Selous yamegwa: Ni kwa ajili ya uchimbaji uranium; Hekta 34,500 ndizo zilizolengwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Selous yamegwa: Ni kwa ajili ya uchimbaji uranium; Hekta 34,500 ndizo zilizolengwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jul 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Friday, July 1, 2011

  *Ni kwa ajili ya uchimbaji uranium
  *Serikali yaomba kibali UNESCO
  *Hekta 34,500 ndizo zilizolengwa


  Na Dennis Luambano

  SERIKALI imetangaza mpango wa kumega sehemu ya Pori la Akiba la Selous ili kuruhusu uchimbaji madini ya uranium.

  Umegaji huo ni mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kila palipo na madini panabadilishwa matumizi.

  Uamuzi kama huo ulishafanywa kwa kuhamisha Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ya Buhemba, Musoma mkoani Mara ili kupisha uchimbaji dhahabu ulioendeshwa na kampuni tata ya Meremeta.

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, amewasilisha maombi ya mpango huo kwenye Mkutano wa Kamati ya Urithi wa Dunia uliofanyika Paris, Ufaransa kuanzia Juni 19-30, mwaka huu.

  Pori la Akiba la Selous ni miongoni mwa maeneo saba nchini Tanzania ambayo yameorodheshwa kwenye Orodha ya Urithi wa Dunia. Maeneo mengine ni Hifadhi ya Serengeti, Hifadhi ya Ngorongoro, Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara, Mji Mkongwe Zanzibar na Michoro ya Mapangoni ya Kolo na Kondoa.

  Waziri Maige alizungumza na waandishi wa habari jana na kusema kwamba Serikali ya Tanzania iliwasilisha kwenye Kamati hiyo, ombi la kutaka mipaka ya Pori la Selous ibadilishwe.

  Serikali inataka kuondoa kipande cha hekta 34,532 kati ya hekta 5,120,000 za Pori hilo. Selous ndilo pori tengefu kubwa kuliko yote duniani.

  Kipande hicho ni kile kilicho Kusini kwa Pori hilo. Mpango huo unalenga kuruhusu uanzishwaji wa mgodi wa uranium. Kisheria uchimbaji madini hauruhusiwi kwenye maeneo ya Urithi wa Dunia.

  Ili ombi likubalike, linapaswa kuungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe 21 wa Kamati.

  Alisema Kamati huwa ina namna nne za kufanya inapopata maombi kama hayo.
  Namna hizo, alisema ni kukubali bila masharti, kukubali kwa masharti ambayo hurejeshwa kwa nchi mwanachama kuyafanyia kazi, kuyakataa na kuitaka nchi mwanachama iyarejeshe tena maombi upya baada ya miezi 18.

  Muda huo hutumiwa na kamati ya wataalamu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni kutembelea nchi husika na kufanya uchunguzi wa kina na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati.

  Namna nyingine ni kukataa moja kwa moja maombi kwa kuwa maombi yanakuwa yanakinzana kabisa na mkataba.

  Waziri Maige alisema, "Baada ya uchambuzi wa kina Kamati ilikubaliana na Tanzania kwa masharti ambayo yanatakiwa yafanyiwe kazi kwa mwaka mmoja ili taarifa iwasilishwe kwenye mkutano ujao wa 36.

  "Ilikubalika mchakato wa tathimini ya athari za mazingira ukamilishwe na uonyeshe athari zitakazojitokeza na mikakati iliyowekwa kupunguza athari hizo. ESIA iliyowasilishwa ilikuwa haijakamilishwa kwa kupata uthibitisho wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na pia ilionyesha baadhi ya athari zinahitaji muda mrefu kugundulika na hivyo haitakuwa rahisi kujua ukubwa wake.
  "Timu ya wataalamu ya UNESCO itembelee eneo la mradi na ishirikiane kutengeneza mipango na mikakati ya kupunguza athari kwenye mazingira."

  Maige alisema kwa kibali hicho, shughuli nyingine zinazoendana na uanzishwaji wa mgodi huo zinaweza kuendelea wakati mambo hayo yakifanyiwa kazi na kuwasilishwa kwenye mkutano wa 36.

  Alisema mgodi huo utakapoanza kufanya kazi, hifadhi ya Selous itakuwa inapata dola milioni tano za Marekani kwa mwaka.

  "Mradi huu una manufaa kwa uchumi wa Taifa, kwa sababu kama utaanza Selous itapata mapato ya dola milioni tano za Marekani kwa mwaka, kwa sasa hivi mapato ya Selous kwa mwaka ni Sh milioni 800," alisema Maige.

  Kuhusu ujenzi wa barabara ya Mto wa Mbu-Musoma, alisema Serikali imeendelea kushikilia msimamo wake kuwa barabara haijengwi kwa lami kupitia hifadhini, bali lami itaishia mjini Mugumu, Serengeti kwa upande wa Magharibi na Loliondo kwa upande wa Mashariki.

  "Tanzania imeeleza msimamo wake kuhusu barabara ya Serengeti itaishia mji wa Mugumu kwa upande wa Magharibi na Loliondo kwa upande wa Mashariki.

  "Hivyo, kuacha kipande cha zaidi ya kilomita 123 kati ya Mugumu-Tabora B (kilometa 12), Tabora B-Kleins Gate (kilometa 53 ndani ya Serengeti) na Kleins Gate-Loliondo (kilometa 57) ambacho hakitajengwa kwa kiwango cha lami.

  "Kipande ndani ya hifadhi kitaendelea kuwa chini ya usimamizi wa TANAPA (Shirika la Hifadhi za Taifa) kama ilivyo hivi sasa tofauti na barabara ipitayo Hifadhi ya Mikumi ambayo usimamizi wake uko TANROADS (Wakala wa Barabara Tanzania) hata kwa kipande cha kilomita 50 ndani ya hifadhi," alisema Maige.

  Alisema taarifa kuhusu ujenzi wa barabara hiyo inatakiwa kutolewa na Wizara ya Ujenzi.
   
 2. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #2
  Jul 1, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Uranium inuzwa?!!!!!!!!!!!

  OMG!!

  Matumaini ya nishati ya kuaminika Tanzania yamefifia
   
 3. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hii kitu siipingi lakini tuwe makini sana.

  imefikia wakati watanzania tushirikishwe kwenye maamuzi makubwa kama haya
  tumewapa mawaziri zamana kubwa sana ili hali wananunulika kirahisi sana rejea BAE
  Haya makikataba ya madini yamekuwa mengi na yana misamaa mingi na waajiriwa wake wengi ni
  waindi nenda GEITA barrick mining wataalamu wakubwa pale ni wahindi

  tuhelezwe faida za huu uchimbaji kwanza kabla ya hiyo mikataba kuwekwa
   
 4. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hii nchi ilishauzwa, nasi tumebaki kuwa waangaliaji tu...
   
 5. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  me ua najiuliza kitu kimoja.
  hivi serikali hua haiamini kua tunaweza kuchimba wenyewe madiniyetu??
  kama ndio hua haiamani kua kuna siku na sisi tutaweza kuchimaba pekeyetu??
  kama ndio, ikifika wakati huo bado tutakua na reserve za madini au yatakua yameshaibwa yote??
  mantiki ni kua, kama serikali ingekua siriaz kuchimba madinikwa sasa tunaweza kabisa.
  wenzetu waaabu sio kwamba ni wasomi ila wao hununua technolojia kwa kutumia rasilimali zao(mafuta)
  sisi inamana tunashindwa kukopa WB na IMF tukanunua mitambo ya uchimbaji, tukawaajiri wataalam toka nje??
  (hata hivyo tunao)migodi mingi ya hapa hom wanaofanya kazi kubwa ni wazawa.wazungu wanasimamaiatu.
  tatizo serikali imewasaliti watu wake kabisa.iko siku tutawafunga viongozi wengi saana walioko/waliokwisha kua madarakani .
   
 6. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2011
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Sisi ni kuharibu haribu tu, hata katika hifadhi za taifa. Uharibifu wa mazingira utokanao na uchimbaji wa rasilimali ardhini ni mkubwa sana na athari zake husambaa kwa kiasi kikubwa pia. Nangojea ripoti ya timu ya "wataalam" ije ituambie kwamba tuchimbe tu na kisha tupate mrahaba wetu wa asilimia 3. Ni heri Selous libakie pori kuliko kukaribisha upuuzi mwingine.

  Tanzania na DR-Congo kumbe hatuchekani
   
 7. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,110
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Tanzania badala ya kutegemea Tax inatakiwa kuingia mikataba ya share ya 20% ya mapato kwenye market. Na hii market price iwe ya wakati inapouzwa. Hii itaongeza kipato badala ya kutegemea kodi pekee
   
 8. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hekta 34,500 za selous reserve ziharibiwe na huku unaendelea kuzungumzia uzalishaji umeme stieglers gorge? Unazungumzia kupeleka maji ya mto rufiji dsm!
   
 9. F

  Froida JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Si wangeanza kuchimba uranium ya dodoma huko na songea huko hatuna haraka kwa nini wasiache kwanza au mimi ndio sielewi jamani japo tunajua walishaanza kuchimba uranium waastralia siku nyingi tuu mungu wangu hawa wajukuu zetu watakuwa salama kwenye nchi hii kweli huu utajiri mkubwa wa rasilimali utatupeleka pabaya naogopa kweli
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Madini ni yetu, Ardhi yetu na bado hao Investors watataka Tax Break...

  What could our worst enemy do to damage this strong and beautiful country? CCM and the President, the One he could do no better than to get us to squander our human and natural resources on dubious missions and then trick us into plugging our ears against the howls of those who ob
   
 11. p

  plawala JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 627
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  I will never trust the current goverment to bring forward any valuable contract for tanzanians,especially in mining industry!

  Hii Uranium si kuna makampuni yanafanya majaribio ya kuchimba tayari?do we know anything good that is happening zaidi ya kudhalilisha wananchi ktk maeneo husika?
   
 12. kibonga

  kibonga Senior Member

  #12
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mikataba kama kawaida imeshasainiwa na MTEMI MANGUNGO kwa wale wanaokumbuka historia ya nchi yetu enzi hizooooooo hatuna letu sie kama wakimbizi wa ndani.................OK.....lakini iko siku za majuto .MAREKANI hawana ndugu Tutajuuuuuuuuuuuta.
   
 13. kibonga

  kibonga Senior Member

  #13
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  CCM mwenyekiti wao wa taifa hana uwezo wa uongozi wala maono ya mustakabali wa nchi yetu huko mbeleni (ccm angalieni mtu huyu hajiwezi)nchi ina angamia JUTENI hata nyie wenyewe (muondoeni )msingoje atumalize 20015 ni mbali sana jamani tuamkeeeeeeee
   
 14. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  completely unfair, hecta 34 elfu za hifadhi zinaharibiwa kwa 3% ya mapato wakati mwekezaji anachukua 97% na tax holiday ya miaka mitano na zaidi, hawa viongozi wanatakiwa wapimwe akili zao
   
 15. lifeofmshaba

  lifeofmshaba JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 868
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tanzania permitted to mine uranium in Selous


  BY GADIOSA LAMTEY
  [​IMG]
  Minister for Natural Recourses and Tourism Ezekiel Maige


  The World Heritage Centre (WHC) committee has permitted Tanzania to start exploring uranium in Selous Game Reserve, after the country has met two referral conditions she had been required earlier to fulfill.
  According to Minister for Natural Recourses and Tourism Ezekiel Maige, the government had been required to work on the two conditions within a period of one year to allow a report to be submitted in the 36th WHC conference.
  Making the revelation on the WHC decision reached in France late last month to journalists in Dar es Salaam yesterday, the minister said Tanzania had first been asked to conduct Environmental and Social Impact Assessment (ESIA) indicating possible effects that might occur and work out strategies to minimise their impacts.
  In the second condition a United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization (Unesco) team was required to visit the project site and work together with government officials in preparing a mining plan and strategies to minimise environmental impacts.
  The first condition ESIA submitted to the centre was incomplete because it was not approved by the National Environment Management Council (NEMC) and it showed that it could take long time to discover some of the effects and might not be easy to know their magnitudes.
  "Under the permit, other activities relating to commencement of mining can continue while the two conditions were being worked on and submitted to the 36th WHC conference," the minister.
  During the conference, the government took the opportunity to endorse the 1972 International Agreement on Biodiversity Conservation and Protection.
  Under the agreement, the minister said, areas that have unique heritage will be recognised and listed in World Heritage Sites under Unesco. According to the agreement, exploration projects are not allowed in the game reserve, he added.
  However, given the importance of uranium mining to Tanzania, the government submitted a requested to have the boundaries of Selous Game Reserve changed, and have its 34,532 ha reduced to pave way for the project, he said.
  "The centre gave us conditions although Tanzania is our land because of the agreement the government signed which prohibits exploration activities at WHS. The project however is important for the community and government because 78 per cent of the mineral products will remain in the country and create employment," he said.
  Commenting on national conservation in the country, he said WHC received the country report but was somewhat pessimistic about conservation of Serengeti National Park (senapa)-specifically on the proposed road project.
  At the meeting, the government explained its stance that the Serengeti road project will not be constructed at tarmac level, (the tarmac will end at Loliondo on the eastern side, leaving 123 kilometers which will be under Tanzania National Parks (Tanapa), he said.
  On Wednesday Tanzania and Uganda signed a multi-billion-shilling railway construction project to run from Tanga via Arusha to Musoma which authorities said would steer clear of the much contested Serengeti National Park stretch by 100 kilometers to preserve the ecosystem.
  According to Transport minister Omar Nundu, the project will consider concerns by Tanzanians and the international community over the need to preserve Serengeti National Park's ecosystem.
  The plan to steer clear of the particular stretch follows reports by the international media that the government has dropped plans to build a highway through the world-famous park.
  The reports also suggest that the government has informed Unesco's World Heritage Committee that it would continue with its plans to build the proposed Arusha-Musoma highway but without touching the 53km stretch through the National Park.  SOURCE: THE GUARDIAN
   
 16. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,583
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  hii kitu BUNGE si lilikataa? naona wamezunguka mlango wa nyuma kupitia UNESCO na UNESCO yenyewe si walewale?
  Si bure jamaa kila siku yupo ulaya na wageni wa MAREKANI hawaishi nchi hii!!!!
   
 17. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Niijuavyo nchi hii sasa hv utasikia mkataba mbovu. Na hawakawii kuufanya siri.
   
 18. m

  mzee wa njaa JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2011
  Joined: Jun 16, 2011
  Messages: 1,368
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Barabara Kupita mbugani wamegoma leo wanakuja na hili la uranium hawa jamaa wako vp? Kuna kitu nyuma ya pazia kwa kweli.
   
 19. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #19
  Jul 1, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,465
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  5 millon dollar ni kidogo bora yakae ardhini.
   
 20. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Ezekiel Maige said he told the recent UN World Heritage Centre meeting it would mean the park's size would need to be reduced by less than 1%.
  The UN body said it would approve the plans, as long as environmental assessments were carried out.

  Money made from the mining would help in the park's upkeep, Mr Maige said.
  According to the UN cultural organisation Unesco, the 5m hectare-Selous Game Reserve in the south of Tanzania has large numbers of elephants, black rhinos, cheetahs, giraffes, hippos and crocodiles - and is relatively undisturbed by humans.

  'Regrettable'
  In an interview with the BBC Swahili Service, Mr Maige said the uranium mining project was in its infancy, but it would only affect about 0.69% of the current World Heritage site park and would be an important source of income for the country.
  Firms could expect to earn $200m (£125m) each year from mining uranium from the site, of which $5m would be paid to the government, he said.
  Some of this would be able to help with the costly business of managing the park, and it would provide employment for about 1,600 Tanzanians.
  During the annual meeting of the World Heritage Committee, the minister said concern had also been expressed about the Undendeule Forest Reserve, to the south of the Selous Game Reserve.
  But Mr Maige, who also serves as Tanzania's tourism minister, insisted there would be no impact on that forest either.
  He said it currently costs the government about $490,000 a year to manage it and the income from mining would help pay for guards to stop poaching.
  He said Tanzania did not need permission from Unesco to go ahead with its uranium mining plan, but the East African nation wanted to take into account the organisation's recommendations.
  "The uranium project will go ahead," he told the BBC.
  Unesco spokesman Lazare Eloundou Assomo told the BBC it would be "regrettable" if Tanzania started uranium mining without the UN body's approval.
  He did not say how long the assessments would take.
  The World Heritage Committee wanted Tanzania's own assessment to be approved by the country's environmental agency, Mr Maige said.
  The second requirement was for a UN team of experts to visit the area to give their own recommendations for the protection of the ecosystem.
  The minister said a decision would then be taken at next year's WHC meeting about changing the boundaries of the Selous Game Reserve.
  Studies so far had shown that there was no need for concern about radiation poisoning from the uranium extraction in the area, Mr Maige said.
  "Radiation levels will remain the same - the minerals in the ground are already emitting a degree of radiation, but it is not dangerous for human beings, the animals or the [Mkuju] river," he said, adding that the uranium would be processed abroad.
   
Loading...