Ahead
JF-Expert Member
- Jan 11, 2013
- 2,407
- 2,729
Ndio,nakuandikia waziri wa nishati January Makamba.
Sina kawaida ya kuandika mada humu ila hili limenigusa,nimeona picha zikisambaa mtandaoni ukiwa majuu(ukila bata aka marupurupu ya uwaziri).
Naomba kukutaarifu huku kwetu Sengerema mwanza ni siku ya tatu hatuna umeme hali iliyopelekea tukose huduma ya maji pia kwa siku tatu hapo sijafanya tathmini ni athari gani za kiuchumi zimepatikana kwa kukosa umeme.
Sijui kama umerudi nchini au bado ila ni vema utambue nafasi yako unawakilisha watanzania wote kutatua changamoto za sekta ya nishati Tanzania nzima hayo mengine ni ziada.Chonde msiturudishe Tanzania kwenye ujima,siku tatu hakuna umeme,siku tatu aah hapana!
Ombi;Mods msiutoe huu uzi kwasababu sio uzushi, waziri na nyie tumieni vyombo vyenu mjue ukweli wa taarifa hii muone namna ya kutatua.