Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,620
- 46,264
Mgogoro wa China na Taiwan ni wa muda mrefu sana ila kwa sasa unakolezwa zaidi na vita vya Teknolojia ya semiconductors/microchips kati ya Marekani na China ambao wote wanategemea kwa sehemu kubwa Taiwan katika uzalishaji na ku supply kwao.
Taiwan ndiye kiongozi katika dunia ya sasa kwa 65% katika teknolojia ya microchips zinazotumika katika simu, computer, ndege, rockets, magari, vifaa vya hospitali, jeshi n.k. Ni kama vile ilivyo OPEC kwenye mafuta. Kampuni ya TSMC peke yake inazalisha 50% ya soko la dunia. Asilimia zilizobaki ndizo zinazalishwa na Korea Kusini, Marekani, China bara na Ulaya.
Xi Jinping, Rais wa China tangu aingie madarakani imeonekana ana nia na mpango wa kuimeza na kuinganisha kabisa Taiwan na China bara. Akifanikiwa na kama ataichukua Taiwan bila vita ambavyo vitaharibu biashara inamaanisha CCP itakuwa na total control ya biashara ya semiconductors jambo ambalo litakuwa pigo kubwa kwa US kwa kipindi kirefu. Pia Taiwan ikifanikiwa kujitenga kabisa inamaanisha China itapoteza ndoto ya kuwa wamilikaji wakuu wa biashara ya microchips duniani. Hapa ndipo kuna hesabu kali za kula au kuliwa.
Marekani tayari imepitisha Chips and Science Act, mpango dollar bilioni 53 kwa ajili ya kurudisha uwekezaji mkubwa wa semiconductor US, katika mpango huu makampuni yatakayowekeza US katika sekta ya semiconductors na kuonyesha mkakati wa kutofanya biashara ya semiconductors na China yatapewa ruzuku katika biashara zao.
Kuna wakati Taiwan ilipuuzwa na pande zote mbili, ila sasa hivi vita vya teknolojia vimeirudisha kuifanya "hot cake" ya kuwatoa wakubwa wa dunia roho.