nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
Friday, July 1, 2011
*Ni kwa ajili ya uchimbaji uranium
*Serikali yaomba kibali UNESCO
*Hekta 34,500 ndizo zilizolengwa
Na Dennis Luambano
SERIKALI imetangaza mpango wa kumega sehemu ya Pori la Akiba la Selous ili kuruhusu uchimbaji madini ya uranium.
Umegaji huo ni mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kila palipo na madini panabadilishwa matumizi.
Uamuzi kama huo ulishafanywa kwa kuhamisha Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ya Buhemba, Musoma mkoani Mara ili kupisha uchimbaji dhahabu ulioendeshwa na kampuni tata ya Meremeta.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, amewasilisha maombi ya mpango huo kwenye Mkutano wa Kamati ya Urithi wa Dunia uliofanyika Paris, Ufaransa kuanzia Juni 19-30, mwaka huu.
Pori la Akiba la Selous ni miongoni mwa maeneo saba nchini Tanzania ambayo yameorodheshwa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia. Maeneo mengine ni Hifadhi ya Serengeti, Hifadhi ya Ngorongoro, Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara, Mji Mkongwe Zanzibar na Michoro ya Mapangoni ya Kolo na Kondoa.
Waziri Maige alizungumza na waandishi wa habari jana na kusema kwamba Serikali ya Tanzania iliwasilisha kwenye Kamati hiyo, ombi la kutaka mipaka ya Pori la Selous ibadilishwe.
Serikali inataka kuondoa kipande cha hekta 34,532 kati ya hekta 5,120,000 za Pori hilo. Selous ndilo pori tengefu kubwa kuliko yote duniani.
Kipande hicho ni kile kilicho Kusini kwa Pori hilo. Mpango huo unalenga kuruhusu uanzishwaji wa mgodi wa uranium. Kisheria uchimbaji madini hauruhusiwi kwenye maeneo ya Urithi wa Dunia.
Ili ombi likubalike, linapaswa kuungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe 21 wa Kamati.
Alisema Kamati huwa ina namna nne za kufanya inapopata maombi kama hayo.
Namna hizo, alisema ni kukubali bila masharti, kukubali kwa masharti ambayo hurejeshwa kwa nchi mwanachama kuyafanyia kazi, kuyakataa na kuitaka nchi mwanachama iyarejeshe tena maombi upya baada ya miezi 18.
Muda huo hutumiwa na kamati ya wataalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni kutembelea nchi husika na kufanya uchunguzi wa kina na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati.
Namna nyingine ni kukataa moja kwa moja maombi kwa kuwa maombi yanakuwa yanakinzana kabisa na mkataba.
Waziri Maige alisema, "Baada ya uchambuzi wa kina Kamati ilikubaliana na Tanzania kwa masharti ambayo yanatakiwa yafanyiwe kazi kwa mwaka mmoja ili taarifa iwasilishwe kwenye mkutano ujao wa 36.
"Ilikubalika mchakato wa tathimini ya athari za mazingira ukamilishwe na uonyeshe athari zitakazojitokeza na mikakati iliyowekwa kupunguza athari hizo. ESIA iliyowasilishwa ilikuwa haijakamilishwa kwa kupata uthibitisho wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na pia ilionyesha baadhi ya athari zinahitaji muda mrefu kugundulika na hivyo haitakuwa rahisi kujua ukubwa wake.
"Timu ya wataalamu ya UNESCO itembelee eneo la mradi na ishirikiane kutengeneza mipango na mikakati ya kupunguza athari kwenye mazingira."
Maige alisema kwa kibali hicho, shughuli nyingine zinazoendana na uanzishwaji wa mgodi huo zinaweza kuendelea wakati mambo hayo yakifanyiwa kazi na kuwasilishwa kwenye mkutano wa 36.
Alisema mgodi huo utakapoanza kufanya kazi, hifadhi ya Selous itakuwa inapata dola milioni tano za Marekani kwa mwaka.
"Mradi huu una manufaa kwa uchumi wa Taifa, kwa sababu kama utaanza Selous itapata mapato ya dola milioni tano za Marekani kwa mwaka, kwa sasa hivi mapato ya Selous kwa mwaka ni Sh milioni 800," alisema Maige.
Kuhusu ujenzi wa barabara ya Mto wa Mbu-Musoma, alisema Serikali imeendelea kushikilia msimamo wake kuwa barabara haijengwi kwa lami kupitia hifadhini, bali lami itaishia mjini Mugumu, Serengeti kwa upande wa Magharibi na Loliondo kwa upande wa Mashariki.
"Tanzania imeeleza msimamo wake kuhusu barabara ya Serengeti itaishia mji wa Mugumu kwa upande wa Magharibi na Loliondo kwa upande wa Mashariki.
"Hivyo, kuacha kipande cha zaidi ya kilomita 123 kati ya Mugumu-Tabora B (kilometa 12), Tabora B-Kleins Gate (kilometa 53 ndani ya Serengeti) na Kleins Gate-Loliondo (kilometa 57) ambacho hakitajengwa kwa kiwango cha lami.
"Kipande ndani ya hifadhi kitaendelea kuwa chini ya usimamizi wa TANAPA (Shirika la Hifadhi za Taifa) kama ilivyo hivi sasa tofauti na barabara ipitayo Hifadhi ya Mikumi ambayo usimamizi wake uko TANROADS (Wakala wa Barabara Tanzania) hata kwa kipande cha kilomita 50 ndani ya hifadhi," alisema Maige.
Alisema taarifa kuhusu ujenzi wa barabara hiyo inatakiwa kutolewa na Wizara ya Ujenzi.