Seif aahidi Zanzibar kujiunga OIC

minda

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2009
Posts
1,068
Reaction score
67
Send to a friend Wednesday, 06 October 2010 08:31
Bernard Lugongo, Zanzibar

MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia Cuf, Seif Sharrif Hamad,amesema amedhamiria kuvifanya visiwa hivyo kuwa mwanachama wa Jumuiya ya Kimataifa ya Kiislamu (Oic).



"Nikiwa rais, suala la kujiunga Oic ni lazima, ikiwa nchi ya Uganda wamejiunga wakati wananchi wake waislamu ni asilimia 12 tu, iweje sisi tusijiunge wakati waislamu tuko asilimia 97," alihoji Maalim Seif.


"Tutakapoingia katika jumuiya hii, tutapata misaada kutoka katika nchi rafiki za kiislamu," alisisitiza.

Jumuiya hiyo husimamia sauti moja ya Waislamu duniani kote na kuboresha amani katika nchi hizo.

Maalim Seif aliikosoa Serikali ya Muungano kwa kusema kuwa haikuwa haki kutoruhusu Zanzibar kuingia katika mahusiano ya kimataifa.


Source: Mwananchi (picha: zanzinet)
 
Maalim Seif, hoyyyyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!
Hakiiiiii!!!!
Haki sawa kwa nani?
haki sawa kwa wote!!!
Asiyependa haki?
Abaki CCM uko!!!
 
"Tutakapoingia katika jumuiya hii, tutapata misaada kutoka katika nchi rafiki za kiislamu," alisisitiza.

Hapa ndo ninapowashangaa wanasiasa wetu. Hivi anataka kuingia ikulu ya zanzibar ili akawe 'mwombaji' mkuu? Ni 'kansa' hii hii ya 'kuombaomba' ndo inayomfanya JK kuzunguka huku na huko badala ya kufikiria namna ya kujitegemea na hata kusaidia wengine. Hivi watan'zan'ia tumerogwa na nani?
 
Mkuu siyo hivyo unavyodhani, hakuna nchi yoyote duniani hata iwe imeendelea kiasi gani ikawa haihitaji msaada wa nchi nyingine, kumbuka OIC ni jumuiya na siyo nchi moja, na jumuiya ni mkusanyiko wa memba wengi kwa malengo fulani ambayo yanatoa fursa na manufaa fulani kwa wanajumuiya, hivyo, kwa Maalim Seif kusema hivyo anakusudia kuwa fursa hizo zinaweza zikapatikana iwapo tutajiunga na jumuiya kama hizo. Na hili si geni kwani Tanzania ni memba wa jumuiya nyingi tu, unataka kusema inafanya hivyo kwa ajili ya kuomba tu..???
 

Amenukuliwa ifuatavyo:
"Tutakapoingia katika jumuiya hii, tutapata misaada kutoka katika nchi rafiki za kiislamu," alisisitiza.

Mkuu, labda kwa ajili ya mjadala huu tukubaliane kuwa 'misaada' ni synonymous na 'fursa' au penngine tuseme amenukuliwa vibaya! Kwa nini asingesema "tukijiunga na OIC tutaweza 'kutoa' misaada kusaidia nchi rafiki za kiislamu"!
 
Si vibaya kuuliza,naomba tu niulize,tunavyojua nchi yetu haina dini kikatiba na itakapotokea kuwa rais wa nchi ni mkristo au muumini wa dini yoyote isiyo uislamu atakuwa anatuwakilisha vipi kwenye vikao vya jumuia hiyo wakati wenzetu nyinyi tunawajua mnavyokuwa mstari wa mbele kuwaita makafiri wale ambao hawaamini katika imani yenu
 


Mkuu, labda kwa ajili ya mjadala huu tukubaliane kuwa 'misaada' ni synonymous na 'fursa' au penngine tuseme amenukuliwa vibaya! Kwa nini asingesema "tukijiunga na OIC tutaweza 'kutoa' misaada kusaidia nchi rafiki za kiislamu"!
[/QUOTE]
Mkuu labda unge google malengo ya OIC utaelewa kama kanukuliwa vibaya au alichokisema ndicho alichomaanisha hasa, ukiwa memba wa OIC kila memba mwenye uwezo na utaalamu ambao memba mwengine hana anakuwa na uwezo wa kumsaidia memba huyo aidha kwa kuombwa au kwa khiyari yake tu, mfano uwezo wa elimu na tekinolojia...hata hivyo sijaona tatizo hata kama nchi itaomba kusaidiwa mambo ya manufaa kwa watu wake. Hoja hapa ni kujiunga na OIC na si 'utegemezi' au 'omba omba'.
 
..."Tutakapoingia katika jumuiya hii, tutapata misaada kutoka katika nchi rafiki za kiislamu,"...





kwani ni lazima hiyo 'misaada' itolewe na nchi rafiki za kiislamu pindi zanzibar itakapojiunga na oic?
kwa nini isitolewe sasa kwa kuwa licha ya kutojiunga, nchi hizo bado ni rafiki? au ni 'urafiki' wa masharti?
 

seif ndo prezdaa wetu since 1995, mabeberu wanakwepa ukweli tu
 
Inawezekana Seif - kwani sasa hivi Zanzibar ni nchi na ina mipaka yake na mamlaka kamili ya kuweza kujiunga na OIC.
 
ila maalim seif asijiamini sana kushinda urais ikumbukwe kwamba anapambana na home boy.
 
i dont give a shit on whats happening is znz...! provided that Tanganyika is not involved..!

by the way maalim seif anagombea ukuu wa mkoa ..as far as the current constitution is concerned...! URAIS ZNZ NI JINA TU...! PERIOD
!!!!!!!!!!
 
Nadhani kuna maswali kidogo katika huu mtiririko wa hii khabari. Napenda kufundishwa:

Hivi hii OIC imekwisha fanya kitu gani kuimarisha hali za watu wa visiwani? Tunahitaji namba. Je, OIC Imechukua maelekezo gani kulingania jamii zake kuhusu matatizo ya vijana wa kiislam kujiua wenyewe katika nchi zao na zisizokua zao. Hebu tupe list ya nchi zilizo nchi zilizo katika hii Jumuiya ya OIC na malengo yao. Naona imetajwa Uganda pekeyake bora tungejua wote tu, na Jinsi wanavotoaga hiyo misaada inayotafutwa na inakwenda wapi. Yaani sheikh Seif kama kweli amesema hayo maneno, basi maneja wake ndio itakua rahisi kumuuliza utu tumaswali tuwili. Kila kitu tunacho, tunahiji msaada wa akili na maarifa kugeuza hali zetu zamaisha. Hii mambo ya kujigonga, tumeshafanya sana. Hebu tufikieni ufumbuzi sisi wenyewe, mwenye roho ya kusaidia atasaidia, kama alivosema Jenuis. (Viumbe wote wanahitaji msaada, wa namna fulani). Sasa unuaonaje kama Zanzibar ishirikiane na wenzake wa EAC, kisha OIC ikiwa na uwezo wa kusaidia inakaribishwa MWENYE MACHO HAAMBIWI TAZAMA!!!.
 

Mkubwa kweli hii kansa mbaya sana hata mabalozi wetu walio nchi za ulaya na marekani nadhani kazi yao kubwa sio kuhakikisha tunapata masoko yenye bei bora za mazao na bidhaa zetu , sio kuhakikisha tunapata wawekezaji wa kweli bali ni nadhani ajenda kubwa ni kuwa tunapata misaada.
 
Member State
Joined
Notes
Afghanistan 1969 Suspended 1980 - March 1989 Algeria 1969
Chad 1969 Egypt 1969 Suspended May 1979 - March 1984 Guinea 1969
Indonesia 1969
Iran 1969
Jordan 1969
Kuwait 1969
Lebanon 1969
Libya 1969
Malaysia 1969
Mali 1969
Mauritania 1969
Morocco 1969
Niger 1969
Pakistan 1969 Blocking India from membership Palestine, represented by the Palestine Liberation Organisation 1969
Saudi Arabia 1969
Senegal 1969
Sudan 1969
Somalia 1969
Tunisia 1969
Turkey 1969
Yemen 1969 From 1990 as Republic of Yemen united with People's Democratic Republic of Yemen Bahrain 1970
Oman 1970
Qatar 1970
Syria 1970
United Arab Emirates 1970
Sierra Leone 1972
Bangladesh 1974
Gabon 1974
Gambia 1974
Guinea-Bissau 1974
Uganda 1974
Burkina Faso 1975
Cameroon 1975
Comoros 1976
Iraq 1976
Maldives 1976
Djibouti 1978
Benin 1982
Brunei 1984
Nigeria 1986
Azerbaijan 1991
Albania 1992
Kyrgyzstan 1992
Tajikistan 1992
Turkmenistan 1992
Mozambique 1994
Kazakhstan 1995
Uzbekistan 1995
Suriname 1996
Togo 1997
Guyana 1998
Côte d'Ivoire 2001
Suspended or Withdrawn Zanzibar Jan 1993 Withdrew August 1993 Observer States Bosnia and Herzegovina 1994
Central African Republic 1997
North Cyprus as 'Turkish Cypriot State' 1979 Official 2004[clarification needed] Thailand 1998
 
Sitaki kumjua aliyeturoga,kwani nilisikia kuwa alishakufa na kama bado yu hai nikimjua siwezi kumwancha hai tena..duh


 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…