Tatizo hapa mnafananisha fenesi na shelisheli,jamani uongozi wa chama hauna mipaka ,hauna muda,hauna pingamizi kuwa mtu akishatimiza kukaa katika madaraka ikiwa balozi ,katibu kata au mtungi kwa miaka fulani iwe basi,hilo halipo katika uongozi wa vyama dunia nzima, ondoeni chuki kwa binadamu mwenzenu ,yaani mtu na chama akipendacho,aliishi ccm na uongozi wa juu kabisa na ni kiongozi peke yake ambae aliwahi kuonyesha upinzani ndani ya Chama chake au ndani ya serikali akipingana na viongozi wenzake kwa uwazi kabisa tena kama haitoshi mbele ya Mwalim Nyerere,na kusema kweli Nyerere aliuona ushupavu wa Seif Sharif kwani kabla ya kifo cha Nyerere ,Mwalimu alimwita Seifu Butiama na kumtaka radhi,akimwambia na kumsifu Seif kuwa ni kiongozi wa kweli anaewapenda raia zake.
Seif alisimama mbele ya bunge mbele ya baba wa Taifa la Tanganyika na kumueleza kuwa Zanzibar haitanunua mafuta kutoka Tanganyika kwa fedha za kigeni na ikibidi itatafuta soko liuzalo mafuta kwa bei poa...Jambo ambalo ndilo lilimpandisha hasira Mwalimu ,na kuamua alivyoamua lakini binadamu hukaa na kufikiri na kujuta na Mwalimu Nyerere alikaa na kufikiri na ndipo alipofanya ubinadamu wa kumwita Seif Butiama au hamkumbuki mazungumzo ya private kati ya Mwalimu na Maalim.
Uraisi wa nchi usilinganishwe na uongozi wa chama cha siasa.Kiongozi gani mwengine alietokea kama Seif ndani ya serikali iliyopo ya Tanzania baada ya kifo cha Mwalimu,kiongozi ambae haoni haya kumueleza ukweli mkubwa wake wa kazi ? Zaidi ya kupiga kofi na meza wakionekana wamefurahi kumbe makeke yao nao wamo ndani ya ufisadi.