Sema ukweli: Mara ya mwisho kununua gazeti ni lini?

Crimea

JF-Expert Member
Mar 25, 2014
25,481
35,138
Nimeona eti gazeti la mwananchi linapunguza wafanyakazi kwakuwa sijui mapato yameshuka. Mimi binafsi hela ya kununulia gazeti huwa naitumia kununulia bando ili nimalize kila kitu ntandaoni.

Kingine huwa sioni kipya kwenye magazeti cha kunifanya ninunue gazeti. Kwahiyo wajilaumu waandishi kwa kashindwa kwenda na wakati kiasi cha kufanya watu kuona bora wapate habari kupitia mitandao.

Je, wewe mara ya mwisho kununua gazeti ilikuwa lini? Mimi toka uchaguzi wa 2015 upite sijawahi kununua gazeti.
 
Nilikuwaga nanunua Mawio - Nikaacha, Nikaja Mwananchi na The Citizen nimeacha. Na kibaya zaidi mitandao ya kijamii ndiyo inayoongoza magazeti - Kiongozi akitoa hotuba unaipata PURE kupitia AYOTV, Kuliko Kusubiri MAGAZETI ambayo kila mwandishi ameandika ALIVYOIELEWA HOTUBA - HOTUBA MOJA TAFSIRI KIBAO
 
Mimi nina miezi 60 sasahivi sinunui gazeti zaidi ya Daily News kwasababu magazeti mengine kazi kuandika migogoro baina ya watu au viongozi na si kutuandikia mambo ya manufaa
 
miaka miwili sasa, hata redio nimepunguza kusikiliza maana intaneti mambo mubashala
 
Mi mara ya mwisho ni 2008.

Kwanza, mengi yanaandika udaku.

Pili, yanasomwa redioni kila muda nasikiliza huko na kuangalia vipindi vya TV.

Tatu, nasoma kupitia internet.

Mwisho, sitanunua tena printed media aina yoyote ile.

Labda, kama malaika watashuka na kufunga mitandao ya kijamii naweza nunua gazeti.
 
Nmeona eti gazeti la mwananchi linapunguza wafanyakazi kwakuwa sijui mapato yameshuka.

Mm binafsi hela ya kununulia gazeti huwa naitumia kununulua bando ili nimalize kila kitu ntandaoni.

Kingine huwa sioni kipya kwenye magazeti cha kunifanya ninunue gazeti.

Kwahiyo wajilaumu waandishi kwa kashindwa kwenda na wakati kiasi cha kufanya watu kuona bora wapate habari kupitia mitandao.

Je, wewe mara ya mwisho kununua gazeti ilikuwa lini? Mm toka uchaguzi wa 2015 upite sijawahi kununua gazeti.
Mimi sinunui sababu magazeti mengi yanakopi habari zao kuu jamii forums ukishasoma jamii forums unajua habari kuu kesho ni ili. Mfano kesho magazeti yataandika kuhusu taarifa ya nape kwa waandishi wa habari pia wataandika kuhusu spika kukubali kujiuzulu uongozi wa kamati wabunge wawili sasa kwa nini nihangaike kununua gazetti
 
Mi mara ya mwisho ni 2008.

Kwanza, mengi yanaandika udaku.

Pili, yanasomwa redioni kila muda nasikiliza huko na kuangalia vipindi vya TV.

Tatu, nasoma kupitia internet.

Mwisho, sitanunua tena printed media aina yoyote ile.

Labda, kama malaika watashuka na kufunga mitandao ya kijamii naweza nunua gazeti.
Mkuu miaka hiyo kulikuwa na hoja zenye nguvu sana huko magazetini lkn siku hizi upuuzi tu
 
pesa.jpg
Mara ya mwisho ilikuwa ni wakati wa kampeni za 2015.
Nilinunua Mawio likiwa na kichwa cha habari '' Samia Suluhu akigawa sadaka kwa wapiga kura''
 
Mkuu miaka hiyo kulikuwa na hoja zenye nguvu sana huko magazetini lkn siku hizi upuuzi tu
Teeeh teeeeeh haaaa haaa haaaa,

Ndiyo ni Kweli sasa hivi Gazeti habari inatoka kisha inaonekana siyo sasa kwa nini nisije hapa JF nikajisomea
 
Back
Top Bottom