Sensa ni ufisadi tuukatae. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sensa ni ufisadi tuukatae.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mohamedi Mtoi, Apr 28, 2012.

 1. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #1
  Apr 28, 2012
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Zoezi la sensa linalo takiwa kuanza hivi karibu lina harufu ya kifisadi ya kupoteza kodi za watanzania. Naweza kuthubutu kusema hivyo baada ya tafakuri ya kina hasa nikirejea kwenye ukuta wa twitter wa Dr Slaa ambapo nimekutana na swali lake lisemalo "kwanini sensa isingejumuishwa
  kwenye zoezi la
  vitambulisho?" kwa mujibu wa Dr Slaa takwimu za fedha zinaonyesha kuwa Sensa itagharimu bilioni 119, wakati vitambulisho vya taifa vitaghalimu bilioni 230 za kitanzania.

  Ukiangalia kwa makini hapo kuna upotevu wa fedha kutokana na kuwa na mipango mibovu. Zoezi la vitambulisho vya taifa lingeweza kutumika kukusanya takwimu za sensa na kuokoa shilingi 119 bilioni. Kiasi hicho kingeweza kutumika kwenye matumizi mengine ya muhimu kama ujenzi wa nyumba za walimu zaidi ya 1000 au hata kujenga maabara ambazo si chini ya 300 na vifaa vyake kwenye shule zetu za kata ambazo hazina maabara wala misingi ya ujenzi kwa majengo hayo.

  Tuna tatizo la kupanga vipau mbele vyetu na matokeo yake ni matumizi mabaya ya rasilimali fedha. Tunahitaji kulipigia kelele hili, tutimize wajibu wetu inawezekana.
   
 2. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  mwisho tutasema watumie daftari la kudumu la wapiga kura. Ni kupigia kelele sensitization iwe kubwa tu. Zoezi la vitambulisho litachukua miaka na miezi mingi sana,hatuwezi kufanya sensa namna hiyo,hili zoezi linaweza kuwa ni zaidi hata ya nhif kwa kuchelewa. Wameanza na wafanyakazi sasa ni leo mpaka wakawafikie kina fid q? Na wavuvi wanaoishi maziwani? Sensa inahitajika kufanyika haraka ili mipango ianze kupangwa kutokana na idadi ya watu. Tukifanya zoezi la vitambulisho liwe la haraka wataharibu kazi aafu waanze kujitetea kwamba waliharakishwa. Hatutaki wapate pa kuchomokea wakiharibu kodi zetu. Huwa sipendi mambo mengi yanayofanywa na serikali yasiyojali manufaa ya wengi, hili hapana!
   
 3. safariwafungo

  safariwafungo Senior Member

  #3
  Apr 28, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 136
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Katika mambo ambayo kwa imani yangu ya Kiislamu tumeambiwa tujichunge navyo ni kiungo kinachoninginia baina ya mapaja mawili pamoja na kiungo kilichopo baina ya taya [ulimi], ni vyema kufanya tafakuru sana kabla ya kuvitumia viungo hivyo, nadhani sasa ni wakati muafaka kuwa makini sana na kuacha kuzungumza mambo ambayo weledi wake kwetu sisi ni mdogo otherwise kama ni kwa lengo la kupata public opinion na kuona ni kwa namna gani jamii inalighamua zoezi lililopo mbele yao,

  kimsingi mimi najikita katika hoja ya msingi kuunganisha zoezi la sensa pamoja na zoezi la vitambulisho vya kitaifa, kiroho safi kabisa nadhani tutakuwa tunapotoka na hari kama ndiyo hivi ni dhahiri inavyoonyesha ni namna gani hivi vitu viwili ambavyo havifahamiki vizuri kwa jamii na hili linaweza kuwa lina sababishwa mosi na ufinyu wa PR activities wa taasisi husika ama kwa sisi kutopitia mambo haya kwa undani zaidi

  Zoezi la vitambulisho ni zoezi endelevu ambalo litachukua muda kiasi na halifanyiki at the spot for the whole country lakini sensa inafanyika mara moja kwa nchi nzima hasa ni kunghamua ditribution ya wakaazi nchi nzima pamoja na demographic factors anuai ambazo zitaliwezesha kwanza taifa kuweza kuyakabili majanga, pili kuweka mikakati anuai kwa ustawi wa taifa, zipo sababu anuai lakini sanjari na hilo vitambulisho vya kitaifa kama inavyo jieleza is a personal ID ya mtanzania ambayo ofcourse itakuwa ina biometric data pamoja na nyinginezo za muhusika na hii itaisaidi sana nchi kuweza kupamabana na uhalifu [if data llike fingure prints, DNA ztakuwepo so forensic investigation will be easy and definitely crime control will be easy and hence safe life which will boost economy if properly managed], ukusanyaji wa kodi na mapato na kama itakuwa integrated na system nyingine hakika impact yake itakuwa kubwa kwa uchumi wa nchi. Kimsingi theoreticaly is very correct to sandwich the two together lakini practically has no physical implication mimi nadhani haya mambo ya kitaalamu tuwaachie watalaamu.

  [main reasons why not integrated together is derived from the definition of the two as well as if we need to have a practical implication we real need to respect proffesional works, maendeleo ni gharama na hizi ndo gharama zeenyewe cha msingi ni je hayo matokeo ya mazoezi haya makubwa mawili utayatumiaje kuleta manufaa kwa umma wa tanzania?]
   
Loading...