Sensa: Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Vitisho kwa Watendaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sensa: Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Vitisho kwa Watendaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwita Maranya, Aug 21, 2012.

 1. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mkuu wa mkoa wa Dodoma ametishia kuwachukulia hatua kali viongozi/watendaji wa kata na vijiji ''watakaohujumu'' zoezi la sensa mkoani humo kwa kisingizio cha kukosa/kutolipwa posho.

  Source: ITV habari saa 2 usiku.

  MY TAKE:
  Kama viongozi wa juu wa serikali wanalipana posho kubwa kubwa na zimetengwa fedha za kutosha (mabilioni ya shilingi) katika bajeti ya serikali.
  Hata wabunge walilipwa shilingi milioni moja kila mbunge kwa ajili ya uhamasishaji majimboni mwao, serikali inatoa wapi kigugumizi cha kuwalipa watendaji wa ngazi za vijiji na kata?
   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Huyu mama tangu kaingia Dodoma ni kuendesha mji kama NGO yake...ndio huyu alipiga stop mikutano ya siasa wakati wa vikao vya bunge kwa kisingizio kuwa askari wanakuwa busy kulinda viongozi. Lakini ukweli aliogopa baada ya kufanya mkutano mkubwa wa kumkaribisha dogo Janja na Madam Pareso. Kifupi huyu mama ana kaubabe fulani kakizamani.
   
 3. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nasikia wanamuita Dkt. Rehema Nchimbi, sijui kama ni udokta wa mezani kama JK ama wa mtandaoni kama Mahanga ama ni udokta wa ukweli.
  Kama ana udokta wa ukweli basi elimu aliyopata haijamkomboa kabisa.
   
 4. M

  Malata Junior JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,780
  Likes Received: 1,207
  Trophy Points: 280
  mimi ni mwenyekiti wa mtaa,bila posho sifanyi kazi yoyote nitabaki nyumbani kuhesabiwa mimi na familia yangu.posho wale wao kazi tufanye sisi!
   
 5. tatanyengo

  tatanyengo JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2012
  Joined: Mar 30, 2011
  Messages: 1,140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tangu tupate uhuru, sensa ya mwaka huu ni KIBOKO!
   
 6. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Swali la kujiuliza ni je hao watendaji wa vijiji waliomba hizo nafasi kwa ajili ya posho ua kuwatumikia wananchi ili wajipatie maendeleo yao.

  Sensa inafanywa kwa maslahi ya taifa, kupitia sensa tutapata idadi kamili ya watu kwa kila mtaa, kijiji, wilaya, mkoa na hatimaye Taifa ili kuwezeshaji uaandaji wa mipango ya maendeleo kwa kila ngazi. Sensa ni kitu cha muhimu sana duniani kote hakuna nchi inajiendesha bila kuwa na takwimu sahihi za watu wake. Ili halina mjadala kwa msomi na asiyekuwa kuwa msomi.


  Pili mimi nadhani kauli ya Mkuu wa Mkoa ni sahihi hasa kwa kuzingatia kuwa Wtz tumekuwa na hulka za ajabu za kutokutii sheria na taratibu zinazotuongoza. Kwa mazingira hayo wewe ulitaka Mkuu wa Mkoa awabembeleze au awahamasishe wasiende kusimamia sensa kwa kuwa hakuna fedha za kuwalipa?. Hizo ni sera na mitazamo ya kimaskini zaidi, na wala siyo za mtu aliye elimika. Ambaye hawezi kuifanya hiyo kazi kama kweli ni mzalendo kwa nini asitangaze kuachia ngazi badala yake anashinikiza kulipwa posho?

  Kwa taarifa tu Dkt. Rehema Nchimbi ni msomi na alikuwa mwalimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya Newala na baadaye Mkuu wa Mkoa Dodoma, PhD yake amefanya South Africa.

  Tuacheni ushabiki usikuwa na maana katika masuala ya msingi kama la sensa, sensa haina chama, itikadi, kabila wala dini.
   
 7. M

  MABAGHEE JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 687
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Huyo Dr tulikuwa tunamwita mama akiwa Mwl pale UDSM. Hakuwa na harufu ya ufisadi yeye kwake uzalendo mbele, Wakati mwingine kiongozi utachukiwa tu hata ukisema mazuri. Yeyote alosoma idara ya history UDSM atakueleza kuhusu uzalendo na busara zake.
   
 8. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #8
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Susieni basi, mnangoja nini?
   
 9. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  sensa imefeli hata kabla ya siku ya kuanza kuhesabiwa haijafika! waislam kiboko.
   
 10. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kama sensa haina mapungufu kwa nini serikali ina haha sana? Tujiulize maswali mengi sana Je, sensa ndio tunaanza tangu tupate uhuru? au sensa zilizopita zilikuwa na vurungu kama hizi? Jk, na viongozi wako wa msimu munajua nini mlichowakosea wananchi hivyo "kumbukeni mlikoanguka mkatubu"
   
 11. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Njoka Ereguu umejieleza vizuri sana. Lakini swali la msingi ni kwanini watendaji wa mitaa, vijiji na kata wasilipwe posho wakati bajeti ipo?
  Kama ''mama mzalendo'' anatoa vitisho badala ya kuhakikisha wamepata na stahili zao, hapo kuna dalili za ufisadi na uzalendo umemtoka siku nyingi tangu aache kufundisha na kuhamia kwenye siasa.
  Uzalendo ni pamoja na kutambua mahitaji/maslahi ya wengine na kuyalinda/kuyasimamia.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Mkulima wa Kuku

  Mkulima wa Kuku JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,259
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Uzalendo ni pamoja na kusimamia haki ikiwa ni pamoja na mgawanyo wa haki kwa kila anayestahili. Hapa naona tatizo la wakubwa wachache kujinufaisha na kuwataka wengine watumike huku wao ndiyo wanaofaidi. Serikali isipolianfalia hili, basi sensa itakuwa ni matakataka
   
 13. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Huyu mama anawabeba waliombeba,na kwa taarifa yake moto wa makarani kususia sensa bila kupata malipo stahili,huu ni moto wa kitaifa kama fedha imeshaliwa tuhairishe sensa tu mpaka 2016,mtakapokuwa mmeshakabidhi nchi kwa wananchi.
   
 14. Zanta

  Zanta JF-Expert Member

  #14
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 2,017
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Serikali imechemka sana kuweka mseto kwenye ukarani wa sensa, maana watu hawana kazi kwa hiyo bila mshiko kazi haifanyiki. Wangekua walimu tu aaah wao hata wakilipwa mwakani poa tu. Sina imani kabisa na Data zitakazotokana na sensa hii. Watu wamejichokea na watazipika tu hizi data thena hao kufuata mshiko. Kama Mtu anasoma Masters au PhD na anapika data itakua hawa wa sensa?
   
 15. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #15
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hakuna kipindi ambacho nchi yetu imekuwa ya kibabaishaji kama sasa,watanzania tupo baharini bado kuzama tu.watu wameshindwa kazi kilichobakia kwao ni kuwatishia wakubwa wenzao kama watoto wao,lakini mwaka huu watawafokea hata mbuzi na kwa bahati mbaya hawatawasikiliza maana wamepoteza maana kama mtu mzima atembeaye masaburi yakingali wazi.
   
 16. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #16
  Aug 22, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wewe ndo unaweka ushabiki.
  Sensa imetengewa fungu, why watu wafanyishwe kazi halafu wasilipwe kwa wakati?
  Unataka wafanye kazi kwa mkopo, kisha waje wadai malimbikizo kwa miaka zaidi ya 30 km wazee wa East Africa?
  Makarani kazeni, msimamo ule ule, no posho, no sensa.
   
 17. u

  usungilo JF-Expert Member

  #17
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 501
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  data nyingi sana zitapikwa sensa ya mwaka huu. Kuna uwezekano mkubwa wa mipango ya kurudia zoezi hili kama litakavyorudiwa la vitambulisho na katiba mpya. Hawa watu waliowaokota mitaani watatutia hasara kubwa sana ambayo ni kurudishana nyuma kimaendeleo.
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Aug 22, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Huu ndio ukweli wenyewe, kama serikali isiposhtuka haraka kwa muda huu mfupi uliobakia na kuwalipa makarani pamoja na watendaji wa vijiji, kata na mitaa ukweli ni kwamba zoezi la sensa halitafanikiwa kabisa, kitakachotokea ni upikwaji wa takwimu ili kuficha aibu.

  Kwa jinsi viongozi wa serikali hii walivyo wa ajabu wanashindwa kuwalipa makarani wa sensa stahiki zao halafu wanategemea kazi nzuri ya sensa. Bajeti ipo kwahiyo fedha zipo lakini wanataka kuwadhulumu makarani ili wakajijazie kwenye accounts zao.

  Kama serikali ingewatumia walimu pekee bila shaka ingeweza kufanikiwa kuwadhulumu kwani wao wamezoea kuidai malimbikizo na hata wamezoea kuisamehe. Lakini kwa jeuri yao ya kuwaengua walimu baada ya kuendesha mgomo sasa ndio serikali imejikuta imeingia choo cha kike.
   
 19. j

  juu kwa juu JF-Expert Member

  #19
  Aug 22, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  dr ni wa ukweli alikuwj anafundisha udsm. Chezea udsm lecture wewe!
   
 20. Alexism

  Alexism JF-Expert Member

  #20
  Aug 22, 2012
  Joined: Aug 14, 2011
  Messages: 2,443
  Likes Received: 1,015
  Trophy Points: 280
  mkuu naona umetazama tu unalolijua wewe tu, lakini kumbuka watendaji hao hawakuomba kufanya kazi kama hizo so posho kwao ni halali.Jaribu ata kuangalia sheria za kazi zinasemaje siyo unakuja na hisia tu.
   
Loading...