Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,918
Makamu wa pili wa Raisi wa Zanzibar, Seif Ali Iddi amesisitiza kuwa uchaguzi wa Zanzibar uko pale pale na kwamba fedha za kugharamia uchaguzi huo zimeshatengwa wanachosubiri ni Tume kutangaza tarehe ya uchaguzi.
Makamu huyo pia amesisitiza kuwa Raisi wa sasa wa Zanzibar ni Raisi halali kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar mpaka pale Raisi mwingine atakapoapishwa.
Katika hatua nyingine,Balozi Seif Iddi amesema Makamu wa Pili wa Raisi wa Zanzibar,Maalim Seif bado anapokea huduma zote za Makamu wa Kwanza wa Raisi.Seif Iddi pia ameongeza kuwa mawaziri wa CUF waliojitoa katika Serikali ya Zanzibar wamejitoa kisiasa tu na si kikatiba.
Hata hivyo,Balozi Seif Iddi amesema, Maalim Seif amekataa kushiriki katika sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar kwa kukataa kuzindua shughuli alizokuwa amepangiwa kuzizindua.
Chanzo:ITV
Hivi mwenye Mamlaka Halali ya kusema uchaguzi upo au haupo kwa sasa huko Zanzibar ni nani?
Matamshi kama haya katika ya mazungumzo ya kusaka suluhu ya mgogoro wa Zanzibar yanaleta picha gani?

Last edited: