Sensa: Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Vitisho kwa Watendaji

data nyingi sana zitapikwa sensa ya mwaka huu. Kuna uwezekano mkubwa wa mipango ya kurudia zoezi hili kama litakavyorudiwa la vitambulisho na katiba mpya. Hawa watu waliowaokota mitaani watatutia hasara kubwa sana ambayo ni kurudishana nyuma kimaendeleo.

sababu sio hiyo tu sensa haitakuwa na data kwa sababu kundi kubwa la watanzania ambao ni waislamu hawatashiriki katika zoezi hilo, mshikamano uliooneshwa katika hili unatia hamasa, enzi za kutosikilizwa waislamu , kutukanwa viongozi wake na kufanywa raia wa daraja la pili zinpotea , huu ni mwanzo mzuri, heshima itapatikana, tukishakuwa na respect sawa haki itatendeka
 
" ... Pili mimi nadhani kauli ya Mkuu wa Mkoa ni sahihi hasa kwa kuzingatia kuwa Wtz tumekuwa na hulka za ajabu za kutokutii sheria na taratibu zinazotuongoza. Kwa mazingira hayo wewe ulitaka Mkuu wa Mkoa awabembeleze au awahamasishe wasiende kusimamia sensa kwa kuwa hakuna fedha za kuwalipa?. Hizo ni sera na mitazamo ya kimaskini zaidi, na wala siyo za mtu aliye elimika. Ambaye hawezi kuifanya hiyo kazi kama kweli ni mzalendo kwa nini asitangaze kuachia ngazi badala yake anashinikiza kulipwa posho?

Unajua hata MAKABURU wa AFRIKA KUSINI (AK) walikuwa na sheria ambazo walikuwa wanasema akina MANDELA wanatabia ya kutozitii, kama wewe usemavyo. Sheria zisizo na usawa siyo sheria (MANDELA alisema, kipindi akipigania uhuru, kuwa HAAMINI kama AK kuna sheria). MIMI nae naamini kama MANDELA, kwamba, siamini kama TANZANIA kuna sheria: sheria gani ambazo zinatumika kwa maskini tu- sensa moja, kwa nini sasa MPs, RCs, DCs, Ministers nk walipwe mamilioni kuhamasisha sensa, alafu, hohehahe wenyeviti wa VITONGOJI wafanye kazi hiyo2 lakini, BILA MALIPO (Inamaana hawa akina NCHIMBI according to GEORGE ORWELL: they are "... more equal than others..." in THE ANIMAL FARM).

ANYWAY tuachane na hilo, maana halinisumbui kwa sababu hata huyo DR NCHIMBI mwenyewe na watu wa aina yake hawatii sheria. (1) HII ni kwa sababu matamshi aliyoyatoa yalikuwa ni HUKUMU. KUTOA hukumu ni jukumu la mahakama (tazama IBARA 107A, 107B KATIBA JMT), na yeye si JAJI wala hakimu, si hata wa mahakama ya MWANZO tu. KWA hiyo kavunja sheria, hatii sheria, kwa nini unataka yeye watu wamtii. (2) Kaingilia mamlaka ya kisheria ya NBS, DR ALIBINA CHUWA Mwanatakwimu huyu anajua nikisemacho. RC NCHIMBI hatambuliwi na sheria ya TAKWIMU, kama unabisha niambie ni kifungu gani cha sheria kinachompa mamlaka ya kuchukulia watu 'hatua kali za kisheria' kama watakwamisha sensa.
 
Hesabu itakayopatikana, ndiyo idadi ya watanganyika. haijalishi umehesabiwa au la.
 
Na kwa nini hawataki kuwalipa wakati ni haki yao?......wao wanalipana maposho makubwa afu hao hicho kidogo wanataka kuwadhulumu.......Wawalipe afu waache kuwatisha!
 
huu mchezo wa posho mwanzilishi ni ccm yenyewe, hivyo wanavyogeukwa wasishangae. Na bado tutaona na kusikia mengi.
 
Unajua hata MAKABURU wa AFRIKA KUSINI (AK) walikuwa na sheria ambazo walikuwa wanasema akina MANDELA wanatabia ya kutozitii, kama wewe usemavyo. Sheria zisizo na usawa siyo sheria (MANDELA alisema, kipindi akipigania uhuru, kuwa HAAMINI kama AK kuna sheria). MIMI nae naamini kama MANDELA, kwamba, siamini kama TANZANIA kuna sheria: sheria gani ambazo zinatumika kwa maskini tu- sensa moja, kwa nini sasa MPs, RCs, DCs, Ministers nk walipwe mamilioni kuhamasisha sensa, alafu, hohehahe wenyeviti wa VITONGOJI wafanye kazi hiyo2 lakini, BILA MALIPO (Inamaana hawa akina NCHIMBI according to GEORGE ORWELL: they are "... more equal than others..." in THE ANIMAL FARM).

ANYWAY tuachane na hilo, maana halinisumbui kwa sababu hata huyo DR NCHIMBI mwenyewe na watu wa aina yake hawatii sheria. (1) HII ni kwa sababu matamshi aliyoyatoa yalikuwa ni HUKUMU. KUTOA hukumu ni jukumu la mahakama (tazama IBARA 107A, 107B KATIBA JMT), na yeye si JAJI wala hakimu, si hata wa mahakama ya MWANZO tu. KWA hiyo kavunja sheria, hatii sheria, kwa nini unataka yeye watu wamtii. (2) Kaingilia mamlaka ya kisheria ya NBS, DR ALIBINA CHUWA Mwanatakwimu huyu anajua nikisemacho. RC NCHIMBI hatambuliwi na sheria ya TAKWIMU, kama unabisha niambie ni kifungu gani cha sheria kinachompa mamlaka ya kuchukulia watu 'hatua kali za kisheria' kama watakwamisha sensa.
Mhe. Nyamkangíl, siyo lengo langu kupingana na maoni yako maana kila mtu anayonamna ya kuangalia na kuchambua mambo. Suala la msingi kwangu lilikuwa je ni kweli Tanzania tumefikia mahali pa kupinga hata sensa kwamba tukae tu bila kuhesabiwa ili tuwe takwimu sahihi za wananchi wa Tanzania kwa nia njema tu ya kuwezesha mipango ya maendeleo ya nchi. Unaweza kusema mipango gani, lakini mimi kama mjasiriamali nahitaji sana kuwa na takwimu sahihi za watanzania ili niweze kujipanga katika kujitafutia maendeleo mimi binafsi na familia yangu au jamii inayonizunguka. Tusiweke suala la posho mbele maana hicho siyo kipaumbele, kwa tukubaliane kimsingi kuwa sensa ni muhimu.

Kama hilo haukubali sitashangaa watu wanaweza kuja na kusema katika hata kufanya uchaguzi pasiwepo na daftari la wapinga kura wala kijiandikisha kupiga kura kwa kwa haina maana kuwa na takwimu hizo.

Ni vizuri tukaelewana vizuri binafsi si shabikii posho, lakini hoja yangu kubwa ni kuwa sensa ni muhimu. Nani kala ngapi hilo lina namna yake ya kushughulikiwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom