Semenya ashindwa rufaa ya kuzuia AFP kudhibiti kiwango cha homoni kwa wanariadha wa kike

Fang

Content Manager
Nov 5, 2008
509
322
PARIS, Ufaransa

MWANARIADHA wa Afrika Kusini, Caster Semenya, ameshindwa katika kesi muhimu dhidi ya Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF), ikimaanisha kuwa shirikisho hilo litaruhusiwa kudhibiti viwango vya homoni za wanariadha wa kike.

Mahakama ya utatuzi wa migogoro michezoni (CAS), imekataa kesi ya Afrika Kusini ya kupinga sheria mpya za IAAF huku ikisema,a ilikuwa na hofu kubwa juu ya utekelezwaji wa baadaye wa sheria hizo mpya.

Semenya mwenye umri wa miaka 28, alibainisha kuwa sheria hizo si za haki na kwamba alitaka kukimbia kama alivyo, jinsi alivyozaliwa.

Sasa mshindi huyo wa Olimpiki, dunia na mashindano ya jumuiya ya madola kwa mita 800 pamoja na wanariadha wengine wenye jinsia zaidi ya moja, watalazimika kupata matibabu ili kushiriki mashindano ya kuanzia mbio za mita 400 au wabadili mbio.

CAS ilibaini kuwa sheria zilizokuwepo za wanariadha wenye zaidi ya jinsi moja zilikuwa ni za kibaguzi,lakini, ubaguzi huo ulikuwa muhimu wa kueleweka na wa uwiano kwa ajili ya kulinda maadili ya wanariadha wanawake “.(AFP).
 
Back
Top Bottom