Selikali itupie jicho biashara za wachungaji hawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Selikali itupie jicho biashara za wachungaji hawa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by silver25, Dec 21, 2010.

 1. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wachungaji hawa mimi nawatabiria Watakufa na Makanisa yao,
  Kwasababu hazina Kichwa wala miguu, na sijui makao makuu ya Makanisa hayo, na Kama hayapo kibiashara, sasa wanafanya nini hapa Tanzania zaidi ya KUGOMBANIA WAUMINI WENYE PESA ZAO?
  sELIKALI INATAKIWA ITAZAME BIASHARA HII WANAYO IFANYA WACHUNGAJI HAWA ikiwezekana basi wapate kibali na wawe wanalipia kodi, haina tofauti na ile ya DECI lakini hii waumini wakitoa hawarudishiwi..

  Mchungaji Joseph Gwajima ("The Glory Church" ufufuo na uzima)
  Mchungaji huyu anawadanganya Uma wa Watanzania kuwa yeye huwafufua watu ambao wameaminika asilimia 100% na kuwaleta duniani tena akidai hawakufa bali wanaishi sehemu tu akiitwa majina ya kigiza MISUKULE.
  UKIFUATILIA HUKUTI HISTORIA YA MTU HUYO KUWA ALIKUFA NA NDUGU HUWAONI INAONEKANA NIWATU TU WA MJINI HUWA WANALIPWA NA KUIFANYA KAZI HIYO YA KUUPOTOSHA UMA WA tANZANIA, na yeye atakufa na kanisa lake coz waumini humfuata yeye tu

  Getrud Rwakatale
  Nayeye anajifanya ni mchungaji Mwanamke, katika Biblia sijawahi kusoma Sura hata moja nikaona Mchungaji au kiongozi wa kanisa ni Mwanamke, Sasa yeye amejiundia Biblia yake pekeyake na kujifanya yeye ni mchungaji ili apate kushirikiana na Selikali kuiba na Kurubuni Mali za Watanzania, na ndiyo maana leo hii amechaguliwa kuwa Mbunge viti maalum. na huyu takufa na kanisa lake.

  Kakobe Zakaria
  Jamaa alianza vizuri sana, lakini na yeye aalewa sifa na kujiona sasa Maisha ameyapatia, kwani sasa anataka hadi kushindana na Selikali katika Mambo ya muhimi na ya kimaendeleo, cha kushangaza Mambo yake binafsi anawashirikisha na waumini wa kanisalake kiasi cha kutishia Amani ya nchi.
  bila kujitambia Waumini humfuata yeye na akifa wata sambalatika kama wenzake Gwajima na getrud

  Lusekelo Anthony
  Jamaa ana mbwembwe sana na haoni haya kumnyima mtu baraka kama yupo nje na kanisa lake Huku akikuambia uje kanisani ili upate upako..
  andalia hapa..
  Awali, waandishi walimwomba Mzee wa Upako kusali kabla na baada ya mkutano ili wapate baraka kutoka kwa Mungu, lakini alikataa akisema wanaotaka kuombewa waende kanisani kwake Ubungo-Kibangu. Baada ya kukataa kushusha sala, aliulizwa na waandishi kama maneno aliyoyasema alishushiwa na Mwenyezi Mungu baada ya kusujudu na kufunga ili kuinusuru Tanzania au alitumwa na mmoja wa watu hao walioko kwenye mvutano. Akijibu swali hilo, alisema hakulishwa maneno na Mungu wala mmoja wa mahasimu, bali aliamua kutoa msimamo wake kama Mtanzania mzalendo. na yeye ataondoka na kanisa lake

  Farancis Mkwera
  Huyu jamaa alikuwa Padre wa kiroma, kutokana na utovu wa nidhamu kulikosea Kanisa kuu kuliko yote Duniani Roman Katoliki, alisimamishwa kwa muda ili ajifunze, kutokana na makosa yake,,
  Mkwera aliamua kuonesha umwamba kwa viongozi wake, na kuamua kuondoka na kuanzisha kikanisa chake ambacho hatujui ni cha aina gani walokole, au pentekoste au hakifahamiki kabia, nayeye anajiuliza je Atazikwa na Kikanisa chake?

  Ufafanuzi wa Thread hii ni kwasababu ya mienendo ya kibiashara ambayo Makanisa haya na Wachungaji wake wamejijengea, sote tumeona Faida anayo pata Mama Rwakatale ni Kuanzisha mashule mbalimbali ili kujinufaisha zaidi, na sasa kwaPesa za waumini wake anampango wa kuanzisha chuo kikuu..

  Hawa wote wakifa watakufa na Dini zao,
  lengo langu mimi ni Salikali iwaangalie hawa kwa jicho la tatu siono tofauti na Matapeli jamani, Wana watapeli Waumini wa Dini zao,./
   
 2. K

  Kagasheki Member

  #2
  Dec 21, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii mada in ukweli kwa asilimia 100,Dini imekuwa biashara inayowalipa wajanja wachache mijini kupitia mgongo wa maskini wengi waliokata tamaa na maisha.Wamefikia hatua ya kumghilibu Mungu kupitia mgongo wa makanisa yao yenye waumini Dar es Salaam pekee na wachache mikoani.Kuna mfano mzuri sana wa Askofu Zakaria Kakobe ambaye miaka kadhaa iliyopita aliwika sana kupitia mahubiri ya Injili, lakini baadae akaanza kukimbiwa na waumini wale wale waliomuunga mkono kwa kiasi kikubwa.Hivi sasa anaganga njaa na waumini wa kuhesabu maana wameibuka wachungaji wengine wanaomzidi umaarufu na kuvuta watu wengine wa aina aliyokuwa nao kanisani kwake.
  Kimsingi chimbuko la kuibuka kwa makanisa kila kukicha haswa Dar es Salaam ni kwasababu ya shida na mahangaiko yanayowakabili walio wengi hivi sasa ktk maisha.Hili linathibitishwa na kukosa uvumilivu kwa waumini wa dini za asili na hatimaye kuvutiwa na ulaghai wa wachungaji hawa matapeli kuwatatulia matatizo yao kwa muda mfupi ila kupitia fedha.Matokeo yake wanatozwa fedha nyingi kwenye makanisa hayo kama sababu ya kuombewa kwa shida walizonazo na kuishia kuwatajirisha wachungaji hao na wao kubaki maskini.Mfano mzuri wa wachungaji wa aina hii ni Anthony Lusekelo wa G.R.C-Ubungo Kibangu ambaye anaishi maisha ya anasa kwa kulaghai waumini wake kuwa ni suluhisho la mahangaiko yao ya dunia.Wizi mtupu.
  Jambo moja ni dhahiri makanisa haya huja na kupotea kama ilivyowahi kutokea kipindi cha Askofu Moses Kulola.Ni utapeli ambao huvuma na kushawishi wajinga walio wengi na kuwapumbaza kwa kipindi fulani,lakini ukweli unapokuja kudhihirika basi ndipo huwa mwisho wa kanisa lenyewe.Ni kweli wanatengeneza pesa ya kutosha kufikia hatua ya kujitangaza kwa gharama kubwa lakini wanachofanya kupita mgongo wa Mungu ni laana kubwa pindi watakapotoweka kwenye uso wa dunia hii.Watatajirika kupitia mgongo wa maskini lakini hawatofurahia na kudumu na utajiri huo kwa muda mrefu.Mwisho wa siku waumini wao watarudi kwenye makanisa yao ya awali waliyoyakimbia na kulazimika kutubu zaidi kwa usaliti walioutenda.
  Dunia ni shule nzuri sana kwa wanaoishi humo maana hufundisha yanayopaswa kwa watu wake.Tunafahamu fika kuwa tunaishi siku za mwisho kama ilivyoainishwa kwenye vitabu vitakatifu lakini ujio wa makanisa ya leo umekuwa tatizo kubwa kwa walio wengi.Ni suala la muda tu ukweli utadhihirika
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,653
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Unaona eh!!! Mimi hapa sitii neno, ila huu ni ukweli kabisa.
   
 4. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #4
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  no comment
   
 5. B

  BA-MUSHKA Member

  #5
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumuachie Mungu pekee ahukumu maana hata hao viongozi wa serikali wanasali humo humo, hawata tenda haki.
   
 6. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #6
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  haya madhehebu ni chokochoko za marekani kuiua roman empire!kuna kipindi bot walizuia 20bil kutoka usa zilikua za dhehebu fulani!
   
 7. c

  chach JF-Expert Member

  #7
  Dec 21, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 439
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  sasa wataanza kufungua mabenki
   
 8. p

  pierre JF-Expert Member

  #8
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Haya ni maisha,kuhusu kusema watahukumiwa au la hilo sio la mwanadamu,maana hakuna ajuaye baada ya kifo.Naona aliyetoa hoja hii naomba kusema kuwa huenda anaona wivu wa mafanikio walioyapata hawa jamaa.Hii tunaiita ni biashara kamili kama ilivyo biashara nyingine halali,unapoiva kiroho na ukaweza kuwapa watu matumaini ya maisha Mungu naye anakuinua kwa kukupa kama walivyopata.Ukiona inalipa ingia uwanjani na wewe ujaribu uone kama utafika walipofika,usikalie kuwasema kwa kushindwa kwako.Lipi bora mtu anayetumia maandiko ya Mungu kufanikiwa ua yule anayeiba???Jihoji nafsi yako mwenyewe.
  Mimi naona cha kufanya ni kuwatafuta hawa ndugu Kakobe,Rwakatare,Gwajima na Lusekelo tuwaulize tufanye nini ili na sisi tuweze kutoka???Badala ya kupiga majungu,naona hii ndio shida ya mtanzania huyu amekalia majungu.
   
 9. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #9
  Dec 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pierre wewe unauhusika wa silimia 70% ya uumini wa watu hawa na ndio maana povu limekutoka kusema mimi nina majungu hivi wewe unayajua majungu, sasa wewe hayo uliyo yafanya ndo majungu
   
 10. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #10
  Dec 21, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Duh! Si mchezo hapa sitii neno
   
 11. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #11
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Unayoyazungumza hapa katika tread yako kama yatakuwa na ukweli basi ukweli wenyewe huo huo unayahusu haya madhehebu mengine unayoyaita ya asili ambapo ndiko uliko wewe. Usifikiri kuna chochote cha ukinyume na biblia kinachofanywa na hao uliowataja ambacho hakifanywi na hayo madhehebu ya kale. Tofauti kidogo iliyopo ni kwamba haya madhehebu ya kale yanawafuata watu wa mataifa ya magharibi kama Roma Italy (Rc) ujerumani(Lutheran), Uingereza(angelikana) nk. Na haya madhehebu mleta tread anayoyashutumu yanawafuata waasisi wa kitanzania na head quoter yao ni hapo hapo katika kanisa la local. Kwa mtizamo wangu nuru ya injili ya Yesu inawaka zaidi na kwa kiwango kinachokaribia ukweli wa kibiblia kwa haya madhehebu ya kina Kakobe kuliko kuliko uvugu vugu na kupoa kulikoyakumba haya madhehebu yanayoitwa ya asili.
  Kuanzia zama za Yesu hadi sasa Nuru ya kweli ya Mungu huwepo kwa mtu fulani kwa wakati fulani na ikiisha kuppita mda fulani kwamba mleta nuru hayupo labda ameishakufa ndipo kizazi cha wafuasi wake huanzisha dhehebu kwa kujaribu kuundia kanuni za sharti kwa kile wanachoita fundisho la yule mtu. Kufanya hivyo ndiko kunakofanya hilo kundi kujitenga na kweli kwa sababu ya error waliotengeneza. Kifupi ni kwamba kazi yoyote iliyoanzishwa na yeyote inayopingana na kipengele chochote cha bibilia haifai kuaminiwa.
  NI YESU(NENO) TU NA YESU PEKEE. FINISH!!!
  .
   
 12. silver25

  silver25 JF-Expert Member

  #12
  Dec 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 744
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sina cha kusema kiby lakini ujue hawa wamezidi bwana wamefikia hata kuppigana vijembe, mi binafsi ninampango wa kuwa mpagani
   
 13. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #13
  Dec 21, 2010
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wivu wa kijinga na uvivu wa kufikiria.
  katiba inaruhusu mtu kuwa na uhuru wakuabudu
  hakuna aliyelazimishwa kwenda huko ila kwa miguu yake na nafsi yake
  hata kama itafikia kuchomwa moto kama kanisa la kibwetere pale kampla uganda.
  wewe ni miongoni mwa wanaotaka kuvunja katiba, WHY?
   
 14. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #14
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Umewasahau akina Fernandes wa ATN,Geo Davie wa ngurumo ya upako,akina Steven Lukindo wa Top Radio na wengine wengi waliobuni viji-ministries huku wakihubiri mahubiri ya miujiza na mafanikio.Wamesahau kabisa kwamba neno la Mungu linasema"tafuteni kwanza ufalme wa Mungu na haki yake na hayo yote mtazidishiwa."
   
 15. kagumyamuheto

  kagumyamuheto JF-Expert Member

  #15
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  No Coment here. Th truth!!!
   
 16. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #16
  Dec 21, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280

  .
  Usijidanganye ndg yangu, upagani nao ni dini. Sema tu tofauti iliyopo kati ya upagani na hizi dini nyingine ni kwamba itakapotokea kukawa na maisha baada ya kifo cha mwili (ambapo na mimi binafsi naamini hivyo), basi tutakuwa tumelamba dume na dini ya kipagani kuingia mkenge. Mambo yakiwa tofauti(ambapo binafsi siamini hivyo), sii upagani wala dini nyinginezo zitakuwa zimepoteza kitu.
  .
   
Loading...