Sema mchezo wako ulokuwa unaupenda

Sema mchezo wako ulokuwa unaupenda

Joined
May 22, 2017
Posts
65
Reaction score
299
NAJUA UMEPITA SHULE YA MSINGI EBU SEMA MCHEZO WAKO ULIOKUWA UNAUPENDA SANA SHULENI ENZI HIZO[emoji3][emoji16]. Mimi mpira wa miguu tena wa tambara weeeee[emoji119]

FB_IMG_1616561637037.jpg
 
Boli tu.. Mapumziko tunakiwasha kweli kweli, wakati wa kutoka kinapigwa tena..
 
Futbol mpira wa karatasi
Kivita vita

Nkiwa chekechea ae l pili kulikuwa na mchezo wa vizibo vya soda ,mtu begi la shule limejaw ivo vizibo ikaja kitu inaitwa puska😄😄😄
 
soka
goroli
kuendesha vilingi na makungo(mifuniko ya ndoo na matairi ya gari au ringi ya baiskeli )
 
Kombolela... mpira wa miguu..goroli...kuendesha na kutengeneza magari ya zile kamba za waya wanafungia mabelo ya mitumba.
 
Aisee kuruka sarakasi mpaka leo.

Enzi hizo primary kengele ya saa nne ikigongwa tu ni moja kwa moja tunaelekea shimoni walipokuwa wanachimba mchanga, basi ni kuruka sarakasi mwanzo mwisho ukitoka hapo umepauka balaa, nikitoka shule saa nane nakula naenda tena mtoni kuruka sarakasi tu majini, pia huko ukitoka umepauka ukiulizwa umeoga kweli leo unajibu ndiyo nilioga mtoni.

Yalikuwa ni mashindano mtaani, yaani sarakasi mpya ikiingia lazima uijue la sivyo unaonekana dogo huwezi kitu.

Mpaka kesho sarakasi siwezi acha aisee
 
Back
Top Bottom