Semi Trailer lavamia duka, watu watatu wanasurika kifo

Semi Trailer lavamia duka, watu watatu wanasurika kifo

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
WATU watatu wamenusurika kifo mjini Morogoro baada ya kutokea ajali mbaya ya lori la mizigo, (Semi Trailer) ambalo dereva wake ameshindwa kulimudu na kuparamia duka la dawa za binadamu.
ajali-morogoro-7.jpg

Hali ilivyokuwa eneo la tukio.



Tukio hilo limetokea leo mchana, Jumatatu Machi 19, 2018 katika Mtaa wa Nguzo, Kata ya ya Mazimbu eneo linalofahamika kama Ipoipo baada ya dereva wa lori hilo mwenye asili ya Kiarabu kufanya uzembe wakati akiendesha.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, wamedai gari hilo ambalo ni mali ya kampuni ya baba yake ijulikanayo kama AA. TRANS LIMITED, alikuwa akiliendesha kwa mbwembwe akitokea maeneo ya Tumbaku kuelekea Kihonda Maghorofani lilipomshinda na kusababisha ajali hiyo.

ajali-morogoro-12.jpg


Walionusurika ni dereva wa lori hilo (jina lake halijajulikana) aliyeumia kichwani na mikononi, muuza duka la dawa, Joyce Mwene, aliyeumia mkononi na begani.

Mwingine ni dereva wa gari dogo aina ya Toyota Noah aliyenusurika baada ya gari lake kukwanguliwa na kupasuliwa vioo vitatu huku yeye akitoka salama.

Jeshi la Polisi mkoani Mororgoro linamshikilia dereva wa lori hilo kwa mahojiano zaidi ambapo kwa sasa amepelekwa hospitali chini ya ulinzi wa polisi.

Source: Global Publishers
 
Kumbe ni mwarabu ni kawaida yao kukimbiza magari. [emoji4] [emoji591] [emoji613]
 
naona ana simu 2 na anapishana na trafic wawili
 
Hivi kulikua na haja ya kusema 'mwenye Asili ya kiarabu'?tumeanza kutambuana kwa Asili zetu?ok tukitoka hapo sijui tutaelekea wapi
 
Back
Top Bottom