Sensa 2012: Yanayojiri

naungana na wewe kaka, baada ya kupata hii habari nimewasiliana na jamaa hapa manispaa wamesema ni kweli TOOLS DOWN, vifaa hakuna mkoani wameagiza dar
 
Kwa nini dodoma vifaa viishe? isije ikawa hawa magamba wamepanga waharibu sensa dom makusudi ili idadi ya watu iwe feki wachakachue vizuri daftari la kudumu la wapiga kura? WAPI GREAT THINKERS
 
kaka usichukulie rahisi hivyo, fikiria umehamasishwa na balozi wa mtaa kuwa kesho usiende shamba utapitiwa kuhesbiwa ,halafu jamaa wanakuja wanakwambia hawana karatasi, ukizingatia huu ni msimu wa kutayarisha mashamba (kubelega): pia wakazi wengine ni wafanyabiashara ya zabibu kusafirisha, unadhani hawa watasubiri vifaa?
 
Kila Mkazi wa Dodoma aliyesahauliwa leo Jumatano atahesabiwa, hilo shaka ondoa, na ni vifaa gani unavyovitaja hakuna? karatasi za dododso au pencil, mavazi si hoja na hata huko Matumbulu watu ni waelewa sana, inachotakiwa ww acha maagizo aliyebaki nyumbani awataje waliolala hapo tarehe 25 kuamkia 26/06/2012. kama kuna ka mgomo kwa waandikishaji hatujakasikia wakazi wote wanahesabiwa chini ya M<abalozi na Wenyeviti wa Mitaa, kwa wale waliosahauliwa wanapitiwa tena
 

tutegemee madudu ya ukosefu wa vifaaa kujitokeza uchaguzi mkuu kwakuwa michakato ya zabuni ......inarudi wizi uliofanywa na makampuni yaliyopewa kazi za sensa ....
Tusije kukosa hadi karatasi za kupiga kura ..kama uchaguzi wa serikali za mitaa ulivyovurugwa ......
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…