Umenikumbusha tukiwa wadogo tulikuwa tunachagua magari barabarani. Mnakubaliana itakayokuja ni ya huyu, itakayofata ni ya mwingine.
Sasa kuna muda linakuja gari zuri sana mnaligombania, na ngumi zinapigwa, mtu akiuliza kwa nini mnagombana yule mwenye haki anasema wanataka kuninyanganya gari langu…!