Sekretariati ya CCM ziarani Sumbawanga: Nape aongoza Ujumbe

Magamba at work. Kwani ni mara ya kwanza kusikia bajeti itayoondoa makali ya maisha. Hakuna jipya.
 
mbona kichwa na habari haviendani?tusubiri tusikimbilie kupongeza ahadi kabla ya utekelezaji kwani ni mangapi yalioahidiwa na hayajatekelezwa hadi sasa?
 
Hivi siasa za bongo imekua kushindanisha umati wa watu? Chadema mambo ya kujaza watu hata kwenye kampeni za uchaguzi mkuu ilikua hivyo hivyo mkapigwa!
 
Hotuba ya Nape imenikosha kwani ameelezea mpango mkakati mzuri sana uloandaliwa na CCM ili kuisimamia Serikali wanayoingoza. Hasa pale aliposema hivi sasa wameitaka serikali kuja na Budget itakayoondoa makali ya maisha. Kwa hili tuwapongeze! Angalau wameanza kuonyesha kuwajibika!

WELL DONE Nauye!

Du, hapo kwenye rangi hiyo statement inaonyesha hakuna unachokiamini toka CCM! Kwani kusema ndo kutekeleza? Kama JK mwenyewe alikwisha ahidi mambo mengi, hasa "maisha bora kwa kila mtanzania" na akashindwa vibaya katika utekelezaji, iweje Nape anatumiwa kama "nappy" na CCM kufronza mkojo wa mtoto mdogo?
 
Hivi siasa za bongo imekua kushindanisha umati wa watu? Chadema mambo ya kujaza watu hata kwenye kampeni za uchaguzi mkuu ilikua hivyo hivyo mkapigwa!

Sema CCM ikajitangazia ushindi kwa kuchakachua! Sasa ugumu wa maisha unatukog'oli mimi na wewe unaeshabikia ujinga! Mfumuko wa bei shilingi inaelekea kuwa sawa na toilet paper!
 
Hivi siasa za bongo imekua kushindanisha umati wa watu? Chadema mambo ya kujaza watu hata kwenye kampeni za uchaguzi mkuu ilikua hivyo hivyo mkapigwa!

Kuendelea kujaa watu maana yake ni kwamba wanasikia yale yanayowagusa,ngoja wajiandikishe wote halafu tume ya uchaguzi ihesabu kura bila upendeleo,ndipo utakapojua maana ya kushindanisha uwingi wa watu kwenye mikutano
 
Hivi siasa za bongo imekua kushindanisha umati wa watu? Chadema mambo ya kujaza watu hata kwenye kampeni za uchaguzi mkuu ilikua hivyo hivyo mkapigwa!
Umesahau kwamba shughuli ni watu,kama huna watu utapataje maendeleo na ili tuendelee tunahitaji vitu vinne Watu, ardhi siasa safi na uongozi bora.
 
Nini bajeti tuliambiwa maisha bora kwa kila mtanzania.Matokeo yake maisha yamekuwa magumu maradufu.Sasa hiyo bajeti ya Nape tutakufa
 
Chadema mambo ya kujaza watu hata kwenye kampeni za uchaguzi mkuu ilikua hivyo hivyo mkapigwa!

Una maana wakachakachuliwa? Mwisho wa kuchakachua ni uchaguzi uchaguzi uliopita. Kama mmeweza kuchakachua na CDM wamejifunza sasa tusubiri ngoma uwanjani.
 
View attachment 31294

hii ni babu kubwa
wanakatisha watoto masomo
weraaaaaaaaaaaaaaaaaa

attachment.php



Je huu nao ulikuwa ni mkutano wa CCM au serikali? Kwa nini nyuma ya Nape kuna bendera kadhaa za Taifa?

Nape kweli ana roho ngumu, pamoja na kwamba asilimia kubwa ya wanaomsikiliza ni watoto lakini yeye anatwanga tu. Na sielewi dhamira yake inajisikiaje kuwaona hao watoto wakiwa kwenye mazingira kama hayo baada ya miaka 50 ya uhuru!! Naamini Mzee Nnauye angekuwepo angemcharaza viboko.
 
Ha ha ha ha ha ha nabado 1 ya 10 ya wa2 wa CDM bado niwengi sana!!Siku si nyingi watakuwa wanajihutubia wenyewe,tunawakaribisha ARUSHA,MWANZA.,MARA(TARIME) ndiyo wataipenda
 
Nani anakumbuka huu wimbo aliotunga Mzee Moses Nnauye enzi ya chama kimoja kwenye chipukizi?

1. Chama chetu kimetuongoza, hadi uhuru tulipoupata.
Kinaendelea kuongoza, kufikia lengo ujamaa.
Mwenyekiti Mwl Nyerere, mwenye hekima na wingi wa sifa Tanzania.

Chorus: Ewe chama chombo chetu, madhubuti wa hakika.
Ndiyo wewe nguzo yetu, mwokozi wa Taifa.
Mwenyekiti Mwl. Nyerere, mwenye hekima na wingi wa sifa Tanzania

2. Ulifika wakati mgumu wananchi tulifadhaika.
Utumwa ukoloni ni sumu, wananchi tulihadaika.
Ni wajibu wetu kushukuru, Nyerere alipojitokeza Tanzania.


CCM bado ni hodari kwa kutunga nyimbo lakini siku hizi hazina mvuto huku mtunzi akiwa mwana wa Moses Nnauye.
 
View attachment 31294

hii ni babu kubwa
wanakatisha watoto masomo
weraaaaaaaaaaaaaaaaaa
Hata hao watoto waliowakatiza masomo hawana hata viatu wala uniform unawaeleza nini maisha bora?Naona wameamua kutumia mbinu mpya ili kubana matumizi na kuepuka kuzomewa.Watoto gharama yao ndogo ni pipi tu maandazi au uji ,ukichunguza katika picha hiyo sare za kijani na khanga almost hazipo.MANTIKI YA CCM HAINIINGII KICHWANI MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Hotuba ya Nape imenikosha kwani ameelezea mpango mkakati mzuri sana uloandaliwa na CCM ili kuisimamia Serikali wanayoingoza. Hasa pale aliposema hivi sasa wameitaka serikali kuja na Budget itakayoondoa makali ya maisha. Kwa hili tuwapongeze! Angalau wameanza kuonyesha kuwajibika!

WELL DONE Nauye!
Ujivue gamba kwanza ndio uingie JF PAMBAFFFUUUUU!!!!!!!!!
 
Hiyo picha imechakachuliwa.
Nimeona TBC1 kulikuwa na watu wengi wenye umri mkubwa tena walikuwa wamevaa nguo za CCM. Wengi wa walokuwa wamekaa mbele walikuwa kwenye viti. hivo hiyo si picha halisi ya laela.
tukubali jamaa alipata watu wengi. Sababu ya kupata watu wengi ni kwamba amefanya mkutano wake kwenye eneo la ujenzi wa barabara ya Tunduma Laela ambako watu wamefurahi kupelekewa miundombinu hivyo kuhudhulia kwa wingi wakidhani kuna kingine zaidi ya hiyo barabara.

We huoni aibu kujaribu kuchachua ukweli? Unaambiwa yeye mwenyewe Nape ameipost hiyo picha kwenye face book yake wewe unasemaje picha hii sio halisi? No wonder umejiunga jamvini jana tarehe 30.05.2011 kwa kazi maalumu ya kuchakachua habari!!! Pole

Tiba
 
Back
Top Bottom