Semina ya walimu wiki nzima wanapewa laki tatu, hii sio Sawa

Semina ya walimu wiki nzima wanapewa laki tatu, hii sio Sawa

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
14,591
Reaction score
31,133
Hebu jithamini yani hata kama una shida kataa dharau, kuna semina zinaendeshwa mikoa yote Kwa Sasa walimu wa sayansi tu wanapewa pesa ndogo sana.

Semina ya wiki nzima wanapewa laki tatu hii sio Sawa tuwe na huruma, kama umasikin basi chanzo ni viongozi kumbuka huyu mwalimu analala hotelini tena gest za hovyo zenye kunguni analipia chumba, anajilisha jioni halafu mnampa laki Tatu sijui itafanya kazi gani.

Mwalimu unaenda kusahisha mitihani zaidi ya wiki mbili at the end unapewa laki tano, walimu jikubalini inabidi usisaini mkataba wa kusaisha au semina kama malipo hayafiki million moja kwa siku ulizokaa maana chini ya hapo utapoteza mda wako tena mbaya zaidi viongozi wanakuandikia umepewa pesaa million kumbe umepewa laki tatu

WALIMU UNGANENI

WALIMU PENDANENI
 
mpwayungu village naomba nikukosoe kidogo; hakuna semina mwl analipwa laki 3 kwa wiki.

Huwa hazidi 10,000-15,000 kwa siku. Hiyo pesa ndio humo humo chakula cha jioni na malazi. Hapo walimu wengine wametoka vijijini kwa nauli zao, wale jioni na walale kwa 10,000 au 15,000.

Asubuhi wanapewa maji, andazi 1, kiazi 1 na chai. Mchana wali, nyama na maji/soda.

Ni dharau ya hali ya juu walimu wanatendewa.

Semina zenyewe kwa mwaka hazizidi 3.
 
Unayelalama unajua utumishi wa uma lakini au unaongea tu. Maana ya kwenda s emina sio kwenda kulipwa hela uje kula na mke wako bali ni hela inayokusaidia matumizi ukiwa nje ya kituo cha kazi, hap9 ukivuka mkoa sehem ambayo hauwezi kurudi kwako watakulipa perdiem kulingana na cheo chako, ukifanyia ndani ya wilaya kuna gjarama yake pia
 
Back
Top Bottom