupitia tena uzi huu ili nifahamu kwa kina kilichojiri...mie nilisoma mwanzo tu na hivyo kuzikosa details nyingi zilizomfikisha huyu dada kuamua kuvunja ndoa yao...ndoa yoyote ambayo mume amefikia kumpiga mkewe haina thamani ya kuipa muda zaidi pale mke anaposema sasa basi maana mara nyingi mke ameshavumilia vipigo vingi sana.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana ila wewe ni dhehebu gani? Kama ni mkristu na ulikuwa mwaminifu mbele ya mungu,muombe sana afanye njia iliyooka maishani mwako. Usifikirie kwanza kuhusu kuingia kwenye mahusiano mapya kwani ulikiri mtakuwa pamoja katika shida na raha, shida mojawapo ndio hiyo,mfarakano katika familia, piga magoti nae atakusikia, ili upate suluhisho lazima ujue chanzo cha tatizo ndipo upate utatuzi wa tatizo halafu suluhisho/muafaka. Waweza kuwa wewe ndio chanzo bila kujua sasa hata ukienda kwa mwingine utajikuta mnaachana. Sikushauri kuingia kwenye uhusiano mda huu. Je! Mlifunga ndoa mahakamani? Kama la kwanini muende mahakamani na msiende kusuluhisha sehemu husika? Huwezi kupata ajali barabarani ukaenda kupima ajali baharini.

Kaa chini na fikiria kwa makini kwani hii ngoma inakuhusu zaidi wewe na si mtu wa pembeni.

+255754048974
 
  • Thanks
Reactions: Sal
Nilipomuuliza kuhusu sababu ya kutaka kuvunja ndoa yake my poin was kama ana sababu za msingi za kuvunja ndoa,kwa upande wangu sidhan kama atafungwa kwa njia yoyote kuanzisha mahusiano mapya muda WOWOTE akitaka.Ila kama hana sababu ya msingi hapo ndo uharam wa mahusiano mapya unapokuja.Hata kama atasubiri kwa muda gani bado atakua na hatia tu!
 
Tuacheni kuwa na mawazo ya kibinadam zaidi, ni vizuri kumshirikisha muumba wetu,je MWENYEZI MUNGU HAJUI TABU TUNAZOPITIA? MAJARIBU NI MTAJI WA IMANI, kufikiria kuna na mtu mwingine within 8 months inamaana hata mumeo akisafiri utafikiria opposite option, tulia na fungua ukurasa mpya,sahau matatizo yenu na mjadili future yenu na ya watoto, kwa mtu ambaye hajaoa wala kuolewa na kuwa mtoto hawezi jua dhamani ya ndoa au ya mzazi kwa watoto, mda huu watoto uko nao ila kuna kipindi watahitaji uwepo wa baba yao mzazi, sara alikaa zaidi ya miaka 60 bila mtoto mbona hakukimbia nyumba ya abraham ilihali ni mateso moyoni kwani wenzako wote wana watoto isipokuwa yeye.

Kemea pepo la mfarakano katika ndoa yenu, mkabidhi MUNGU kuwa mlinzi,kiongozi katika ndoa yenu,
 
BAK ukisoma post zake za nyuma utapata majibu yote, hadi polisi amepelekwa hoping ataxha kuwa abusive!

Mdada hadi kufikia hatua hiyo maana imeshindikana, kwani wanawake wengi (my mom included) huvumilia ndoano for the sake of kids.

Dada hajawa na mtu mwingine, lkn anajua it will happen ndio maana kauliza when is morally legally acceptable?

I am sure,angeanza na case yake (abusive marriage) na kuuliza avumilie au la; wengi wetu tungemshauri atoke kwenye hiyo ndoa (it happened before) lkn to me, case yake was so clear na she knew what she wanted ndio maana hakuileta humu kwa ushauri.

Alichokileta humu ndicho kinachomtatiza!

.....kinachoniumiza, wengi wanaompinga na kumkebehi ndio hao ambao wangetoa ushauri wa 'mpige chini!'......'mtafutie nyumba ndogo' -iwapo mleta mada angekuwa mwanaume!
 
Last edited by a moderator:
hahaha Mbu bana usje ukasababisha shem akaninyima mwaliko wa besdei yake mpya.

bek to ze topik: Mimi bado nina wasiwasi na hii kesi, kinachonifanya nisiropokwe ni uamuzi wa mleta mada kwamba hataki ushauri anataka maelekezo tu ya uhusiano mpya.

.....hahahaha....besdei yake mpya ee? Na kweli bana, kwetu tunashereheka kwa kalenda zote, Gregorian, Islamic, Chinese, Coptic, Hindu Solar, Ethiopic, .....almuradi zote 19 zinazotambulika 'hepi ni besdei tu yuu'....

....mleta mada anajua maji yapatikana kisimani, anachouliza ni njia tu, iwe ni shortcut, au mzunguko.....au salama. Haya maswali mengine maji anayafanyia nini yatuhusu nini? Akiyanywa yeye, akiyakoga yeye, hata kama ni kwa 'bustani' tu...maji ni uhai bana... ;)
 
Umeona eeh!...halafu mahusiano mapya yakishindikana inakuwa tabu nyingine.

....kaka BAK bana, atleast she's daring to move on than dwelling in her miseries. Watu wengi wapo pessimistic wakati huo huo hukemea kwa nguvu zote manyanyaso ya kijinsia.

There's no harm kujitambua 'thamani yake' na kujiridhisha mahusiano alonayo hayakidhi matakwa, malengo na yote aliyoyakusudia....
Kajikubalisha, ameamua. Ya huko mbele ya safari ni matokeo tu kaka....".....a glimpse of light at the end of the tunnel!'
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
Hi people asanteni kwa kuchangia, nawaombeni radhi kwa mnaonishauri nirudi, that chapter is closed na I will never go back to that one sababu mpaka nimefikia maamuzi hayo nilishafanya mengi mno ambayo haimake sense kuyaandika hapa, so nimeamua, wazazi wa pande zote mbili wameridhia na kujihakikishia kuwa kuendelea kuwa huko kuna mtu anaweza kuja kufa, so na wao wameshauri the same. asiyetaka ni yeye tu. tuachane na hayo lakini nimegundua kuna watu wanapreffer uongo (cheating to yourself and your other half) kwenye mambo ya mahusiano (which I dont believe in honestly, yes Im one of those few people). If this, the same heart that had decided to love him very much na nikaufuata leo hii umemreject big time sababu ya demage aliyosababisha, kama nilikuwa nafurahisha moyo wangu kuwa nae kwa nini leo niutese kuwa nae wakati moyo hautaki. I will go with the same spirit.
Asanteni kwa ushauri, na kuhusu eti kuwa na mahusiano tusiwe na mawazo ya sex tu, there are lot of things in there, the process ni ndefu mpaka kufikia huko coz you start with knowing someone, kushirikishana kwenye mambo ya maisha, kushauriana etc hayo mambo mengine baadae sana(for few of us) until you are very confortable with a person ndio hayo ya kumuintroduce kwa watoto uone reaction then you decide, hiyo process tu can take years. Nilichokuwa nataka kujua je endapo itagundulika Im so close to someone of oposite sex na ofcourse sitapenda kudanganya eti ohh huyu rafiki tu, maana intention yetu itakuwa clear from the beggining (For security purpose! LOL) itakuwa nimekosea?? kisheria hasa. hilo hasa ndio nilitaka kujua.
 
dada fata moyo wako unakuambia nini, hata kama jamaa hayupo tayari kukuacha, ni wewe unaejua kero zake,

watu wanataka kujua chanzo cha break up, ili iweje sasa, mleta mada hataki kuendelea kuishi na huyo mtu, moyo ukikataa umekataa,
 
Back
Top Bottom