Sensa: Ponda, wenzake wahesabiwa

Hongera Sheikh Ponda... Sasa Karibu Ubungo Unaweza kugombea UBUNGE...
 

Kwani Sheikh Ponda hapigi kura? Kama anapiga kura data zake zipo katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa hiyo zinajulikana asiwe na mashaka ya kuhesabiwa kesha hesabiwa siku nyingi. Na kama hapigi kura basi si raia maana hana cheti cha kuzaliwa au hana mpango wa kutafuta cheti hicho atarudishwa sijui Congo, Burundi au Rwanda? Naona labda anapendelea Iran basi atapeleka huko kama watampokea kuombea mitambo ya nuclear!
 
hadithi ya sensa hii kali, eti mtu amekuja kuchukuliwa na askari 5 ndani ya cruiser, akapelekwa kituo cha polisi akahojiwa kwa nini hujajiandikisha akasema sijafikiwa na watu wa sensa, wakamwambia wako pale kwenye kata ngoja tukupeleke tukuone akafika akajiandikisha kuhofia wale askari akaachiwa, RASILIMALI ZA NCHI HII!
 
Habari ya kuzushi,uongo na kikanjanja.Shekhe Ponda hajahesabiwa! Kama huyo mwandishi katumwa au kiherehere tu basi alete ushahidi wa wazi hapa.Acheni unafiki tzdaima.
 
Hizo ni propoganda!ukweli ni kwamba zoezi la sensa limekua hovyo.viongozi ngazi za chini hawakushirikishwa

Pamoja na hayo PONDA KAHESABIWA.

Shida yenu hamjui yanayojiri nyuma ya pazia, hata kwenye vitambulisho vya Taifa alisumbua yule, lkn baadae alikwenda kituoni mwenyewe kuandikishwa kwenye daftari. Ukiona umefikia kuongozwa na yule mnyarwanda ujue umefilisika kichwani.

Safari hii hakupata wa kumuunga mkono mtaani kwake, wenzake walihesabiwa bila shwishwi. Yeye akajificha lkn maagizo alimuachia mama chanja kiujanja. Aliona noma
 
Habari ya kuzushi,uongo na kikanjanja.Shekhe Ponda hajahesabiwa! Kama huyo mwandishi katumwa au kiherehere tu basi alete ushahidi wa wazi hapa.Acheni unafiki tzdaima.

Hakuna ushahidi kwa kukuridhisha wewe. Dodoso limeandikwa TUNZA SIRI

Wewe leta ushahidi kuwa hajahesabiwa. Tumia akili zako, Ponda anapotosha
 
Hongera Sheikh Ponda... Sasa Karibu Ubungo Unaweza kugombea UBUNGE...

Wenzake wanamgwaya hawezi kupata kura hata moja.

Wakati wa National ID, maeneo yote ya Ubungo Islamic wakazi waligoma kuorodheshwa kwenye daftari la wakazi, baadae yeye akawa wa kwanza kujisajili asiwaambie wenzake (kawauza). Safari hii ya sensa wamemshit, kaona noma basi tu hana pa kuficha uso.
 
Asante kwa kutupa habari. Huyu Ponda amekuwa akipotosha uma na cha kushangaza serikali ya Jk wanamtizama tu
 
Propaganda za magamba zinazo pendwa na cdm ndo hizi. Tehe tehe liwalo na liwe tunajua kua sensa imedoda imekula kwao
 

Acha uvivu wa kufikiri,mbona dai la waisilamu lipo wazi ...usitake kuudanganya uma kwa maneno yako ya kusadikika eti "wanataka maboresho ndani ya maswali ya sensa" ...Inamaana kujua huyu ni Mtanzania muislamu na huyu ni Mtanzania Mkristo ama Mpagani hapo kuna tija!!!
 
Ni mnafiki tu kunasababu gani kusema Ponda kahesabiwa-ili kuwarubuni waislam wahesabiwe? amekwama na Allah amekwisha malipa jaza yake. Anadaganya laivu kuwa nchi zenye kipengle vcha dini zimepata matatizo -mbona hata hataki kuzitaja? Mwongo Mkubwa. UK, USA, Germany, Sweden, Kenya, Uganda, France, kote huko watu wanahesabiwa si tu kwa dini bali pia dhehebu kuna vita huko? kama yeye mbumbumbu wa masuala ya dunia aseme hivyo. KWani waislam na wakristo hatjuani mitaani tunakokaa? Mbona hatujapigana? Ikitokea kupigana uje sababu ni ujinga wa serikali yenyewe na wanaowasukumu nyuma. Wakati huu si wakati tena wa kudhani kuwa kuna baadhi ya watu ndo wanataarifa kama enzi za Nyerere hata akaonekana mwenye maono-bahat mbaya mtakwimu Chuwa anaamini hivyo mpaka leo kuwa nyerere aliona maono ndo maana akaondoa kipengele cha dini-ni ujinga wa kutupwa. Mungu awape nguvu waislam wote katika hili.
Wakristo nao vipi? KWani hawaoni kuwa kwa kukaa kimya na kufurahia hili hakuwaweki pembeni ikiwa nchi itaingia kwenye machafuko? Kama kweli wanataka amani ya upogo tuliyonayo basi waikemee serikali iliyomkomni mwaodhidi ya hali hii-Huu ni mtumbwi mmoja ukizama wajue nao wamezama.
Ingekuwa kweli Ponda kahesabiwa nyumbani kwake magazeti na television wangealikwa kushuhudia mke wake akitoa taarifa-mama Mrisho muogope Mungu na achana na kufanya Propaganda za kitoto
 
He Mkomamanga-kwani wangapi walio Wa TZ hawapigi kura na wala hawajajiandikisha kwenye daftrai hilo? Suala la kupiga kura kwa m-tz ni la umuhimu kuliko hata la sensa kwani linaangalia moja kwa moja maslahi ya mwanachi kwa miaka 5 ikiwa amechagua bomu ajue atakaa nalo mpaka miaka 5.
Sensa isiyouliza hata hali ya huduma za jamii sehemu za wananchi ni sensa ya maslahi yapi? Nilitegemea sensa iulize upatikanaji wa maji, afya, shule, usafi wa mazingira, ili serikali ijue kuwa sehemu fulani mahali fulani hapa Tz kuna tatizo la maji, hospitali, shule na uharibifu wa mazingira-kuliko kuuliza sensa mfuto -maskai, manzese, kibangu-matatizo hayafanani badala yake wanakaa kuwindana na waislamu wanaodai haki yao. bahat mbaya zaidi kabisa kuna wa TZ wanaoshangilia kudharirihswa kwa waislamu wajue iko watakuwa wanadharirishwa wao.
 
Hivi katika sakata hili Kituo cha Sheria na haki za Binadamu hwalioni au ndo walewale ikiwa linawahusu waislam si suala la kusghulikiwa? Wameonana na wavamizi wa viwanja madale na kutaka serikali itoe misaada ya kibinadamu kwa waharifu, je hili la waisla vipi? Au ndo UDINI live?

Ingekuwa suala hili linahusu kibaka (aliyevunja sheria) angetetewa asiuuawe lkn vipi wanadada wa kiislamu wanaonyanyaswa kwa kutohesabiwa wakiwa na sababu maalumu na za msingi Kituo kimekaa kimya maana yake nini? TUAMINI kuwa la wasilamu siyo ISSUE?

Hebu acheni udini wa kupindukia-tendeni kwa misingi ya haki za binadamu blia kujali imani za watu ikiwa mnataka kujenga imani juu ya wananchi
 
wewe karani mwongo-mbona gazeti ma bosi wako Mrisho anadai wakati wa zoezi yeye Ponada alikuwa mskiti wa Mtambani? Tushike la nani -lako au bosi wako aliyeongea na vyombo vya habari? nawe acha unafiki na undumilakuwili-toa taarifa zilizosahihi
 

hivi kwa nini polisi wasimkamate shehe Ponda na hao wamiliki wa redio Imam kwa kuzuia sensa badala yake wanapiga marufuku mikutano ya CHADEMA eti inaathiri sensa?kati ya Ponda na M4C nani anayeleta madhara kwa sensa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…