Sehemu za kutembelea hapa Dar

Sehemu za kutembelea hapa Dar

rodreven

Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
61
Reaction score
98
Natumaini wewe unaesoma uzi huu ni mzima wa afya.

Nimekuwa nikikaa hapa Dar kwa muda mrefu kidogo na kumakinika na kazi tu. Hii imekuwa ni 'one way go and return home'. Kwa sasa naona kuna umuhimu wa kutembea sehemu mbalimbali za kutulia na hata kuona jinsi watu wanavyokula maisha hapa Dar.

Kwa hiyo kama kuna anayejua sehemu mbalimbali nzuri iwe ni bichi, klabu, migahawa au mahali mtu anaweza kwenda kutuliza akili kidogo kwa muda na kurudi ambazo zipo hapa Dar. Na hizo sehemu nikienda kutulia hata vinywaji na chakula gharama ya chini iwe 20k.

Kuwe na watu wengi ambao wanakuja sehemu hiyo, muingiliano uwepo kidogo wa watu, hata kukiwa na 'vibe' kidogo sawa kabisa. Eneo na jina la mahali ndicho nachohitaji ili nianze kwenda kupoa siku za wikiendi na siyo kuzubaa tu nyumbani.

Kwa msaada wa google maps yote yanawezekana!
 
Okay itategemea na interests zako. Ila me naweza kukushauri kama unapenda nature, tembelea sehemu hizi:

1. Pugu Natural Forest (Ushoroba) Hii ipo opposite na Minaki Secondary, kwahiyo daladala ni kama 2000/= jumla kutokea Ubungo.
Hapo utaweza kufanya hiking, camping, kuendesha boat, etc.
Gharama jiandae kuanzia 20k hadi 80k kutegemea na huduma.
PXL_20221016_101803597.jpg

2. Vikindu forest reserve. Hii ipo opposite na kiwanda cha juice cha Bakhresa kipo Mbagala kwa mbele nimepasahau jina.
Activities ni sawa kabisa na Pugu hapo namba 1 ila ni cheaper na kasoro hiking hawana milima.

PXL_20220911_120432032.jpg

Me kwa hizo mbili ndio recommend kama mtu wa kurelax mfano na bebe au friends.

Beaches, Malls, na sehemu zingine watakupa wadau.
 
Okay itategemea na interests zako. Ila me naweza kukushauri kama unapenda nature, tembelea sehemu hizi:

1. Pugu Natural Forest (Ushoroba) Hii ipo opposite na Minaki Secondary, kwahiyo daladala ni kama 2000/= jumla kutokea Ubungo.
Hapo utaweza kufanya hiking, camping, kuendesha boat, etc.
Gharama jiandae kuanzia 20k hadi 80k kutegemea na huduma.
View attachment 2390959

2. Vikindu forest reserve. Hii ipo opposite na kiwanda cha juice cha Bakhresa kipo Mbagala kwa mbele nimepasahau jina.
Activities ni sawa kabisa na Pugu hapo namba 1 ila ni cheaper na kasoro hiking hawana milima.

View attachment 2390964

Me kwa hizo mbili ndio recommend kama mtu wa kurelax mfano na bebe au friends.

Beaches, Malls, na sehemu zingine watakupa wadau.
Wooh asante mkuu
Anaetaka twende aje pm
All bills on me
Ila uwe unajitambua
Usiwe mnywa pombe
Silipii pombe mie
 
Natumaini wewe unaesoma uzi huu ni mzima wa afya.

Nimekuwa nikikaa hapa Dar kwa muda mrefu kidogo na kumakinika na kazi tu. Hii imekuwa ni 'one way go and return home'. Kwa sasa naona kuna umuhimu wa kutembea sehemu mbalimbali za kutulia na hata kuona jinsi watu wanavyokula maisha hapa Dar...
Siku ya Jumapili sehemu za kutembelea ni posta, ocean road, tanzanite bridge, oysterbay, masaki, coco beach. Mimi huwa nafurahi kutembea tu kwa miguu maeneo hayo. Siku ya Jumapili posta haina watu kwa sisi ambao hatushindi huko wiki nzima inafurahisha kuzunguka mitaa yake

Masaki, oysterbay kuna mitaa mizuri sisi wa uswahilini inafurahisha kupita mitaa iliyotulia kama hiyo yenye miti mingi na siku hizi kuna pub na vimigahawa vingi.

Hayo ndio maeneo ninayooenda kutembelea mimi na ndio huwa naenda wikendi hasa Jumapili,
 
Back
Top Bottom