Self defence basics: Part 1

zubedayo_mchuzi

JF-Expert Member
Sep 2, 2011
4,873
1,217
HABARI ZENU WAKUU???

Leo nakuja tofauti kidogo,kwani baada ya kuona wanajamii wengi wamekua wakivamiwa na vibaka wadogo wadogo,kwa wakati mwingine huwa kuna mazingira ya kuwataiti lakini mtu anakosa maarifa.

Nianze na mtu mwenye mazoezi ya pumzi,namanisha kwa yule anaekimbia,na kufanya mazoezi ya kurusha ngumi hata kama ujui unarusha ngumi ya aina gani na kwa wakati gani lakini unajitahidi kufanya hivyo.

leo tuoangalie sehemu 5 muhimu katika mwili wa binadamu ambazo ni rahisi kuzishambulia na adui wako wakakukimbia na kukuacha kabisa,leo tutaangalia sehemu 3 za msingi kabisa kwa yeyote yule kujilinda pindi anapo vamiwa gafla na watu wawili au watatu.

1.PUA
2.KOROMEO
3.MAKENDE

MTU mwingine atashangaa yaani hivi vitu vitatu ni hatari kwenye mwili wa binadamu nasema ni hatari kuliko unavyodhania wewe.

Sasa basi pindi unapovamiwa na kuwekwa kati kitu cha kwanza tulia angalia kati yao watu walipoweka uwazi mkubwa wa wewe kupita eneo hilo,utakacho kifanya hapo ni kuhakikisha awa kuweki katikati kuepusha mashambulio ambayo yanaweza kukudhuru ,nikimanisha kama wanasilaha yoyote.

kitu cha pili kuwa makini na movement ya mikono yao kujua wamebeba nini mkononi,akili yako iwe shapu kuamua na kushambulia.

hakikisha unaposhambulia unashambulia kati ya sehemu hizo tatu hapo juu,ingawa pua na makende ni rahisi sana,unaposhambulia maeneo hayo hakikisha unavuta pumzi nje na unapo shambulia unapeleka shambulio la nguvu moja ambalo litamfanya adui apate maumivu makali,kama watakupa nafasi ya kushambulia wawili au mmoja vizuri wengine watasita kuja kichwa kichwa,na wewe utapata nafasi ya kujiokoa.

kila adui atakaekuja utamshambulia kwa kuangalia udhaifu wake ,kama atakupa nafasi ya kupiga kwnye makende piga kama hautapiga tena,

kwenye koromeo ni hatari sana kwani unaweza poteza uhai wa mtu kama utashambulia kwa shambulio zito.upigaji wa koromeo unahitaji mazoezi sana,kwa ngumi ni ngumu kidogo.

ila wanapokua zaidi ya wa tatu hakikisha unapambana nao huku ukikimbia kimbia yaani usikae eneo moja unapokimbia yule mwenye mbio ndie atakae kufikia kwa haraka basi,kwasabab hajui utampigaji utamshambulia kwa kujua kua huyu hapa hatarudi tena.

ila katika mashambulio hayo ni lazima uwe na mazoezi yatakayokupa stamina,watoto wa mtaani wanaita stopa.Nahakikisha unapopeleka ngumi unapiga sana jap ,jab ni ngumi inayopigwa kwa kunyoosha mkono.

kwa leo yangu haya

ANGALIZO: MASHAMBULIO HAYA MSIYAFANYE KWA WAUME ZENU NA WAKE ZENU MTAFUNGWA.

Ukishambulia sana pua utasababisha pua hizo zivuje damu kwa wingi na kama utashambulia zaidi utasababisha adui yako macho yake yaone kama ukungu.ukiendelea kushambulia zaidi mtu anaweza kudondoka chini na kupoteza fahamu.

zubedayo_mchuzi mzee wa kutembea umbali mrefu.
 
Kwa kuongeza unapovamiwa ghafla jifanye ni muoga na upo tayari kutoa ushirikiano huku ukihakikisha hawakuzunguki kwa namna itayokunyima kushambulia au kutoroka ....ukionyesha uoga mara nyinyi adui anapunguza tahadhari inayokupa fursa ya kumshambulia kwa nguvu ghafla.
 
Mi hayo mambo ya kuruka juu siyawezi maana ka mwili kangu haka na kamkono mapigano huwa siyawezi kabisa.

Self defence yangu mi ni strategies ya kujiepusha na hatari in advance. Ndo mana mpaka sasa pamoja na kuishi maeneo hatari hatari ila sijawahi kuwekwa kati na vibaka.

Mfano wa Strategy zangu
1 Nikichelewa usiku wa manane kama mida kuanzia saa 7 usiku. Huwa napita vichochoroni nikiamini kwamba wakati huo vibaka wengi wanakuwa wanatega kwenye njia kuu. kwa hiyo ni kama napishana nao.

2 Huwa napenda kupita njia tofauti tofauti. Hii inaondoa kuwa predictable. Sio kila siku usiku unarudi home kupita njia moja. Ukiwa predictable utachorewa ramani kirahisi.

3 Huwa napenda kutembea pembezoni kabisa mwa barabara maana ukiwa hiyo location ni rahis kutulia na ku observe situation pale unapoana jambo lisilo la kawaida pasipo kushtukiwa. Na kama kuna hatari ukapata mwanya wa kupotea kwa haraka pasipo kushtukiwa.

4 Pia huwa napenda kusoma nyuso za watu nnaowaona ama kupishana nao. Maana in most cases intention ya mtu ukitulia vizur inajionesha kabisa kwenye uso wake bila kificho.

5 Epuka maongezi na mtu usiyemfaham katika mazingira na mda usioridhisha. Sio upo mitaa ya keko saa za jioni unaona kajamaa kanakuja kanajifanya kanakufaham mara imepanda imeshuka hapo unajiweka kwenye hatari.

Ni hayo tu na ujanja ujanja mwingine ulioniwezesha ku survive kwenye maeneo hatar hatar pasipo kuwekwa kati hata siku moja.
 
Nimeipenda hii, asante kwa kushare!
 
Ni nzuri sana ,maana vibaka wameongezeka sana siku hizi na msaada kwa jesho la polisi ni mdogo saana.Vijana wengi wanajulikana hawa.
Kuna maeneo huku Zanzibar walivamia muda mrefu,alikufa mmoja tu walitia akili,pakatulia kwanza.Sasa hivi eti polisi wanatafuta muuwaji,aisee
Mie mkuu natembea na kisu kiunoni,ndio maisha yangu,baada ya huu mchezo wa kabakaba kizembe
 
Hii mada nimependa sana, mfano hapo kwenye pua, ukipigwa ngumi ya pua ikaingia sawa sawa, ni chungu hasa kama umeingiliwa na kitunguu machoni. Mziki mwingine hatari ni kwenye makende hapo lazima mtu alie kama nguruwe. Pamoja sana mleta mada na wachangiaji wengine.
 
Sasa kama na hao vibaka wanasoma Maujanja haya si hatari jiddah? Itakuwa sawa na Simba na Yanga kuloga kwa mchawi mmoja
 
mkuu unapovamiwa kwanza lazima utulie,usipaniki kinachotokea ni wewe kucheza na weekness zao wakati wanataka kukushika wakusachi,hata hao vibaka wanao piga ngumi,wao wanajua kupiga ngumi tu,hawajui mwili wa binadamu unamaeneo yake muhimu ukimpiga mtu anatulia.

kwa mfano unapopigwa kabali ya nyuma,kikubwa watakacho kufanya ni kukukata pumzi kwa kupiga lower cross,sehemu wanayopiga tunaamini kuwa ni kwenye mapafu.

unaangalia anakujaje na wewe unamshambulia vipi.
 
Mkuu kuna ile ya kung' at a piap
kung'ata ni tekniki ya kupangua kabali ya nyuma,na nikitendo unachotakiwa kukifanya huku ukihahakisha una pumzi ya kushambulia adui wako wa mbele anaekuja,

unaposanikiwa kutoa kabali hiyo,hakikisha muda ule ule anaopiga kelel kwa maumivu unamshushia konde jingine kwe nye pua,au koromeo.kumchanganya adui wako
 
hii yako ni nzuri ,maana hapa unacheza na mazingira,kuna kuvamiwa kwa kufuatiliwa vijana ndivyo wanavyofanya,vibaka wetu akibeba kisu anajiamini kweli kweli.ukijua si mbaya

Mi hayo mambo ya kuruka juu siyawezi maana ka mwili kangu haka na kamkono mapigano huwa siyawezi kabisa.

Self defence yangu mi ni strategies ya kujiepusha na hatari in advance. Ndo mana mpaka sasa pamoja na kuishi maeneo hatari hatari ila sijawahi kuwekwa kati na vibaka.

Mfano wa Strategy zangu
1 Nikichelewa usiku wa manane kama mida kuanzia saa 7 usiku. Huwa napita vichochoroni nikiamini kwamba wakati huo vibaka wengi wanakuwa wanatega kwenye njia kuu. kwa hiyo ni kama napishana nao.

2 Huwa napenda kupita njia tofauti tofauti. Hii inaondoa kuwa predictable. Sio kila siku usiku unarudi home kupita njia moja. Ukiwa predictable utachorewa ramani kirahisi.

3 Huwa napenda kutembea pembezoni kabisa mwa barabara maana ukiwa hiyo location ni rahis kutulia na ku observe situation pale unapoana jambo lisilo la kawaida pasipo kushtukiwa. Na kama kuna hatari ukapata mwanya wa kupotea kwa haraka pasipo kushtukiwa.

4 Pia huwa napenda kusoma nyuso za watu nnaowaona ama kupishana nao. Maana in most cases intention ya mtu ukitulia vizur inajionesha kabisa kwenye uso wake bila kificho.

5 Epuka maongezi na mtu usiyemfaham katika mazingira na mda usioridhisha. Sio upo mitaa ya keko saa za jioni unaona kajamaa kanakuja kanajifanya kanakufaham mara imepanda imeshuka hapo unajiweka kwenye hatari.

Ni hayo tu na ujanja ujanja mwingine ulioniwezesha ku survive kwenye maeneo hatar hatar pasipo kuwekwa kati hata siku moja.
 
hii yako ni nzuri ,maana hapa unacheza na mazingira,kuna kuvamiwa kwa kufuatiliwa vijana ndivyo wanavyofanya,vibaka wetu akibeba kisu anajiamini kweli kweli.ukijua si mbaya
Mbinu zako ni nzuri.. Ila kwa watu wengine kama sisi suala la kupigana hatuwezi halafu isitoshe wao wanakuwaga na silaha halafu wewe hujajiandaa. So risk ya kujeruhiwa naona ni kubwa sana.
 
Back
Top Bottom