Seif Iddi: Uchaguzi wa Zanzibar upo pale pale

Seif Iddi: Uchaguzi wa Zanzibar upo pale pale

Zanzibar ikiripuka huyu idi atasema magufuli ndio anahusika yeye atakataa atasema hajasema haya anayosema
 
huyu ni moja ya wanaccm mahafidhina huko zanzibar. wao wanaamini hakuna mwenye mamlaka ya kutawala zanzibar isipokuwa ni wa kutoka ccm....
 
Narudia Kusisitiza Naiona Zanzibar juu ya Bahari !Nani anajali !!!

wakati Tunasubiri Busara itumike Tuiombee Zanzibar Na Tanganyika ili Tanzania Ibaki sal
 
Hili lijamaa ukiliangalia usoni na maneno yake unaweza ukadhani breakfast yake ni dam za watu.
Na ndicho akitafytacho, huwezi mtu mzima ukawa mropokaji kuvile
 
Makamu wa pili wa Raisi wa Zanzibar, Seif Ali Iddi amesisitiza kuwa uchaguzi wa Zanzibar uko pale pale na kwamba fedha za kugharamia uchaguzi huo zimeshatengwa wanachosubiri ni Tume kutangaza tarehe ya uchaguzi.

Makamu huyo pia amesisitiza kuwa Raisi wa sasa wa Zanzibar ni Raisi halali kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar mpaka pale Raisi mwingine atakapoapishwa.

Katika hatua nyingine,Balozi Seif Iddi amesema Makamu wa Pili wa Raisi wa Zanzibar,Maalim Seif bado anapokea huduma zote za Makamu wa Kwanza wa Raisi.Seif Iddi pia ameongeza kuwa mawaziri wa CUF waliojitoa katika Serikali ya Zanzibar wamejitoa kisiasa tu na si kikatiba.

Hata hivyo,Balozi Seif Iddi amesema, Maalim Seif amekataa kushiriki katika sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kwa kukataa kuzindua shughuli alizokuwa amepangiwa kuzizindua.

Chanzo:ITV

Hivi mwenye Mamlaka Halali ya kusema uchaguzi upo au haupo kwa sasa huko Zanzibar ni nani?

Matamshi kama haya katika ya mazungumzo ya kusaka suluhu ya mgogoro wa Zanzibar yanaleta picha gani?
Eti mazungumzo ya kuleta suluhu....baada ya kushindwa uchaguzi????? We mzee ni mazafanta kweli...
 
Hizi Busara mnazoimba kila kukicha ni ujinga tu
 
Kwa suala la Zanzivar itamlazimu tu Magu atatue mgogoro huo kwa kutumia madaraka yake makubwa aliyopewa kwenye Katiba ya Jamhuri ya.Muungano wa Tanzania ya Uamiri Jeshi Mkuu, kwa kuwa ni dhahiri sasa kutokana na matamshi hayo ya Sefu Idi, hao wahafidhina wa CCM wamepania kuitumbukiza nchi hii kwenye machafuko makubwa.
 
Back
Top Bottom