Sasa ki ungwana kwa kuwa yeye katoa hoja ya kuwa hakuna mtu naye sema makosa ya Ben wazi basi swala ni wanaotaka afikishwe mahakamani wamkumbushe tu makosa yake,thats it! Unajua alichoongea kama mtu hajui makosa ya Ben ni point kubwa sana na analamba hizo point kwa watu milioni nyingi Tz ,sasa atokee mtu ajibu na yeye kwa media .
Naomba kutofautiana na wewe nyuzi 180.
Dai analotoa Mbunge kwamba Tunao dai MH Mkapa afikishwe Mahakamani tumkumbushe makaosa ya mkapa ni suala linalo mdidimiza, kumdharirisha na kumbomoa MH Sendeka.
MH Sendeka asile H/W yake hapa ili afanyiwe na kupata alama chee.
Huyu ni mjumbe katika Baraza la kutunga sheria.
Huyu ni mtu wa watu.
Huyu ni muwakilishi wa matatizo kero na unyonge wote walio nao wananchi wa Tanzania bila kujali jimbo lake au nani alimteua.
Sidhani kama ni haki (sheria) kwa mtunga sheria kuja hapa jamvini na hoja hafifu namna hiyo ya kudai kwamba hajui kulikoni.
MH Sendeka Rejea maelezo ya Kina ya Mbunge wa Moshi vijijini.
Hata kama ulikuwa umelala fofo pale Bungeni au ulikuwa inajivinjari mitaani wakati wenzio wako Bungeni au ulikuwa na udhuru wowote ule wa maana, ulitakiwa kujua kiacho msibu MH Mkapa badala na kuja na hoja ilo via kiasi hicho.
Maswali ya nini kinamsibu Mzee Mkapa kiasi kwamba sisi vijana tunataka sheria ichukue Mkondo na kumkumba Babu huyu asiye na huruma hata chembe, babu aliyetetewa wakati wa uchaguzi wa 1995 kwa nguvu zote na Marehemu MWalimu Nyerere kwamba ni mtu safi, kumbe wapi bwana ilikuwa ni nidhamu ya woga na kujipendekeza kwingi kwa ndiyo mzee nyingi,
yalitakiwa yaulizwe na MH Mbunge siku ile Mbunge wa Moshi Vijijini alipo mtolea uvivu MH Mkapa na Jiko lake pale Bungeni.
Vinginevyo asituvurugie nia na hamu yetu ya kuwafikisha mafisadi wote mbele ya sheria bila kujali Umri, heshima vyeo,mvi na vipara vyao.
Tunaheshimu Mvi za mtu kwa kutegemea hekima na busara kutoka kinywani mwake na katika matendo yake. Lakini nathubutu kusema siku hizi kuna baadhi ya mvi zisizostahili heshima hata kidogo, na ukweli usiopingika kwamba vichwa na viwiliwili vilivyobeba mvi hizo kamwe havitakiwi kubaki mitaani na kuvuta hewa safi ya Muumba bure, mahali pao pa kupumzika mpaka uhai uwatoke ni jela tu.
Hoja ya MH Sendeka inaturudisha nyuma, aidha inatuingiza kwenye mviringo wa hoja unaotulazimu kueleza jambo hilo hilo kila mara.
Hatuwezi kutekwa kirahisi namna hiyo, hatuwezi kupelekwa alijojo kirahisi namna hiyo. Hii si hoja ya kutufanya tudhani mbunge hajui kulikoni.
Hizi ni njama za makusudi za kuvuruga uzito wa hoja kwa kutumia dhamana yake kama mbunge na nafasi yake katika jamii na heshima kwa wanao mheshimu ili kwa mara nyingine tena kutufanya wajinga na punda wa dobi.
Mbunge anajua kinachoendelea ila anajipamba kisiasa ili kujenga hoja itakayo mpa shibe ya kifisadi huko mbeleni kwa kuupa joto ufisadi.
MH Sendeka hapa hatuko kona zile za Pikadili kule Landani ambako inasemekana watu hutembea kisengerenyuma.
Usitizingue na wala usitutengulie udhu wetu kwenye hii hoja.
Hoja hafifu kama hizi kwa kawaida huwa zinawagharimu wote wanaozitoa. Iko siku ambayo haiko mbali kuanzia leo MH Sendeka utameza Maneno yako yote ulosema ikiwa ni pamoja na karatasi iloandikiwa au Wbsite nzima.
It is extremely expensive.