Unajua hata MAKABURU wa AFRIKA KUSINI (AK) walikuwa na sheria ambazo walikuwa wanasema akina MANDELA wanatabia ya kutozitii, kama wewe usemavyo. Sheria zisizo na usawa siyo sheria (MANDELA alisema, kipindi akipigania uhuru, kuwa HAAMINI kama AK kuna sheria). MIMI nae naamini kama MANDELA, kwamba, siamini kama TANZANIA kuna sheria: sheria gani ambazo zinatumika kwa maskini tu- sensa moja, kwa nini sasa MPs, RCs, DCs, Ministers nk walipwe mamilioni kuhamasisha sensa, alafu, hohehahe wenyeviti wa VITONGOJI wafanye kazi hiyo2 lakini, BILA MALIPO (Inamaana hawa akina NCHIMBI according to GEORGE ORWELL: they are "... more equal than others..." in THE ANIMAL FARM).
ANYWAY tuachane na hilo, maana halinisumbui kwa sababu hata huyo DR NCHIMBI mwenyewe na watu wa aina yake hawatii sheria. (1) HII ni kwa sababu matamshi aliyoyatoa yalikuwa ni HUKUMU. KUTOA hukumu ni jukumu la mahakama (tazama IBARA 107A, 107B KATIBA JMT), na yeye si JAJI wala hakimu, si hata wa mahakama ya MWANZO tu. KWA hiyo kavunja sheria, hatii sheria, kwa nini unataka yeye watu wamtii. (2) Kaingilia mamlaka ya kisheria ya NBS, DR ALIBINA CHUWA Mwanatakwimu huyu anajua nikisemacho. RC NCHIMBI hatambuliwi na sheria ya TAKWIMU, kama unabisha niambie ni kifungu gani cha sheria kinachompa mamlaka ya kuchukulia watu 'hatua kali za kisheria' kama watakwamisha sensa.