Sekta ya nyumba imeanza kufufuka kwa kasi chini ya Rais Samia Mama wa Uchumi

Real estate ilidorora hapa dar kwasababu ya serikali kuhamia dodoma and not either way.


Mbona hujiulizi kwanini dodoma real estate ilishamiri na viwanja vilipanda bei baada ya serikali kuhamia huko.


Umewahi kujiuliza real estate itakuwa hivyo hivyo dodoma kama serikali ikihamia mbeya au iringa
 
Hakuna mahala nimesema tabu zimemalizika ila nasema kujenga ni kazi kuliko kuharibu .

Uchumi uliharibika Kwa miaka 6 sio rahisi kujengeka Kwa miaka 2 ila Hali ni nzuri zaidi Sasa kuliko hapa awali.
Hali ni nzuri kukiwa na mfumuko wa bei hali ni nzuri wafanyabiashara wakihodhi mafuta na serikali haiwezi sema kitu. Hali ni nzuri gharama za maisha zimepanda thamani ya pesa imeshuka na vipato havijaongezeka mzee upo serious kweli? Kama vipi andika namba za simu na mahali ulipo unastahili teuzi
 
Hali ni nzuri kukiwa na mfumuko wa bei hali ni nzuri wafanyabiashara wakihodhi mafuta na serikali haiwezi sema kitu. Hali ni nzuri gharama za maisha zimepanda thamani ya pesa imeshuka na vipato havijaongezeka mzee upo serious kweli? Kama vipi andika namba za simu na mahali ulipo unastahili teuzi
Wewe nyumbu unaujua mfumuko wa bei kweli? Tanzania Kuna mfumuko wa bei?
 
Wewe nyumbu unaujua mfumuko wa bei kweli? Tanzania Kuna mfumuko wa bei?
Usitumie nguvu kubwa kutaka kila mtu afikiri sawa na mawazo yako. Unajibu kila mtu umeleta uzi soma mawazo ya watu kama hawako sahihi ww jiweke sahihi. Usisahau kuweka namba na mahali ulipo teuzi zipo karibu.
 
Usitumie nguvu kubwa kutaka kila mtu afikiri sawa na mawazo yako. Unajibu kila mtu umeleta uzi soma mawazo ya watu kama hawako sahihi ww jiweke sahihi. Usisahau kuweka namba na mahali ulipo teuzi zipo karibu.
Jibu swali unaelewa maana ya mfumuko wa bei? Vinginevyo tafuta wajinga wenzio ndio mjazane ujinga.
 
Wewe nyumbu unaujua mfumuko wa bei kweli? Tanzania Kuna mfumuko wa bei?
Na sijaongelea mfumuko wa bei tu japo hilo swala lipo na tissii wetu wanatumia nguvu kubwa kunyamazisha watu wasiseme, sijaona ukisema mafuta au nayo yapo mtaani kama kawaida? Uchawa usikupofushe unajimwambafy kwenye jf ukorudi pangoni mwako unalala njaa na vikenge vyako😂😂
 
Na sijaongelea mfumuko wa bei tu japo hilo swala lipo na tissii wetu wanatumia nguvu kubwa kunyamazisha watu wasiseme, sijaona ukisema mafuta au nayo yapo mtaani kama kawaida? Uchawa usikupofushe unajimwambafy kwenye jf ukorudi pangoni mwako unalala njaa na vikenge vyako😂😂
Una akili timamu? Yaani ya Bandari yasemwe ila wewe nyumbu uzuiwe kuzungumzia mfumuko wa bei si ndio?

Nimekwambia tafuta wajinga wenzio mjazane ujinga , I rest my case.
 
Kujenga majumba ni upuuzi,magufuli aliwaambia jengeni viwanda sio majumba Bado mnaakili finyu ndio maana magu anabali akili kubwa TZ. Halipo mpa bakharesa eneo ajenge kiwanda Cha sukari ata yy bakharesa alishangaa lakini Leo si hiyo sukari tunatumia Tanzania nzima naakiuza nje madoka yatakuja,Sasa ayo majumba yenu ata njombe ayafiki pia ayaleti ata Dola
Jifunze kuandika kwanza kijana
 
Hamna lolote mnamfagilia Sana kuliko uhalisia

Amkeni-Ney wa Mitego
Au siyo? Wivu utakuua 😁😁
 
Naendelea kuwakumbusha tuu kwamba miaka 6 ya Uongozi wa Awamu ya 5 sekta ya nyumba "Rea estates" ilidorora,Kudoda na kuporomoka kwa kasi ya mwanga hadi kufikia nyumba nyingi huko Dar kuwa empty na matangazo ya benki kupiga bei nyumba yalijaa mitaani na wanunuzi hakuna sababu uchumi iliporomoka na pesa hakuna.

Aidha bei ya ardhi na nyumba ilishuka na biashara hii kiujumla ilivurugika na ikafikia mahala Ukiwa na kiwanja au nyumba kama dhamana banks zikawa zinakataa au unapewa hela kiduchu.

Ni katika awamu ile ndio Posta Mpya ilibakia magofu huku majumba mengi ya ghorofa yakikosa wapangaji nankubakia tupu.

Ujenzi wa miradi mikubwa ya makazi ulisimama mfano Kawe, Morocco Square, Kigamboni ECO Village, magorofa ya mashirika ya pensions nk, Shirika kama NHC, kampuni za ukandarasi wa majengo zilijifia.

Punde si punde Mungu akasikia kilio akamleta Rais Samia Mama wa Uchumi na Mwanamageuzi wa kweli (Reformists) akapiga chini mipango ya Kijima na Kijamaa kwenye uendeshaji wa nchi, akafungua uchumi na kurekesha Imani ya wafanyabiashara na wawekezaji hatimaye uchumi ukaanza kurejea kule kwa enzi ya Jakaya.

Sasa hivi kwa kutumia mfano mmja tuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC kimeanza tena kupata faida na kufufua miradi yake yote iliyokuwa imekwama.

Hongera sana Rais Samia wewe ndio Mama wa Uchumi unaandika historia na alama ya kudumu kwenye mioyo ya Watanzania maana kila sekta inafurahia uwepo wako.

My Take
Ogopa sana Wajamaa, ujamaa ni umaskini na Utapeli.

=====

View attachment 2707848

Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) limeipongeza serikali ya Tanzania kwa kuimarisha utulivu wa kiuchumi wakati ambapo dunia ilikuwa inapitia changamoto mbalimbali ikiwemo janga la Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO-19), vita vya Urusi na Ukraine na mabadiliko ya tabianchi.

Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa IMF, Bo Li baada ya kumaliza ziara yake nchini ambapo amesema “jitihada za haraka za serikali ya Tanzania zilisaidia kudhibiti mfumuko wa bei na kulinda uchumi dhidi ya athari za vita nchini Ukraine.”

Licha ya mafanikio hiyo, taasisi hiyo imeihimiza Tanzania kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani ambayo yatakuza uwezo wa Serikali katika kugharamia huduma za kijamii na kuongeza uwekezaji katika elimu, afya, maji na sekta nyingine muhimu.

Li akizungumza na wawakilishi wa sekta binafsi, asasi za kiraia na wadau wengine wa maendeleo ameeleza kuvutiwa sana na nguvu na uhai wa uchumi wa Tanzania.

Tanzania ni moja ya nchi chache barani Afrika zenye kiwango cha chini zaidi cha mfumuko wa bei ambapo kwa miezi sita mfululizo umekuwa ukishuka kutoka asilimia 4.9 Januari hadi asilimia 3.6 Juni mwaka huu.

=======
Ujenzi wa Nyumba 560 za mradi wa Samia Housing Scheme, unaoendelea Kawe, Dsm, umefikia ghorofa ya nne kwa ujumla.

Kwa mujibu wa mmoja wa wasimamizi wa mradi huo Mhandisi George Shanel, kinachoendelea hivi sasa #SHS kwa ujuma, ni usukaji wa nondo, maboksi ya kushikia zege (form work), umwagaji zege, nguzo, beam na slabs kutoka ghorofa ya tatu kwenda ya nne.

aidha, ameongeza kuwa kingine kinachoendelea ni ujenzi wa kuta za tofali kwaajili ya kutenganisha vyumba ghorofa ya pili kufuatia kukamilika kwa ghorofa ya kwanza.

Kazi nyingine inayoendelea ni Uwekaji wa mifumo ya umeme na maji ghorofa ya chini (Ground floor), upigaji wa plasta kwenye kuta za ndani ghorofa ya chini (finishing).

Mradi ulianza Oktoba 2022 unatarajiwa kuisha mapema mwakani.


Mama yuko kazini

Haya yoote tunakubalina na wewe, ishu yetu ni moja tu. Mkataba urekebishwe uwe katika mode ya win win situation. Ila ukibaki kama ulivyo, basi uwanufaishe na ndgu zetu wa Zanzibar na bandari zao ziwepo kwny mkataba.
 
Back
Top Bottom