SEIF SHARRIF HAMAD Tunasubiri "Plan B" yako

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,715
29,653
Wadau,

Ule uliobatizwa jina la uchaguzi wa Zanzibar ndio huo umeisha na yale yanayoitwa matokeo ya uchaguzi ndio hayo yametangazwa ambapo yamempa Shein Kura 299,000+ (Hizi kura ukijumlisha 20,000 tu zinakua sawa na kura zote walizopata Seif na Shein kwa pamoja October2015). Tumeona ukisusia huu uchaguzi na tumedhani labda wewe uko na Plan B yako baada ya ile ya kwanza ya kutaka Bwana Jecha akutangaze wewe kushindikana.

Hatutaki kuamini kua ndio umeamua kususa moja kwa moja mpaka 2020 utakapofanyika uchaguzi mwengine maana hii litakua kosa kubwa sana kuwaachia hawa CCM kila kitu. Ikiwa ni hivyo ki ukweli tutapata mawazo kua umeamua kuuza Urais kwa Shein na pengine yale yaliyoitwa Majadiliano baina yako wewe pekee kutoka CUF against wajumbe 6 wa CCM hayakukwama kama ulivyotuaminisha, bali yalifanikiwa kwa kuishia kwa wewe kususa kisha kumpa Shein Kijanja. Ila hili hatuliamini, bali tunachoamini ni kua wakati umesusia huu uchaguzi wa Jecha na CCM basi uko na Plan B yako ulioiandaa kuhakikisha kua Mshindi wa halali anatangazwa au uchaguzi wa halali unafanyika.

Tumekaa mkao wa kula kusubiri ukitangaza hiyo Plan B yako Bwana Seif Sharrif Hamad, Katibu Mkuu wa CUF Taifa.
 
kilichonisikitisha ni wale wabunge wa CUF ambao hawataingia bungeni kwa miaka 5, itakuwaje kwa wale wananchi waliowaamini na kuwapa majukumu hayo??
 
Mnachekesha kweli ninyi..

Mtu yupo hotelini anatumbuwa hela alizopewa na Shein alafu wew unaota plan B?
 
Licha ya seif shariff hamad kuwa na plan b pia hadi muda huu ccm hawajui what next na mkwamo wa kisiasa waja.
 
"Hakuna cha plan B...yeye ataendelea na wadhifa wake wa umakamu wa rais....hapo ndiyo utajua ni nini maana ya Tawala"
anasema mnywa viroba namba moja.
 
ZNZ PANA MTEGO MKUBWA SANA LETS WAITS.
Yataka ufungue jicho la tatu ndipo utauona!


Naam

Ndio kwanza jumuiya ya kimataifa inakumbushia kwamba .

Rais magufuli aoneshe uongozi kuutatua mgogoro huo kwa njia za amani na shirikishi

Kwamba uchaguzi utokane na pande zinazohusika na mgogoro wa uchaguzi wa 25 oktoba, 2015 na uwe unawakilisha uhalisia wa wazi wa watu.

Kwa haya ya Jecha ni kana kusema hautambuliwi TUSUBIRI nini kitafuata.

Mimi naona kuna furaha ya muda huku wakisahau mvurugano wa kijamii .

wanasahau umoja kuwa hujengwa wao wanauvunja kwa hila za jecha.
 
"Hakuna cha plan B...yeye ataendelea na wadhifa wake wa umakamu wa rais....hapo ndiyo utajua ni nini maana ya Tawala"
anasema mnywa viroba namba moja.
Sasa yeye hajawa wa Pili, hajapata walau 10% wala hana hata mwakilishi mmoja Zanzibar, atakuaje Makamu Wa Rais??
 
"Hakuna cha plan B...yeye ataendelea na wadhifa wake wa umakamu wa rais....hapo ndiyo utajua ni nini maana ya Tawala"
anasema mnywa viroba namba moja.


Mwaka huu ukishindwa kukiuondowa kiburi cha watawala wa CCM basi ITAKUWA DEMOKRASIA YA WAZUNGU IMEFELI KABISA AFRIKA.
Sitaki kuamini lakini naona mara hii kunaweza kukatoka funzo "Lesson" acha tuone JIPU litatumbukia wapi?
 
"Hakuna cha plan B...yeye ataendelea na wadhifa wake wa umakamu wa rais....hapo ndiyo utajua ni nini maana ya Tawala"
anasema mnywa viroba namba moja.
Sasa yeye hajawa wa Pili, hajapata walau 10% wala hana hata mwakilishi mmoja Zanzibar, atakuaje Makamu Wa Rais??
 
JAPO ZNZ INAJITAPA JUU YA UCHAGUZI HUU WA MARUDIO LAKINI MATAIFA HAYAONI KAMA KUNA JAMBO LOLOTE LIMEFANYIKA, ITS ZERO./ uchaguzi huwa unaheshima take bwana hasa pale ukiwa huru na wa haki!
 
Sasa yeye hajawa wa Pili, hajapata walau 10% wala hana hata mwakilishi mmoja Zanzibar, atakuaje Makamu Wa Rais??
Ukisoma vizuri vile vifungu vya katiba vinavyoelezea nafasi ya umakamu utagundua Rais aliyechaguliwa naweza kumteua yeyote. achana na kile kifungu kinachozungumzia 10%
 
Hii nchI hii imebarikiwa na mungu ukiwa na nia mbaya nayo hili utawale then uwasumbuwe watu wallahi upati hata kama ukiwa ndani ya CCM au mkajiunga vyama vyote hau pati kwa sababu sio msafi
 
Mie sijakusoma kuwa umeandika kitu cha msingi ila naona kuwa ni utumbo tu. Unaelewa nmaana ya kulazimisha lakini au ni kwa sababu nawe unataka usomwe kuwa ni baadhi ya wapuuzi? Kimsingi msimamo wa Seif ni mzuri na kaonyesha kuwa hayuko kimamlahi kama mwenzake Shein aliyetumia mamlaka ya dola kurudi madarakani. Seif katumia utaratibu ya kuwasusia na kamwe hakuonesha kufanya fujo. Sasa wewe unahitaji plan B ya Seif ikusaidie nini na madaraka kawaachia waongoze hata kama ni mawe waongoze tu.
 
Plan B ya CUF hivi sasa ni Press conference ya kila wiki ili kubakia relevant mpaka 2020 na watachochea uvunjifu wa Amani kila baada ya miezi mmine ili wapate nafasi ya kutoka kwenye taarifa za habari wakiilaumu serikali ya CCM ya kuwa inawaonea wapemba lakini hapo hapo vurugu hizo zikitokea tumbatu watasema inawaonea wazanzibar haitokuwa waunguja.na Ikikaribia uchaguzi watakuja na slogan mpya ya Pemba kwanza
 
Back
Top Bottom